Ndugai hakupaswa kuomba msamaha hapa ndipo kosa lake lilipokuwa limejificha...huko kwengine kote alikuwa sahihi. Kuhoji ni kazi mojawapo ya bunge na serikali ilipaswa kutolea ufafanuzi zaidi ili muhimili wa uelewe zaidi, sasa Rais alitaka aulizwe nani kuhusu hizo mikopo?...Taasisi ya Urais ni kubwa na nyeti sana wala haipaswi kujibu hoja kwa jazba wala kejeli. Ile hoja bunge likianza inatakiwa speaker ailete kwa mtiririko mzuri ili wabunge waielewe zaidi na serikali ifafanue kwa kina watu waelewe. Naungana na wote wanaounga kuhoji mikopo ya nchi kama alivyo fanya speaker ila siungi mkono kuomba msamaha hapa!!