Lissu amtetea Job Ndugai, asema lazima kuna jambo

Lissu amtetea Job Ndugai, asema lazima kuna jambo

Uzuri mmoja kuhusu Lissu jamaa ni mkweli sana kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi hata uwe adui yake ukionewa atakutetea. Na hii ndio aina ya viongozi ambao hatuna Afrika.

Kwa vitu alivyofanya Ndungai kwa Lissu kwa mtu mwingine angekuwa amepata pa kumpigia angempolomoshea kila aina ya matusi.
Moja wa wanasiasa wachache wa Tanzania wanaojielewa
 
Mimi sijawahi kuungana na hizo taka ngumu toka CCM wakati wowote. Huyo Ndugai alikuwa anaongea kwa sifa kabisa ili kukomoa wapinzani. Wakati ule wa siasa za kishenzi alikuwa anaona fahari sana kunyanyasa wapinzani. Sio kila mtu anaweza kumkubali shetani na mambo yake. Isitoshe kaikana kauli yake na kuomba msamaha. Mwambie ajitokeze asimamie hoja yake tumuunge mkono.
Wewe umekanyagwa kuliko Lisu?

Kwa nini Lisu kaona hoja kwa Ndugai ila nyie wafuasi mnamshambulia ndugai na kuacha hoja yake?

Hoja ya Ndugai ndio imemfanya mama apanic namna ile!

Tungekuwa na akili tungamuunga mkono Ndugai kama alivyofanya Lisu
 
Lisu kaongea vizuri sana kwamba kaomba msamaha sababu yeye ni ng'ombe tu kwa mama!

Ila ujumbe wake uko clear!

Tungekuwa na akili tungeungana na Ndugai bila kujali madhaifu yake!

Mbona tuliungana na Nyarandu, Lowasa na kina Sumaye?
Kweli kabisa... Chadema tukitaka kushinda uchaguzi, tumkaribishe ndugai agombee 2025[emoji1745]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Uzuri mmoja kuhusu Lissu jamaa ni mkweli sana kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi hata uwe adui yake ukionewa atakutetea. Na hii ndio aina ya viongozi ambao hatuna Afrika.

Kwa vitu alivyofanya Ndungai kwa Lissu kwa mtu mwingine angekuwa amepata pa kumpigia angempolomoshea kila aina ya matusi.
Hapa hiyo nyeupe ilienda wapi?
20211028_123608.jpg
 
Wewe umekanyagwa kuliko Lisu?

Kwa nini Lisu kaona hoja kwa Ndugai ila nyie wafuasi mnamshambulia ndugai na kuacha hoja yake?

Hoja ya Ndugai ndio imemfanya mama apanic namna ile!

Tungekuwa na akili tungamuunga mkono Ndugai kama alivyofanya Lisu
Ndungai ni kama walivyo CCM wengi tu hawana political legitimacy ya kukosoa utawa kwasababu wao pia walitenda hayo hayo walipokuwa na nafasi.

Mfano Polepole alipoitwa TCRA analalamika amesahau kuwa yeye aliwahi kuzima mitandao kabisa ili watu wasipate taarifa.
 
Wewe umekanyagwa kuliko Lisu?

Kwa nini Lisu kaona hoja kwa Ndugai ila nyie wafuasi mnamshambulia ndugai na kuacha hoja yake?

Hoja ya Ndugai ndio imemfanya mama apanic namna ile!

Tungekuwa na akili tungamuunga mkono Ndugai kama alivyofanya Lisu

Lisu amuunge mkono kimpango wake. Mimi huwa siungi mkono mabazazi wa aina ya Ndugai, na sifanyi maamuzi kwa kusubiri mtazamo wa Lisu.
 
Sioni kosa la ndungai kama spika wa bunge . Wenye kazi ya kuisimamia kushauri na kuikosoa serikali alifanya kazi yake tatizo labda ni right thing wrong place angeyaongelea bungeni.
 
Lisu amuunge mkono kimpango wake. Mimi huwa siungi mkono mabazazi wa aina ya Ndugai, na sifanyi maamuzi kwa kusubiri mtazamo wa Lisu.
Wewe ni timu gaidi unajulikana
 
Hapa ndipo unaona mapungufu ya huu muhimili kwamba haujitegemei. Ndo maana Spika anaonekana kama mteule wa Rais. Anatetemeka na kuomba radhi.
Watz wanadai katiba mpya Ndugai kwa unafiki wake anajifanya haelewi acha yamkute.
Jenerali Ulimwengu alishasema. Watu wanaingiwa na hofu ambayo haikupaswa kuwepo. Jobo kathibitisha.
 
..kama kawaida yetu Watz tunasoma kichwa cha habari na kuanza kutoa majibu.
 
Anamtletea mtu aliyemnyima mshahara na haki zake zote za ubunge. Ndugai hata akiwa na haki siwezi kumtetea mshenzi sana.

Infact akitokea nyoka na nsugai wanahitaji msaada otherwise atakufa basi nipo radhi kusaidia nyoka hiyo mbwa Ife.
Lissu anajua siasa hawezi kusema asichoamini eti kisa Ndugai alimnyima mshahara.
 
Kwenye video hii Tundu Lisu amemtetea spika Ndugai kutokana na kukataa kwa mara ya kwanza bunge kuwa rubber stamp wa serikali, kwani mikopo yote hupita bungeni lakini huu wa trillion1.3 haukupelekwa bungeni mbali ulipitishwa juu kwa juu.!

Lisu amesema Ndugai amekaa bungeni kwa miaka 22 huku akishika nafasi mbalimbali za uongozi hivyo haiwezekani akawa hajui utaratibu wa wapi pa kuongelea mbali amefanya hivyo kwa sababu kuna jambo.

Tundu atuache tu kwenye hili, ndugai aliomba radhi kwa mama tayari hivyo ni wazi alikanyaga nyaya za umeme

Tundu ana jambo anatafuta kwa ndugai kwa vile ametangaza kurud karibuni.,

Issue sio mkopo umepita bungeni au la issue ni mikopo ina tija kwa maendeleo ya nchi au la, tundulisu ajielekeze huko., toka zamani Tz viongoz wanakawaida kupitisha mambo ikulu haikuanza kwa mama tu

Lakini jengine ni kwanini ndugai alitaja 2025?? Hapa ndio kuna kiza kinene., mama yuko sawa kabisa
 
Ndugai ni mgombea urais kupitia chadema 2025
 
Back
Top Bottom