Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Sasa mlitaka Chama tuwe na vyanzo gani vya mapato kama so vile vyote vilivyoanzishwa kipindi cha Chama kushika hatamu..kwa hiyo basi hivyo ni vya wananchi ambao ni CCM wote..ila kama vvipi tugawane kwa kigezo cha population iliyokuwapo miaka ile kabla 1992
 
Viwanja vya CCM vingi viligaiwa enzi za Chama kushika hatamu.
Wakati wa Kampeni za Rais wa awamu ya 3 Mjomba Beni Wapinzani nao ilikuwa ruksa kufanyia Mikutano ya Kampeni kwenye Viwanja vya Taifa (now CCM) Nakumbuka Mrema aluvyojaza watu pale Samora.
Baada ya hapo ndio Wakajitwalia na Kubadili majina na Viwanja vyote ndani kuna bendera za CCM.
Mwaka 1996 ndio kujitwalia Majengo na Viwanja ndipo kulipoanzia.
Na hii yote walijua wazi endapo wangeshindwa basi wangekosa mahali pa 'kutafuna'.
 
Nimetoa machozi ccm ndio wametufanya Watanzania tuwe masikini.


swissme
 
Mlijenga nyie au watanzania?
 
Hivi sheria imekaaje ktk hili? Haiwezekani kufungua kesi mahakamani? Maana viwanja vyote vya umma vimeporwa na ccm.

Mahakama iwatake sisiem kuonyesha pasipo shaka wapi walipata fedha za kujenga viwanja vyote nchini.
 
Magufuli Akipewa Kuwa M/kiti Wa Chama Kitu Cha Kwanza Kufanya Ni Kurudisha Viwanja Vyote Kwa Umma Wa Watanzania Ikiwezekana Na Miradi Yao Mingine
 
Kwa kadiri ninavyojua ccm haijawahi kumiliki kiwanja wala jengo lolote nchi hii .
 
hapo ni kijana gani kachangia kama si watanzania wote, hata Lowasa wa Cahdema aliwa mwanzilishi wa miradi, Guninita na Sumaye ndio waliokuwa wasimamizi wakuu, pumzika kijana umeishiwa pumzi

na hiii
 
Huu ni utapeli wa waz waz,ni sawa na kuwambia watu wajikusanye kwa ajili ya kulima mashamba kwa faida yao,na wakati wa mavuno hawatambuliki kama walihusika kwenye Shamba husika.
 
Hukufukuzwa ccm. Kipindi hicho kila raia alikuwa ni raia mzalendo chini ya chama cha mapinduzi. Hukupata kazi bila kujinasibisha na ccm. Hukuingia chuo kikuu bila kuwa sehemu ya ccm. Hivyo ccm ndio ilikuwa yenye mali zinazozalishwa na michango ya wanachama wake. Ukijiondoa katika chama unatoka kwa mapenzi yako hupati ulichochangia kwa sababu haikuwa hisa. Kwa kutambua hilo utakuwa muelewa.
Nikupongeze kwa kuleta hoja zilipendwa ili kuondoa sonona kwa wapenzi wa chadema
 
Jana katika baraza la Idi Karimjee,Rais Magufuli alionyesha kuchukizwa na waislam walioshirikiana na matajiri kupora maeneo ya jumuia hiyo.Hilo lilikuwa chukizo zuri sana!

Pamoja na kuwa Rais Magufuli sio mnafiki na anachukizwa na uporaji wa mali za jumuia za wananchi kwenda kwenye vikundi vya watu,nataka kumwambia kuwa kikundi kidogo kiitwacho CCM kilipora na kunyanganya viwanja vilivyojengwa na wananchi!Karibia mikoa yote Tanzania vipo viwanja vya michezo kama Mkwakwani-Tanga,Kambarage-Shinyanga,Al Hassan Mwinyi-Tabora,Kirumba-Mwanza,Jamhuri-Dodoma,nk vilijengwa na wananchi wote kipindi cha mfumo wa chama kimoja.

Tofauti na ilivyokuwa kwa shule za mashirika ya dini kurejeshwa serikalini,viwanja hivyo vikaporwa na chama!!Je,Rais kama mlinzi wa mali za umma,ni lini atatoa tamko juu ya urejeshwaji wa viwanja hivyo?
 
Hoja yako inafanana na ya mwanamke aliyeamua kuachika kwa mume wake kisha akalazimisha kugawana mali walizochuma pamoja ilhali mali hizo zimeandikwa hati ya mume na watoto wake. Ndivyo chadema wanavyofanya. Mali ni za ccm na hati zina majina ya CCM. Msahau kabisa chadema kupata viwanja hivyo. Kama mnashindwa kujenga hata ofisi, mtaweza kumiliki viwanja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…