Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Hili swala linaniumaga sana,kesho nitakuja kulijadili vizuri hili swala,ila kwa sasa niacheni nipumzike na wifi yenu
 
Huu ni upuuzi kutafuta njia za mkato kushiriki michuano ya kimataifa
 
Wadau pamoja na maswali mengi ninayojiuliza juu ya vyanzo vya mapato vya CCM na uhalali wake hili nalo linanipa utata, labda mnisaidie japo hili moja sababu karibu viwanja vyote vikubwa tulivyo navyo mmiliki ni CCM,

Nauliza tu; Ni nani aliwamilikisha CCM viwanja vyote hivi na alitumia vigezo gani? (Maana nimefuatilia sijaona hata kimoja walichojenga kwa hela ya chama, vyote naambiwa vilikuwa vya umma)
 
kikitawala chama kingine kitavichua vyote viwe vyake ndio utaratibu usiokuwa rasmi
Uadilifu wa ccm na mwelekeo wake juu ya ufisadi ndio maana unatiliwa shaka kwa maana hivi viwanja na mali zingine za umma walivipora kwa nguvu na wala hawakumilikishwa. Kuna tume halali kabisa ya kijaji ilibainisha jinsi hivi viwanja na mali zingine zilivyo mali za umma na sio chama lakini wakaiweka kapuni.
Nianachoweza kukuhakikishia mkuu gogo la shamba, sio mpaka watawale chama kingine bali hata hawa hawa waliopo wakipatikana wabunge kama 50%+ ambao IQ zao zinakaribia 30 basi wanaweza kusimamisha muswada na mali hizi zikarudishwa (sio kwa cdm wala cuf) bali umma kupitia halmashauri za maeneo hivyo chama chochote kitakachoshinda hapo ndicho kitazisimamia!
Kibaya kabisa hata maeneo yaliyokuwa ya wazi katika master plans za miji waliyashikiria na kuyauza kinyemela kwa 'wahalifu' wengine na yamejengwa kiasi kwamba hata pa kuchezea watoto au recreation centres zimepotea kwa zaidi ya 80%.

 
hayo yote yanafahamika hata walioiba Escrow wanafahamika ila hatuna serikali ya kuchukua hatua kaka, wewe ushangai waliomuua mwangosi wanaonekana wazi kwenye picha jinsi walivyomuua lakini mpaka leo hakuna chochote,hii ni serikali kandamizi la muhimu ni kuiweka pembeni kwanza alafu lianzwe moja baada ya moja
 
Hivyo viwanja ni vya serikali. Si viwanja tu, ni pamoja na majengo mengi ambayo leo ccm inayaita ccm mikoa. Serikali ya UKAWA inayachukua kwa matumizi ya serikali. Viwanja vitafanyiwa taratibu kama zilivyo raslimali zingine za uma.


Ccm wapangaji. Wajiandae kulilpa kodi, au kushindana kwenye kuvinunua kutoka serikalini kwa utaratibu wa tenda maalumu kama serikali itaazimia kuviuza.

Ccm wanaweweseka na mauza uza kwa sababu nyingi!.
 
vuta subra kidogo sana mkuu , siyo viwanja tu , hata majengo waliyojimilikisha kijanja kama jengo la uvccm na ofisi ndogo lumumba , hivi vitarejeshwa kwa wenyewe wananchi kabla ya january 2016 .
 
hayo yote yanafahamika hata walioiba Escrow wanafahamika ila hatuna serikali ya kuchukua hatua kaka, wewe ushangai waliomuua mwangosi wanaonekana wazi kwenye picha jinsi walivyomuua lakini mpaka leo hakuna chochote,hii ni serikali kandamizi la muhimu ni kuiweka pembeni kwanza alafu lianzwe moja baada ya moja
nimeshindwa kujizuia , andiko lako limeniporomosha machozi !
 
Hana msimamo huyo! Na watu wanafki kama hao hatuwataii na ni Afadhali kabisa alivyjitoa mwenyewe.
 
Hivi hiki chama kilikua na vyanzo gani vya mapato mpaka kuviwezesha kujenga viwanja vingi hivi?mfano Sheikh Amri Abeid Arusha,Umoja Mtwara,CCM kirumba,Sokoine nakadhalika?
Au ndio chama kilichukua faida ya "chama kushika hatamu" katika awamu ya kwanza?

Nini itakua hatma ya viwanja hivi siku hiki chama kikiwa cha kipinzani?
 
ccm haijawahi kutafuta fedha ya kujenga chochote achilia mbali viwanja vya soka , kabla ya january 2016 kila kilichoporwa kitakuwa nikononi mwa wenyewe wananchi tena , shaka ondoa .
 
Ccm haina viwanja niwakora tu.

Viwanja hasa vya michezo nimali ya raia wa tanzania.

Tulishiliki bega kwa bega sisi sote kabla ya ujio wa vyama vingi.
 
Na kwa uhakika wabunge wetu wa upinzani inabidi 2015 -2020 mdai asset zetu zote ziliibwa na CCM kwa kisingizio cha chama kushika UTAMU,warudishe
 
ni hoja muhimu na ya msingi mno kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya nchi yetu,ccm bila aibu wala hiyana wamekwiba hivi viwanja na najengo mengine mengi tu hapa nchini kwa faida yao na vizazi vyao,sasa wakati umefika kudai waturudishie mali zetu kwa manufaa ya taifa zima bila kujali itikadi yoyote kwa sababu viwanja hivi vilijengwa kwa ajili ya taifa letu sote..!!
 
Back
Top Bottom