Kama kuna kitu cha kusikitisha, ni hivi viwanja maccm yalivyo vichukua kwa ubabe wao. Tumewazoea wala hatushangai kitu, ila ujue, kwa kuwa vitu vingi walivinyang'anya kwa mabavu, ngalia jinsi ambavyo wanaviacha kuharibika kwa sababu ni mali isiyo na wenyewe tu.
Niliingia katika kiwanja cha Sokoine pale Mbeya. Kiwanja kilikuwa na hadhi ya kipekee katika viwanja vilivyojengwa Tanzania. Sasa hivi, Hakuna huduma yeyote mle ndani. Umeona wapi uanja ka ule, mtu akitaka kujisaidia atoke nje, mpaka kwenda kununua chai hotelini ili ajisaidie?? Nyiye Maccm mnajiaibishaaaa.
Sikieni ushauri; Kodisheni au uzieni watu wenye njuluku zao, wazimwage humo ili virudi kwenye hadhi yake na zaidi. Hamtakuwa mmeishiwa bali mtakuwa mmetumia vizuri resources mlizokwida.