Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Tomaa Mireni,Mkuu ni hivii:

Viwanja vyote mfano CCM Kirumba, Uwanja wa Taifa, Sheikh Amr Abeid Arusha, wa Mbeya n.k vilijengwa na Wananchi ambao hawakuwa na fursa ya kuchagua vyama vingine kwasababu hakukuwa na vyama vingi wakati huo.

Kwahiyo si wanaCCM.

Labda hata wasingetaka kuijua CCM ni nini.

Ni kama hizi shule zote nzuri na za zamani zilizojengwa na jumuiya ya wazazi, ambazo CCM wanaziita kuwa ni shule zao.
 
Tomaa Mireni

Ivyo viwanja ni Mali ya CCM kwakua kipindi icho vinajengwa wananchi walikua wana CCM tena kwa Kadi kabisa ilikua kadi ya CCM ni kitambulisho Chako. Sasa vilivyo ingia vyama vingi aliyetaka Kubaki CCM alibaki, aliyeona aitaki CCM alienda kujiunga na chama kinacho Mpendeza. Hivyo viwanja havikua mali serikali kusema vilitakiwa vichukuliwe na serikali.
 
Sasa mkuu wasimamizi wake ni kina nani sasa hivi? Na kwanini wasijjongeze waende na ukisasa
Mkuu ni hivii:

Viwanja vyote mfano CCM Kirumba, Uwanja wa Taifa, Sheikh Amr Abeid Arusha,wa Mbeya n.k vilijengwa na Wananchi ambao hawakuwa na fursa ya kuchagua vyama vingine kwasababu hakukuwa na vyama vingi wakati huo.

Kwahiyo si wanaCCM.

Labda hata wasingetaka kuijua CCM ni nini.

Ni kama hizi shule zote nzuri na za zamani zilizojengwa na jumuiya ya wazazi, ambazo CCM wanaziita kuwa ni shule zao.
 
Ivyo viwanja ni Mali ya CCM kwakua kipindi icho vinajengwa wananchi walikua wana CCM tena kwa Kadi kabisa ilikua kadi ya CCM ni kitambulisho Chako. Sasa vilivyo ingia vyama vingi aliyetaka Kubaki CCM alibaki, aliyeona aitaki CCM alienda kujiunga na chama kinacho Mpendeza. Hivyo viwanja havikua mali serikali kusema vilitakiwa vichukuliwe na serikali.
Sio kweli mkuu viwanja vilijengwa na wananchi bila kujali itikadi zao,watu walichangishwa,mifugo mazao na pesa taslimu watumishi walichangishwa nguvu zao hivyo kusema eti vilijengwa na wanaccm sio kweli.,Hakuna tangazo lolote la ujenzi wa viwanja lililowahi kutolewa na CCM kuwa inajenga Viwanja kama leo Klabu ya Simba ilivyotangazwa.Viwanja ni vya Serikali.
 
Kwa mantiki hii pia hospitali nyingi za mkoa ni mali ya CCM si ndo hivyo?!
 
Mim si lazimishi ivyo viwanja viwe vya CCM ila histolia ya ya ujenzi wa viwanja hivyo ndio inaibeba CCM, inazungumzia itikadi wakati Chama kilikua kimoja yaani CCM ilikua na Nguvu kuliko serikali, Labda nikueleze hivi , Mjumbe wa nyumba kumi ambae kwake kuna pepea bendera ya CCM alikua ananguvu kuliko polisi wa leo. Serikali ya wakati uo ilikua inajua kunasiku vitakuja vyama vingi na CCM inaweza ikatoka madarakan ndio maana ivyo viwanja na baadhi ya majengo yalipewa u ccm.
Sio kweli mkuu viwanja vilijengwa na wananchi bila kujali itikadi zao,watu walichangishwa,mifugo mazao na pesa taslimu watumishi walichangishwa nguvu zao hivyo kusema eti vilijengwa na wanaccm sio kweli.,Hakuna tangazo lolote la ujenzi wa viwanja lililowahi kutolewa na CCM kuwa inajenga Viwanja kama leo Klabu ya Simba ilivyotangazwa.Viwanja ni vya Serikali.
 
Ivyo viwanja ni Mali ya CCM kwakua kipindi icho vinajengwa wananchi walikua wana CCM tena kwa Kadi kabisa ilikua kadi ya CCM ni kitambulisho Chako. Sasa vilivyo ingia vyama vingi aliyetaka Kubaki CCM alibaki, aliyeona aitaki CCM alienda kujiunga na chama kinacho Mpendeza. Hivyo viwanja havikua mali serikali kusema vilitakiwa vichukuliwe na serikali.
Sio kweli hivyo viwanja vilijengwa na wananchi wa Tanzania na si kila mwananchi alikuwa mwanachama wa CCM
 
Iko wazi, tuseme karibu ya Viwanja vyote vya michezo Tanzania vinamilikiwa na CCM, sina shida na hilo...

Shida yangu ni kutaka viwanja hivi vipewe serikali, kupitia halmashauri za wilaya hata ikiwezekana kwa ubia, CCM hawawezi kuviendeleza, srikali ikipewa itaviemdeleza.

CCM ndio inayoshika dola, maendeleo yetu kama nchi tunategemea kusimama na kutekelezeka kwa ilani ya CCM, CCM itoe hata kwa ubia viwanja hivi kwa serikali, vikarabatiwe na wote serikali na CCM watanufaika kwa mapato.

Tukivipata hivi viwanja na vikaboreshwa hata ligi yetu itakuwa ni bora sana, badala ya kujenga vipya vya serikali
Ni wazo jema lakini kwa manyang'au ni vigumu kurejesha mali walizowapora wananchi kwa jina la chama na bado kwa kuwa hawana uchungu navyo wanahiyari viharibike tu!
 
Nzi wa kijani wangese sana, viwanja vimejengwa na wazee wetu Leo wanaviita ccm.
Laanatullah
 
Michango ya Wananchi,CCM wamepora toka kwa Wananchi.
 
Yaani wakati serikali inataifisha makampuni ya wafanyabiashara ambao wanaajiri na hata wengine kubaki hawana kitu na kukimbia nchi hasa wahindi CCM ilikuwa busy kujibinafsisha viwanja!. Sasa ni kwanini hivi viwanja havijawa vya serikali? Mbona wenyewe waliruhusiwa kufanya biashara? tena kwa vitu ambavyo ni vya serikali maeneo ya watu. Itakuwa busara warudishie wananchi wote wa Tanzania viwanja vyao.
 
Una sema FISIEMU au ccm? Hawa ni wazee wa kazi
 
Nikiwa mwanafunzi wa sekondari tulikuwa tunajitolea kujenga uwanja ule kati ya mwaka 1980 hadi 1981 kama maandalizi ya sherehe za miaka 5 ya CCM. Wakati huo nchi ilikuwa na chama kimoja tu, na wote waliojitolea kuujenga uwamnja ule hawakufanya vile kwa vile walikuwa wana CCM kwani hata mimi nilikuwa sijajiunga CCM Kwa nini uwanja uwe mali ya CCM prkrr wakati ulijengwa na watanzania wote?
 
Back
Top Bottom