Watanzania,
Nimekuwa natafakari maono ya TANU na baadaye CCM katika ujenzi wa viwanja vya michezo nchi nzima ni wa kupongezwa na kuendelezwa.
Leo hii karibu katika kila makao makuu ya mikoa kuna uwanja wa michezo ni jambo jema sana kwetu sisi wapenda michezo.Ninakumbuka miaka ya 90 mwanzoni nikiwa nasoma Tabora School mkuu wa mkoa wa Tabora ndugu Lawrence Gama (RIP) alivyosimamia kidete ujenzi uwanja wa Ally H.Mwinyi.
Kumekuwa na malalamiko kuwa CCM wanyang'anywe viwanja hivyo sababu vilijengwa enzi za chama kimoja.Hii hoja haina mashiko kwani leo mtu akihama dhehebu lake huondoka na mgao wa mali kadri alivyochangia?mfano,ukihama ukatoliki utadai mali zako?la hasha utaondika mwenyewe.Na ndivyo ilivyokuwa baada ya mwaka 1992 ilikuwa ni hiyari kuhama CCM hivyo kudai rasilimali za CCM ni ujinga.
Nawatakia jumapili njema