Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Chadema hata banda lao la makao makuu wanashindwa kupiga rangi
 
Nimefuatilia viwanja vya mpira vya CCM Kirumba, Abed Karume Stadium Arusha, Aly Hassan Mwinyi Tabora, Lake Tanganyika Kigoma na vingine vilivyojengwa na wananchi wakati wa mfumo wa chama kimoja na kujiuliza ni lini na ni nani aliviondoa viwanja hivi vya mpira mikononi mwa serikali na kukabidhiwa kwa chama Cha siasa?

Tanzania tuna Wizara ya Michezo na pia tuna shirikisho la mpira ambalo ni mali ya serikali, wakati huo huo chama changu Cha Mapinduzi kimefanya vyema kutaifisha ardhi na mali za umma zilizokuwa zinamilikiwa kinyume Cha taratibu na watu binafsi na Sasa Mali hizo Ni za wananchi.

Nadhani ni muda muafaka Sasa kwa chama chetu kurejesha viwanja hivi mikononi mwa wananchi chini ya Wizara ya Michezo ili viweze kuendelezwa na pia kutumiwa kwa shughuli za wananchi na hivyo kuongeza kipato. Aidha kurejesha viwanja hivi kwa serikali kutatoa tafsiri pana kwama chama chetu kinaheshimu haki na kina wajibu wa kupambana na unyonyaji.......

Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
samora iringa na cha dodoma pia kile cjui kinaitwaje?
 
Viwanja vyote hivi vimeshikiliwa bila ukarabati na vingine kufungwa wakati mikoa husika inazo timu za wananchi hazina maeneo ya kuchezea mpira.Huku nikujilimbikizia mali kusiko na msingi wowote, natumaini katibu mkuu wa CCM na mwenyekiti watalitafakari ili na kuturejeshea viwanja viweze kuendelezwa na kupitia viwanja hivyo pamoja na suala la kulifufua shirika letu la ndege tunaweza kushawishi tupewe nafasi ya kuandaa kombe la mataifa ya afrika ambapo itakuwa njia moja wapo ya kujitangaza kimataifa na kukuza uchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko wazi, tuseme karibu ya Viwanja vyote vya michezo Tanzania vinamilikiwa na CCM, sina shida na hilo...

Shida yangu ni kutaka viwanja hivi vipewe serikali, kupitia halmashauri za wilaya hata ikiwezekana kwa ubia, CCM hawawezi kuviendeleza, srikali ikipewa itaviemdeleza.

CCM ndio inayoshika dola, maendeleo yetu kama nchi tunategemea kusimama na kutekelezeka kwa ilani ya CCM, CCM itoe hata kwa ubia viwanja hivi kwa serikali, vikarabatiwe na wote serikali na CCM watanufaika kwa mapato.

Tukivipata hivi viwanja na vikaboreshwa hata ligi yetu itakuwa ni bora sana, badala ya kujenga vipya vya serikali
 
Baba Jesca kabla hajatoka madarakani hajitahidi awe amerudisha viwanja vyote ambavyo chama chake walijimilikisha kinyume na utaratibu.
 
Ache vikae hivyo hivyo - vikienda serikalini vitauzwa na sisi mambo ya sekta binafsi hatuyawezi
 
Enzi zetu tulikuwa tunacheza biafraa
Sahv kiwanja chichiem wamewaweka watu wa gereji nk, Sahv pale ni vurugu tu.....
Kiwanja kingine cha buibui chupuchupu wakigawe wfanye ujennzi bila kusimama kidete nacho kingeondoka
Kuna watu mule hawafaham umuhimu wa viwanja vya wazi wao ni kuuza tu

Ova
 
Chawa wa kinenani hutoka pale tu unapokwangua kinena chote kwa kutumia wembe "Nacet" halafu umamalizia kwa kinena kusuguliwa na ugoro!
 
Yaani mwizi kaiba tayari mali halafu airudishe kirahisi tu! Labda nchi iwe chini ya uongozi wa serikali nyingine isiyotokana na ccm.

Kama vipi tuwashauri Tff, wadau, timu mbalimbali za mpira wa miguu, Halmashauri, Majiji, Miji, nk wajipange tu kuendelea kujenga viwanja vyao vipya ili kuondokana na hivyo vilivyo kwapuliwa na ccm.
 
Hili lilipaswa kupiganiwa kwa nguvu na watanzania wote wanaopenda maendeleo ya michezo nchi hii
 
Open space zote wamezipangisha hawa
Watoto Hawana hata sehemu za kucheza.....

Ova
 
Labda kama siyo CCM...

Ila vingekua vinashikilwa na chadema sasa hivi zamani washavirudisha serikalini...

Cc: mahondaw
 
Napoitazama ligi ya Tanzania naona naona kichefuchefu napoona viwanja tofauti na taifa.

Viwanja vingi vinaitwa CCM (Mfano Kirumba n.k) Sasa ninachojiuliza, waliojenga miaka hiyo wako wapi sasa hivi? Sijaona ujenzi wa kiwanja kipya Tanzania achilia Taifa na maboresho ya Shamba la Bibi.

Kwanini waliojenga hivyo vya CCM wasijenge vingine vya kisasa kama hivi?
Walijengaje zamani na sasa wameshindwa kuboresha vikawa vya kisasa kama wenzetu?

Karibu tujadiliane hapa kama ikiwezekana tuanzishe kampeni ya ujenzi na uboreshaji wa viwanja hivi.
 
Back
Top Bottom