Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakati wa Kampeni za Rais wa awamu ya 3 Mjomba Beni Wapinzani nao ilikuwa ruksa kufanyia Mikutano ya Kampeni kwenye Viwanja vya Taifa (now CCM) Nakumbuka Mrema aluvyojaza watu pale Samora.Viwanja vya CCM vingi viligaiwa enzi za Chama kushika hatamu.
Mlijenga nyie au watanzania?Sasa mlitaka Chama tuwe na vyanzo gani vya mapato kama so vile vyote vilivyoanzishwa kipindi cha Chama kushika hatamu..kwa hiyo basi hivyo ni vya wananchi ambao ni CCM wote..ila kama vvipi tugawane kwa kigezo cha population iliyokuwapo miaka ile kabla 1992
Kwi! Kwi! Kwi!Magufuli Akipewa Kuwa M/kiti Wa Chama Kitu Cha Kwanza Kufanya Ni Kurudisha Viwanja Vyote Kwa Umma Wa Watanzania Ikiwezekana Na Miradi Yao Mingine
Kwi! Kwi! Kwi!
Kwa kadiri ninavyojua ccm haijawahi kumiliki kiwanja wala jengo lolote nchi hii .
hapo ni kijana gani kachangia kama si watanzania wote, hata Lowasa wa Cahdema aliwa mwanzilishi wa miradi, Guninita na Sumaye ndio waliokuwa wasimamizi wakuu, pumzika kijana umeishiwa pumzi
hapo ni kijana gani kachangia kama si watanzania wote, hata Lowasa wa Cahdema aliwa mwanzilishi wa miradi, Guninita na Sumaye ndio waliokuwa wasimamizi wakuu, pumzika kijana umeishiwa pumzi
Hukufukuzwa ccm. Kipindi hicho kila raia alikuwa ni raia mzalendo chini ya chama cha mapinduzi. Hukupata kazi bila kujinasibisha na ccm. Hukuingia chuo kikuu bila kuwa sehemu ya ccm. Hivyo ccm ndio ilikuwa yenye mali zinazozalishwa na michango ya wanachama wake. Ukijiondoa katika chama unatoka kwa mapenzi yako hupati ulichochangia kwa sababu haikuwa hisa. Kwa kutambua hilo utakuwa muelewa.Hamashauri na Manispaa mbalimbali, sasa zinataka haki itendeke ili kujiongezea kipato waweze kuhudumia jamii yao kwa miundombinu bora, shule na Hospitali za Viwango vizuri. Ndiyo maana Magufuli aliposhinda Urais walishangilia sana kwani CCM iliwanyanyasa sana kwa kuwanyang'anya haki yao.
Kabla ya vyama vingi, Jamii za kitanzania, walikuwa wanajingoza kwa kujitafuta vyanzo mbadala vya mapato. Walijenga Viwanja vya Michezo, Nyumba za Kupangisha, Maduka n.k. Tena kila mwananchi alishiriki kujenga, eidha kwa kutoa mchango au kutumia nguvu zao kwa amri ya Serikali sio chama.
Mfano, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Meja jenerali Tumainiel kiwelu. Mkuu huyu ndiye aliyetoa wazo la kuujenga uwanja unaoitwa "Nelson Mandela".
Mkuu huyu aliagiza kila mtanzania aliopo mkoani Rukwa Kwa maana ya wilaya zake lazima ashirika ktk ujenzi huo .
Wilaya zilichangisha wananchi wakulima wafugaji watumishi wafanyabiashara n.k michango yote ilipokelewa Na ofisi ya MKUU wa mkoa Kwa udhibiti.
Baada ya hiyo michango ambayo ilikuwa endelevu ikiwa in pamoja Na nyongeza ya bei kwenye bidhaa kama soda via Na mafuta.Ujenzi wa uwanja ulianza Kwa kushirikisha makampuni yote ya ukandarasi yaliyopo mkoa wa Rukwa Na mikoa ya jirani.
Pia aliwaleta wakimbizi wa Burundi waliokuwa kwenye kambi iliyopo katumba mpanda kwani wajenzi wazuri ambao waliweka kambi ndani ya majengo ya Idara ya ujenzi mjini sumbawanga.
Watumishi walikuwa wanashiriki kusogeza Tofari Kwa kila Idara hata watumishi wa afya manesi walishiriki mpaka ujenzi ulipokamilika Na kuitwa "Nelson Mandela Stadium.Pongezi Kwa Mzee wetu shujaa wa Uwanja wa Nelson Mandela Mzee Kiwelu.
Ajabu baada ya vyama Vingi mwa 1992, zilinguvu za Watanzania wakasema zilikuwa nguvu za CCM hivyo Vitu vyote vikarudi CCM. Umma ukabaki mikono mitupu na vitega uchumi vyao vikaanza kuteteleka na huo ndo ukawa Mwanzo wa Umasikini wa kutupwa wa Watanzania walio Wengi.
Na majina walibadilisha sijui wakaita CCM kilumba n.k.
View attachment 355699
Hizi mali za Umma bora Zirudishwe kwa Umma ziendeshwe na ALAT kama vyanzo vyao vya mapato kwani wanafanya kazi nzuri sana.
Mbaya zaidi, Vitega Uchumi hivyo ambavyo CCM walipora, havilipi kodi wala mchango wowote, hata Mwenge ukija wananchi ndio wanachangia.
Nashauri Mali zote ambazo zilikuwa za CCM au kujengwa kwa nguvu ya wananchi au fedha za serikali wakati wa chama kimoja zitarudishwa mikononi mwa umma. Mali walizozipata kwa nguvu ya wana CCM baada ya 1992 zitaangaliwa na kupimwa kuona kama hazikutumia hata shilingi moja toka fedha za umma.
View attachment 355702
Hii itarudisha Imani kwa Wananchi na kuendeleza Mshikamano. Vijana wa chama kimoja walifanya makubwa kuliko vijana wa Sasa. Hawa Vijana wa sasa wanatumia Urithi wa babu tu na kujitapa wana maendeleo wakati waliojenga wapo barabarani Ombaomba wengine Wamewekwa kwenye majumba ya kulelea wazee bila huduma yoyote.
View attachment 355700
View attachment 355701
Waliotumia nguvu zao wakijua zitawasaidia uzeeni, Sasa hivi wanahangaika. Mbaya zaidi wale waliotumia haki yao ya kujiunga na upinzani ndo kwaanza wanaonekana kama hawana haki ya kukaa nchini wala kufaidi Mema ya nchi waliopanda wenyewe.
Kama kulima kote tumelima wote, Hata kupanda Kote tumepanda wote, Kupalilia tumepalilia wote, Aah nashangaa sasa Mbona hatuvuni wote CCM ni nini kimewasibu?
Bado naamini Rais Magufuli akipata uenyekiti atafanya jambo kwaajili ya Masikini waliompigia kura.
Hii itamsaidia pia kutimiza ahadi zake. Ikibidi CCM wapelekwe mahakama za kifisadi. Wamefisadi nchi