Lissu aanza mgomo wa kula. CHADEMA yasema mawakili wake wamezuiwa kumwona gerezani

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, ameanza mgomo wa kula kuanzia Oktoba 26, 2026, huku chama hicho kikilalamikia kuzuiwa kwa mawakili wake kumwona gerezani.

Hatua hiyo inafuatia taarifa iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Dk Rugemeleza Nshala Oktoba 24, kuwa kiongozi huyo alipinga kuzuiwa kuzungumza na mawakili wake kwa faragha kama ilivyoelekeza amri ya Mahakama iliyotolewa Oktoba 16, baada ya mawakili wa Lissu kufungua kesi.

Soma pia: Mawakili wa Lissu waibuka kidedea, Gereza la Ukonga lapewa maagizo

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia Oktoba 26, 2026, CHADEMA imesema hatua hiyo inakuja wakati haki ya Lissu kupata msaada wa kisheria, mawasiliano na uwakilishi wa mawakili wake ikiendelea kuwa suala la wasiwasi.

Soma zaidi: Lissu atangaza mgomo wa kula chakula kuanzia Jumatatu, 26/10/2026

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mawakili wa Lissu, Dickson Matata, Doris Kafuku na Neema Massame, walikwenda gerezani kwa lengo la kumwona na kuwasiliana naye, lakini walizuiwa kuingia.

CHADEMA imesema hali hiyo inazua maswali kuhusu upatikanaji wa huduma za kisheria na namna haki za Lissu zinavyolindwa akiwa gerezani.

“Tunazitaka mamlaka husika kuhakikisha mawakili wake wanaruhusiwa kumwona bila vikwazo visivyo na msingi wa kisheria, na kuchukua hatua za haraka kulinda usalama na ustawi wake,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Chama hicho kimeongeza kuwa kinafuatilia kwa karibu hali ya Mwenyekiti wake na kitaendelea kuujulisha umma kuhusu maendeleo ya suala hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA.

HVlJqo4WQAAajG5.jpg
 
Hiyo kesi kajitetea mwenyewe;

Mawakili wa nini.

Atakufa njaa kudai mawakili wakati nae wakili.
Mawakili si kwa ajili ya kesi iliyopo mahakamani pekee, Haki, wajibu na sheria havisimami mtu anapokua mahabusu. Sio kila jambo la kutetea, inakuwa kama uchawa sasa, yaani unapingana mpaka na mahakama ambayo ndo mhimili wa haki, kesho wewe ukiwa mahabusu?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, ameanza mgomo wa kula kuanzia Oktoba 26, 2026, huku chama hicho kikilalamikia kuzuiwa kwa mawakili wake kumwona gerezani.

Hatua hiyo inafuatia taarifa iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Dk Rugemeleza Nshala Oktoba 24, kuwa kiongozi huyo alipinga kuzuiwa kuzungumza na mawakili wake kwa faragha kama ilivyoelekeza amri ya Mahakama iliyotolewa Oktoba 16, baada ya mawakili wa Lissu kufungua kesi.

Soma pia: Mawakili wa Lissu waibuka kidedea, Gereza la Ukonga lapewa maagizo

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia Oktoba 26, 2026, CHADEMA imesema hatua hiyo inakuja wakati haki ya Lissu kupata msaada wa kisheria, mawasiliano na uwakilishi wa mawakili wake ikiendelea kuwa suala la wasiwasi.

Soma zaidi: Lissu atangaza mgomo wa kula chakula kuanzia Jumatatu, 26/10/2026

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mawakili wa Lissu, Dickson Matata, Doris Kafuku na Neema Massame, walikwenda gerezani kwa lengo la kumwona na kuwasiliana naye, lakini walizuiwa kuingia.

CHADEMA imesema hali hiyo inazua maswali kuhusu upatikanaji wa huduma za kisheria na namna haki za Lissu zinavyolindwa akiwa gerezani.

“Tunazitaka mamlaka husika kuhakikisha mawakili wake wanaruhusiwa kumwona bila vikwazo visivyo na msingi wa kisheria, na kuchukua hatua za haraka kulinda usalama na ustawi wake,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Chama hicho kimeongeza kuwa kinafuatilia kwa karibu hali ya Mwenyekiti wake na kitaendelea kuujulisha umma kuhusu maendeleo ya suala hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA.

View attachment 3699443
Nilishauri kwa vile hukumu very soon inatoka, ahairishe mgomo tusikilizie hukumu!
 
mawakili gani hao?
mbona Tundu Lisu hakuwahi kua na mawakili, wala hakuna wakili alie kua akimtetea mahakamani, na hata mashahidi wake tu aliamua kuwaweka viongozi vilaza wa chadema kwa kujimwambafai tu, tena wasio wanasheria na kumdharau hata mwanasheria mkuu wa chama chake mwenyewe, sijui anaitwa wakili nani sijui yule.

Dunia nzima inajua Tundu Lisu hakua na wakili wa kumtetea na alijitetea mwenyewe mwanzo mwisho hadi mwisho wa kesi yake ambayo hivi sasa inasubiri hukumu tu. Acheni unafiki.

Ni vizuri Tundu Lisu na chadema kwa ujumla wake wakaacha porojo, uongo na upotoshaji useless wa hadharani kama huu na itapendeza zaidi.

Kutafuta kiki na public sympathy nonsense namna hii ni vitu useless sana aise 🐒
 
Mwambieni ale ugali hakunaga shujaa aliyefia jela. Na akumbuke kufia jela ni kuwapa ushindi maadui zake. Yaani ushinde shambulio la risasi Zaid ya kumi mwilini alafu uje ufie jela kwa kugoma kula this is bady idea
 
Hiyo kesi kajitetea mwenyewe;

Mawakili wa nini.

Atakufa njaa kudai mawakili wakati nae wakili.
ni mnafiki sana huyo jamaa aise,
dharau zake dhidi ya mawakili tangu mwanzo wa kesi zinamuumbua na kumuathiri vizuri sana hivi sasa.

ni muhimu sana,
wacha tumshuhudie mtu aliekaa na njaa wiki nzima kwa makusudi anafananaje nadhani itapendeza zaidi 🐒
 
mawakili gani hao?
mbona Tundu Lisu hakuwahi kua na mawakili, wala hakuna wakili alie kua akimtetea mahakamani, na hata mashahidi wake tu aliamua kuwaweka viongozi vilaza wa chadema kwa kujimwambafai tu, tena wasio wanasheria na kumdharau hata mwanasheria mkuu wa chama chake mwenyewe, sijui anaitwa wakili nani sijui yule.

Dunia nzima inajua Tundu Lisu hakua na wakili wa kumtetea na alijitetea mwenyewe mwanzo mwisho hadi mwisho wa kesi yake ambayo hivi sasa inasubiri hukumu tu. Acheni unafiki.

Ni vizuri Tundu Lisu na chadema kwa ujumla wake wakaacha porojo, uongo na upotoshaji useless wa hadharani kama huu na itapendeza zaidi.

Kutafuta kiki na public sympathy nonsense namna hii ni vitu useless sana aise 🐒
Unabishana na Amri ya mahakama?Wewe si ndio ambaye umekuwa Ukisema mahakama zetu ni huru na zinatenda haki?Haya ndio imempa haki ya kuonana na mawakili wake!
Mbona mnajizima data?
Mahakama ndio ilitakiwa iseme hana wakili,sio wewe!
 
amri ya mahakama haijasema mtuhumiwa wa uhaini anaesubiri hukumu na ambae hakua na wakili hata moja na ambae alijitetea mwenyewe mwanzo wa mwisho wa kesi yake aruhusiwe kuonana na mawakili ambao hakua nao kabla.

hakuna amri kama hiyo.

baada ya hukumu,
mawakili wanaweza kuruhusiwa kuonana nae kwaajili ya kesi zake zingine zinazomkabili ikiwa hatua ya kunyongwa itakua bado 🐒
 
Ni wapi mahakama imesema baada ya hukumu?Acha kujizima data,na kwanini kule magereza walisema wana Nia ya kukata rufaa ila utaratibu utabaki ule ule?
Kwamba mawakili wake wamuone ila hawatapewa faragha!

Kama ni hivyo,wangezuiwa kabisa kumuona baada ya hiyo hukumu!Haikuwa hivyo,waliruhusiwa kumuona ila mbele ya maafisa maalumu wa magereza!
Hii maana yake,magereza wanatambua haki yake ya kuonana na mawakili wake ili wamegomea suala la faragha ambalo ndio kesi aliyoshinda!
Hata kujua kuwa ameanza mgomo wa kula,ni baada ya kuonana na mawakili wake na kunyimwa faragha!Ndio akawaambia mawakili wake kuwa amedhamiria kuanza hunger strike ili hukumu yake izingatiwe na magereza!

Acheni kujizima data!
 
relax gentleman,
hujui sheria bana 🤣
 
Kisayansi kwa Mwanaume ni siku 7 tuu so Next monday tutajua kama kafa au lah R.I.P
 
Back
Top Bottom