Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Hayo majeshi yatahitaji miondombinu na huduma nyingine katika majimbo yafanye kazi zake kwa ufanisi,serikali kuu lazima ihakikishe uwepo wa mambo hayo katika majimbo husika.
Pesa za jeshi haziendi majimboni zinatoka serikali kuu kwenda jeshini moja kwa moja Jeshi ni jukumu la serikali kuu sio Jimbo gharama zinaebwa na serikali kuu ya baada ya kupokea michango ya majimbo ya gharama za uendeshaji serikali kuu
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo...
SERIKALI YA MAJIMBO
Wakati naandaa somo kuhusu umuhimu wa serikali za majimbo kiuchumi; tuanze kutafakari jambo hili;
Nchi ya Rwanda ina ardhi yenye ukubwa karibu sawa na mkoa wa Tanga. Rwanda ina kilometa za mraba 26,338 wakati Tanga ina 26,677 (Tanga ni kubwa kidogo)

Rwanda ina idadi ya watu karibu milioni 13 wakati Tanga ina idadi ya watu milioni 2.

Tanga ina fursa zaidi za kiuchumi; kuna fursa ya kuingiza fedha za kigeni kama misitu mikubwa, na hifadhi za wanyama (Saadan, Mkomanzi) sambamba na vivutio vingi vya utalii kuliko Rwanda. Kuna bahari, kuna madini, kuna ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo.

Lakini kwenye maeneo ya Uchumi, Elimu, Miundombinu, Michezo, Kilimo, Biashara... Utaona Tanga ni kama kitenisi kwenye uwanja wa Rwanda.

Nini sababu kubwa ya tofauti hizi?

Je! Vipi kama Rwanda ingekuwa ni mkoa mmojawapo wa Tanzania, na mfumo wa utawala ukawa kama ilivyo sasa kwa mikoa mingine ya Tanzania? Rwanda ingekuwa kama ilivyo Sasa?

Kumbuka Tanga ambayo ni kubwa kuliko Rwanda bado kuna mikoa 13 ya Tanzania ambayo ni mikubwa zaidi.

Tutafakari kwanza maswali haya.
R = Rwanda
T = Tanga
Dr. Christopher Cyrilo
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo...
Kwani sasa hivi Magufuli anapata wapi hela ya kujenga Airport kijijini? Wakati tunajua makusanyo ya kodi kwa mwaka wilaya ya Chato hayatoshi kujenga hata km 10 za lami standard?

Anakwapua Mtwara kwenye gas na korosho, Dar kwenye bandari, Kagera kwenye kahawa na kwenda kupendezesha kwao Chato. Tunataka kukataa huu unyonyaji wa kikoloni. Kila mtu apambane na hali yake. Hakuna jimbo wala mkoa masikini Tanzania
 
SERIKALI YA MAJIMBO
Wakati naandaa somo kuhusu umuhimu wa serikali za majimbo kiuchumi; tuanze kutafakari jambo hili;
Nchi ya Rwanda ina ardhi yenye ukubwa karibu sawa na mkoa wa Tanga. Rwanda ina kilometa za mraba 26,338 wakati Tanga ina 26,677 (Tanga ni kubwa kidogo)...
unafananisha Tanga na Rwanda au na kigali? kwa Rwanda palipoendelea ni kigali tu na ni mji mkuu wa nchi utaufananishaje na Tanga mji wa kawaida tu?

halafu maendeleo na mzuguko wa pesa huendana na population Rwanda ina watu milioni 13 tanga milioni 2 ,kiuchumi unasema rwanda ina wateja wa bidhaa mbalimbali mfano chakula milioni 13 utalinganisha na tanga yenye wateja milioni 2?
 
Kwani sasa hivi Magufuli anapata wapi hela ya kujenga Airport kijijini? Wakati tunajua makusanyo ya kodi kwa mwaka wilaya ya Chato hayatoshi kujenga hata km 10 za lami standard?

Anakwapua Mtwara kwenye gas na korosho, Dar kwenye bandari, Kagera kwenye kahawa na kwenda kupendezesha kwao Chato. Tunataka kukataa huu unyonyaji wa kikoloni. Kila mtu apambane na hali yake. Hakuna jimbo wala mkoa masikini Tanzania
sio kweli
Kwenye mapato ya dhahabu ya migodi iliyoko kwenye mkoa wake wa Geita inayoingiza mabilioni ya pesa za kigeni
 
sio kweli
Kwenye mapato ya dhahabu ya migodi iliyoko kwenye mkoa wake wa Geita inayoingiza mabilioni ya pesa za kigeni
Unajua Wilaya ya Chato inakusanya TZS za kodi kiasi gani kwa mwaka? Usijitoe ufahamu
 
Unajua Wilaya ya Chato inakusanya TZS za kodi kiasi gani kwa mwaka? Usijitoe ufahamu
Tunaongelea mkoa wa Geita ambapo chato ipo ni mkoa unaoongoza kuingiza pesa za kigeni kwa mauzo ya dhahabu hizo korosho na gesi hazioni ndani .Waweza jenga viwanja vya ndege hata 20 zaidi ya chato mkoani kwao wakitaka pesa ipo
 
Kwani gharama za kuendesha mikoa yote hii na sekretarieti zinatika wapi? We jamaa bwana uwezo wako wa kufikiria ni mdogo usikute eti na wewe ndio think tank wa ccm.

Alafu ni vyema mkaelewa ,lengo la mfumo wa majimbo ni kuleta ufasini wa kiutawala na kiutendaji,kuwapa wananchi nguvu ya kuamua maendeleo yao na si kupunguza gharama za kiutawala hata Kama zitapungua kidogo kulinganisha na sasa maana hata bunge la nchi litakuwa na wabunge wachache sawa tu na serikali.

Pili badala ya kuwa na Baraza la madiwani kila halmashauri kutakuwa na bunge la majimbo kwa hiyo itapunguza urasimu na gharama kuasi lakini hili la gharama za utawala sio lengo kuu
 
Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.

Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu...
Usiwe kiazi kwani majimbo yapo marekani tuu? Mbona takribani kila nchi Afrika inatumia mfumo huu? Huu ujinga ambao umekuwepo wa kutukuza mtu eti rais ametuletea bilion hizi Mara zile ili kujinufaisha binafsi na kujipendelea hatuukubali tena.Unahalalisha wizi,matumizi mabaya ya madaraka na mtu mmja kuwa alpha na omega yaani atakachoota usiku ndio wote tufuate.

Kwani umeambiwa kukiwa na majimbo tunu za utaifa zitaondika? Unaelewa maana ya kutunga sheria zusizo contradict na sheria mama za Jamhuri? Maccm mnaweweseka kwa vile mnajua ulaji wenu vikiwemo viwanja mlivyojimilikishwa vitachukuliwa na umma.
 
Tunaongelea mkoa wa Geita ambapo chato ipo ni mkoa unaoongoza kuingiza pesa za kigeni kwa mauzo ya dhahabu hizo korosho na gesi hazioni ndani .Waweza jenga viwanja vya ndege hata 20 zaidi ya chato mkoani kwao wakitaka pesa ipo
Hv ni kwamba haujui au unajitoa ufahamu? Geita haipo hata katika top 10 ya mikoa yemye makusanyo makubwa ya kodi nchini. Geita ingekuwa hivyo unavyosema isingekuwa moja ya mikoa 4 masikini zaidi Tanzania
 
Usiwe kiazi kwani majimbo yapo marekani tuu? Mbona takribani kila nchi Afrika inatumia mfumo huu? Huu ujinga ambao umekuwepo wa kutukuza mtu eti rais ametuletea bilion hizi Mara zile ili kujinufaisha binafsi na kujipendelea hatuukubali tena.Unahalalisha wizi,matumizi mabaya ya madaraka na mtu mmja kuwa alpha na omega yaani atakachoota usiku ndio wote tufuate...

Mkuu tafuteni nchi nyingine wenye kuutumia huu mfumo muende mkaishi huko kama mnaupenda sana.
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo...
Lissu ni chokoraa mkuu hapa nchini
 
Sera ya majimbo ni kuligawa taifa.
mkoa wa Geita umepata kiwanja cha ndege Chato basi ni kelele kutwa nzima.
 
Suluhisho la hasira zako haliwezi kuwa sera ya majimbo ya kukopi na kupesti kutoka nchi nyingine.

Nchi huwa haifanyiwi majaribio kwa sera zisizokuwa na msingi wa asili, watu wataumia.
Kwani mfumo tulionao tumeiga wapi chief? Serikali kuu imehodhi mamlaka yote,mapato yote lazima yaende serikali kuu,walioko juu hawajui vipaumbele vya busokelo huko. Devolution ndiyo the way forward tukiachana na milengo yetu ya kisiasa.
 
Amesema sio lazima yawe majimbo,inaweza kubaki hata mikoa au iite chochote unachotaka jambo la msingi ni kwamba viongozi wake lazima wachaguliwe na wananchi na wananchi waweze kuwawajijibisha.
Wabunge na madiwani wanachaguliwa na wananchi kumbuka kuhusu hilo jambo.

Cha muhimu ni hao wanaochaguliwa kuwa karibu na hao wanaowapigia kura.
 
Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.

Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu...
Sera yenu msingi wake ni udikteta na kubinya uhuru wa kuchagua viongozi wananchi wanaowataka. Mnataka ma RC na maDC makada wa chama chenu ndiyo waongoze majimbo mikoa na wilaya. Wakati hawajachaguliwa hata kwa kura moja na wananchi na walio wengi ni walioshindwa ubunge.

Msingi wa utawala wa majimbo ni wananchi kuongozwa na viongozi waliowachagua wenyewe, siyo sasa tunadanganyika tunachagua viongozi kumbe ni wawakilishi tu wasio na mamlaka ya kuagiza hata choo cha tundu moja kijengwe, mamlaka yote yapo kwa mawaziri, madc, marc na maDED ambao HAKUNA HATA MMOJA ANAYECHAGULIWA NA WANANCHI. NO POLITICAL LEADER SHOULD COME INTO POWER WITHOUT BEING ELECTED BY VOTES OF THE POWER THROUGH A BALLOT BOX
 
Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha ujuha wako.

Je, unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?...

Na ww uwezo wako wa kufikiria umeishia hapo siyoo? Chukua Mfano kenya wanaotumia mfumo wa Kaunti zinazoongozwa na Ma senator, unasikia kila siku vurugu za kikanda na kikabila na Baadhi ya Kaunti kama Nairobi na Mombasa kuwa na Uwezo Mkubwa kulinganisha na nyingine.

Hii inaleta mgawanyiko ndani ya taifa na Mwisho kukosa Muungano wa kitaifa kama Kenya wanavolia kila siku.
 
Back
Top Bottom