Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Wenzako walishapeleka mahakamani hilo suala na wakashindwa kisheria. Nenda kakate rufaa
 
mimi nakubali viwanja vya mpira vimejengwa kwa michango ya wananchi kwa sherehe za ccm sasa ili viwanja viboreshwe ni bora muingie ubia makampuni au mwenye uwezo wa kuboresha hivyo viwanja viwanja vingi vimeanza kuchakaa bila huduma yoyote
 
Kama kuna kitu cha kusikitisha, ni hivi viwanja maccm yalivyo vichukua kwa ubabe wao. Tumewazoea wala hatushangai kitu, ila ujue, kwa kuwa vitu vingi walivinyang'anya kwa mabavu, ngalia jinsi ambavyo wanaviacha kuharibika kwa sababu ni mali isiyo na wenyewe tu.
Niliingia katika kiwanja cha Sokoine pale Mbeya. Kiwanja kilikuwa na hadhi ya kipekee katika viwanja vilivyojengwa Tanzania. Sasa hivi, Hakuna huduma yeyote mle ndani. Umeona wapi uanja ka ule, mtu akitaka kujisaidia atoke nje, mpaka kwenda kununua chai hotelini ili ajisaidie?? Nyiye Maccm mnajiaibishaaaa.
Sikieni ushauri; Kodisheni au uzieni watu wenye njuluku zao, wazimwage humo ili virudi kwenye hadhi yake na zaidi. Hamtakuwa mmeishiwa bali mtakuwa mmetumia vizuri resources mlizokwida.
 
Nawaombeni CCM hivi viwanja vya mpira wa miguu ni bora mvibinafsishe.

Nimeona kiwanja cha jamhuri Dodoma hakifai kabisa bora viwanja vya ndondo ni vumbi tupu.

Kiwanja hiki kimezungukwa na maduka makubwa ya vifaa vya ujenzi, sioni sababu kutokuboresha uwanja.
 
Jamal Malinzi kabla hujaondoka fanya kitu hiki.
1.Tumia urais wako kushawishi halmashauri za miji yetu kujenga viwanja vya michezo.
2.Kutoa elimu kwa vilabu vya soka umuhimu wa kuwa na viwanja vyao.
NB: Inatia huruma sna miaka 50 hakuna viwanja bora Tanzania ukitoa wa Taifa. Viwanja vya CCM vitatukwamisha kuandaa hata mashindano ya vijana Afrika.Vilabu au halmashauri zikimiliki viwanja vyao watavitunza sana...
Malinzi jaribu hili wadau tutakukumbuka kwa hilo....najua kujenga viwanja ni harama kubwa laikini ni kitega uchumi cha kudumu.
Miaka 50 viwanja vya mikoani vinachakaa badala ya kuboreka zaidi
 
Rais Kikwete amejipambanua kama Rais mpenda michezo nchini, na ushahidi tunao wa jambo hili. Ninachomuomba Rais Kikwete ni kutumia nafasi yake kama Rais, Mwenyekiti wa CCM na mkereketwa no.1 wa michezo nchini kukishawishi chama chake cha CCM kirudishe kwa TFF viwanja vyote vya mpira wa miguu inavyovishikiria ili kuendeleza mpira nchini. Sitaki kusema wala kuhoji kama viwanja vile ni mali ya nani au vimejengwa na akina nani hapa, ila ninachomuomba Rais auone umuhimu wa TFF kukabidhiwa viwanja vile ili vifanyiwe matengenezo ya mara kwa mara kulingana na viwango vya FIFA.

CCM ni chama kikubwa, hakiwezi kufa wala kuteteleka eti kwasababu kimejitoa kwenye umiliki wa viwanja vya mpira wa miguu nchini. Chonde chonde CCM ya Kikwete fanikisha hili ili umma wa wapenda michezo nchini wakutukuze.
 
ccm imekufa but yu as mbumbumbu yu will neva know. ccm is a dead pat also jk is a dead spiriti
 
Jk anatakiwa kuvirudisha viwanja vyote kabla octoba kabla hajaondoka madarakani
 
Kiuhalisia viwanja vyote hivyo ni wananchi wote maana vilijengwa wakati wa chama kimoja na wananchi wote walishiriki kuvijenga kwa nguvkazi au kodi zao.
 
Kiuhalisia viwanja vyote hivyo ni wananchi wote maana vilijengwa wakati wa chama kimoja na wananchi wote walishiriki kuvijenga kwa nguvkazi au kodi zao.

Kama ni hivyo wachukue basi hata barabara, shule, viwanda, reli, hospitali, mashirika na vitu vyote vilivyojengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja ili waviendeshe wao.
 
Hii ndiyo shida ya kushindwa kupambana na maisha na kutamani vya mwezio.
 
ccm imekufa but yu as mbumbumbu yu will neva know. ccm is a dead pat also jk is a dead spiriti

Mi sio mbumbumbu, CCM ipo, haijafa wacha siasa za kijinga, ina maana wale wanaovaa sare za kijani na wanaoshangalia wakati mgombea wa CCM anapotangazwa mshindi kwenye uchaguzi ni watu wanaotoka kwenye ukoo wenu?
 
Mi sio mbumbumbu, CCM ipo, haijafa wacha siasa za kijinga, ina maana wale wanaovaa sare za kijani na wanaoshangalia wakati mgombea wa CCM anapotangazwa mshindi kwenye uchaguzi ni watu wanaotoka kwenye ukoo wenu?

narudia ww ni mbumbumbu ccm hawajawahi kushinda uchaguzi isipokuwa wao kutangazwa viongozi. familia yangu haiwezi kuwa kwenye ukoo wa panya. slaa pekee atarudisha viwanja si mwingine. umelewa?
 
narudia ww ni mbumbumbu ccm hawajawahi kushinda uchaguzi isipokuwa wao kutangazwa viongozi. familia yangu haiwezi kuwa kwenye ukoo wa panya. slaa pekee atarudisha viwanja si mwingine. umelewa?
Kwahiyo wanaovaa sare za CCM zenye picha ya Rais kifuani tunaowaona mitaani ni UKAWA? wewe ni mbumbumbu wa siasa. Ukijamba kwa hasira unaweza kujichafua mwenyewe.
 
mitaaa gani labda bwagamoyo ndo wanakovaa. ila cyo kwa wajanja. kikwete kafanya nn kwenye michezo?
 
Inasikitisha CCM kuwa na viwanja vibovu kama Mkwakwani, Sheikh Amri Abeid na vinginevyo.

Hebu muingie ubia na wadau wengine wa soka kama mlivyofanya na Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine ili vikarabatiwe.

Mbona mnaakili mgando mnamatatizo gani
 
Kuna viwanja kama sokoine Mbeya na Kirumba Mwanza. Hivi viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na wananchi wote. Vilipokuja vyama vingi wengine wakatoka CCM na walipaswa kupata mgawo wa mali hiyo. Pia wengi walioshiriki ujenzi hawakuwa hata na kadi. Ni wakati wa hawa jamaa kurudisha mali kwa wananchi.

Pia kuna shule za wazazi na viwanja vya sabasaba. KAMA KUNA MALI YA WANANCHI AMBAYO UNAJUA CCM WANAJIMILIKISHA ITAJE HAPA
 
Hili suala ni gumu ccm wakiwa bado madarakani. Wameharibu mhimili wa mahakama kwa kuweka watu wao. Kuna majaji wamepewa kiushikaji na wanajua hawastahili. Kwa hiyo hili suala lina nafasi ndogo sana. Ndio maana Kenya walisafisha mhimili wa mahakama baada ya kupata katiba mpya. Majaji na mahakimu wafawidhi wengi walistaafishwa. Ilikuwa sehemu ya kutekeleza katiba hiyo.

Nikirudi kwenye maada, tusubiri ccm ing'olewe ndio tuanzishe huu mjadala. Viwanja vyote ccm Kirumba, Sokoine Mbeya, Majimajo Songea nk vimilikishe kwa halmashauri husika maana ni mali za wananchi wote. Viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na rasilimali nyingi za serikali zilitumika.
 
Back
Top Bottom