Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Saaa ya ukombozi ipo karibu
Tutawanyang'anya vyote wabakiwe na office zao tuu
 
Nikiwa mwanafunzi wa sekondari tulikuwa tunajitolea kujenga uwanja ule kati ya mwaka 1986 hadi 1987 kama maandalizi ya sherehe za miaka 10 ya CCM. Wakati huo nchi ilikuwa na chama kimoja tu, na wote waliojitolea kuujenga uwamnja ule hawakufanya vile kwa vile walikuwa wana CCM kwani hata mimi nilikuwa sijajiunga CCM Kwa nini uwanja uwe mali ya CCM prkrr wakati ulijengwa na watanzania wote?
1986-1987? Umepotea maboya aliyekutuma kakudanganya. Uwanja umekamilika mwaka 1980.
 
Habarini. Suala kama hilo linawezekana? Ni taratibu gani mtu anatakiwa kutuata akitaka kufungua kesi kama hiyo?
 
CCM wanajua ukweli wanakaa kimya!
Siku akipatika Rais/Mwenyekiti jasiri,Viwanja vyote vya mpira vitarudishwa kwenye Halmashauri ili visimamiwe,kutunzwa na kuleta tija.
Tanzania itainuka kimichezo endapo tu viwanja vitarejeshwa,na kukarabatiwa na Serikali
CCM ilifanya dhuluma kuvichukua viwanja,huku ikijua kuwa vilijengwa kutokana na michango ya wananchi.
 
Hivi ni kweli kuwa vile viwanja vya michezo (eg, Kirumba-Mwanza, Majimaji-Songea, Ally Hasan Mwinyi-Tabora etc) ni vya CCM kama wanavyotangaza? Na ni kweli kuwa vilijengwa kwa fedha za CCM?
Sio kweli. Pia kuna majengo mengi tu yanamilikiwa kiharamu na ccm ktk halmashauri mbalimbali. Maeneo ya serikali yaliporwa wafanya biashara wakaambiwa wajenge, halafu wake muda filani bila kulipa kodi, baadae waondoke jengo libakie kuwa la ccm. Huu ni utapeli. Jengo la ccm Kilimanjaro lilijengwa na wananchi kabla ya mfumo wa vyama vingi- wananchi walikatwa pesa zao kwenye mauzo ya kahawa kwaajili ya ujenzi. Baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi ccm wakalipora wakati ni mali ya umma.
 
Back
Top Bottom