Pre GE2025 Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa kama ni hivyo unavyo fikiria wewe, tatizo liko wapi?
Kwa vile watu anaohutubia watamwona kuwa na sifa hizo unazodai, si hiyo ndiyo itakuwa nafuu kwenu, au unatakaje?
Cheap politics Kwa kiwango Cha elimu aliyonayo hakitendei haki kiwango chake Cha elimu
 
Abdul naye anaweza kutoka hadharani na kusema Lissu aliniomba rushwa nikamkatalia.

Sasa tutamuamini nani?.

Watanzania tuanze sasa kufikiri Kwa nguvu tuache hizi siasa holelaholela na oyaoya.
 
Kujulikana sana sio sifa kuwa uko Vizuri sana kichwani

Mfano hakuna mtanzania asiyejua mnyama aitwaye Mbwa

Lakini mbwa hajawahi kuwa mwanasiasa Wala kuhutubia popote na hatarajii lakini anajulikana sana
Kitendo cha kuwafanya watu wawe wanakukubali na kukushabikia ndiyo akili yenyewe hiyo. Au unadhani akili ni kukariri maandishi peke yake? Akili ni jambo Pana sana.
 
nahisi tundu lisu ni timu makamba, rostamu &Co. raisi samia haendelei 2025 na ana wa kumwachia tayari, makamu wake na hilo wanalijua, tifu lote liko hapo kwani itavuruga kila kitu mpaka 2025/35 …
Timu Makamba ndiyo inamtuma Abdul kutembea na makapu ya fedha kujaribu kuhonga watu?
 
Kitendo cha kuwafanya watu wawe wanakukubali na kukushabikia ndiyo akili yenyewe hiyo. Au unadhani akili ni kukariri maandishi peke yake? Akili ni jambo Pana sana.
Washabakia halafu kura hawampigii akili hiyo? Akili ni kutafuta wapiga kura watakaokupigia kura sio washabiki
 
Unasubiri nini kumburuza?
 
Cheap politics Kwa kiwango Cha elimu aliyonayo hakitendei haki kiwango chake Cha elimu
Dah!
Mkuu 'Shotocan', mbona unachanganya. Dakika chache tu zilizopita ulieleza hata ile elimu ya "law class 101 hana"..., na sasa hapa unasema kinyume chake!

Hapana. Ni hivi, mimi nakuelewa unachogombea; na ili uweze kukieleza vizuri jaribu kuelewa anachosema Lissu, na kwa nini anakisema hivyo. Ukimwelewa vizuri, utapata njia nzuri ya kukabili hoja zake unazoziona hazifai.. Lisu analo lengo la kufanya anavyofanya. Hilo ndilo unalopaswa kulijuwa.
 
ulitaka achezi na siasa za namna gani wakati siasa zina angle nyingi za ku focas? Mbona anafanya siasa vema tu, umeambiwa akina ally hapi waliingia mpaka msikitini kufanya siasa na haitakiwi kufanya siasa kwenye nyumba za ibada za kidini, hiyo yote ni kutaka simple winning situation japo si nzuri kufanya siasa misikitini
 
Wewe umejuaje ni uongo?....
 
Umemsikiliza?
 
Lissu aache siasa za kitoto aweke ushahidi wa kufikiwa na Abdul na kutaka kuhongwa, lakini pia apeleke TAKUKURU Ili wachukue hatua
Yaani wewe badala ya kuwaona Abdul na Mama yake kuwa ni wajinga wa mwisho, unalalamika upewe ushahidi wewe?

Kwanza walifikiria nini kumwa - approach Tundu Lissu kwa rushwa huku wakijua kabisa kuwa watapasuliwa mchana kweupe??

Inashangaza kuwa wewe hapa unaomba ushahidi? Seriously? Na eti unasema nini? Awapelekee TAKUKURU iliyo na mteule wa Mama Abdul?

Ndugu hiyo ni silaha ya kuwamaliza kisiasa Abdul mwenyewe na Mama Abdul kwa wao kuitoa hiyo silaha kwa hiari yao wenyewe..

Kasemwa Abdul hapa. Mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Yeye ndiye anayepaswa kushitaki kusingiziwa Ili ushahidi ukatolewe huko mahakamani.

Na nadhani humjui Tundu Lissu wewe. Unadhani ni huyu mwamba ni mtu wa kukurupuka tu kusema wazi jambo zito kama hili la kumtuhumu mtu?

Na unadhani ni kwanini ile "Nissan nyeupe" imeanza kumfuata kila anapokwenda tena?

Hawataki aseme anavyosema Ili umma ujue!!
 
Aliyekwambia Tundu Lissu anachoka ni nani?

This man is Gifted.

Aliweza kufanya mult task na aka perform kwa weledi mkubwa sana at same time akiwa
1. Wakili mahakama Kuu
2. Mkurugenzi wa Sheria Chadema
3.Mnadhimu Mkuu Kambi Rasmi Bungeni
4. Rais wa TLS
5.Mbunge wa Jimbo wa kuchaguliwa
6. Mtetezi wa Kesi za Wanyonge zisizopungua 50 kila mwaka.

Ukitazama namna anavyogawa muda wake huku akiwa Mbunge bora mwenye taarifa za ndani za kila Hoja utashangaa sana
 
Kwa kawaida Mwanasheria anapokuwa anazungumza jambo lo lote huwa analizungumza kwa tahadhari kubwa lisije kumbana ikitokea amefikishwa mbele ya vyombo vya Sheria!
Sasa hapo huyo Abdul ajitokeze kumshitaki kuwa amemsingizia uongo usikie kesi itaishaje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…