Huu ni uzi wangu bora kwa siku ya leo
Naunga mkono hoja
Taifa limejaa watu wajinga na wapumbavu halafu washamba
Sina maana kua watu wasifurahie maisha au wawe serious muda wote hapana ila kuna vitu ukiangalia unaona kabisa ni upuuzi
Na ukiseme kinyume watu wanakuja kukuita shoga
Dudu baya anachopinga ni sahihi lakini lakini ukingalia ni kama anatumika
Kuleta attention mtandaoni
Airtime aliyopewa japo sio kwa ubaya
Ingetumika kwenye mambo ya msingi pia tungefika mbali sana
Nimegundua watanzania ni wafata mkumbo
Mtu kama TL angepewa Airtime kama hivi tungekua tumepiga hatua sana
Hili taifa hili 🙌🙌
Mkuu, hapo ndipo ninapotofautiana nawe kidogo. Huwezi kuhitimisha kwamba Watanzania ni “wajinga, wapumbavu na wafata mkumbo” kwa sababu tu leo wameipa attention Dudu Baya.
Kama tunataka kwenda mbele lazima tuangalie kwenye mzizi wa tatizo, tuangalie kwanza mfumo wa siasa wenyewe. Ajenda nyingi tunazoziona zikihama kutoka jambo moja kwenda jingine zinatengenezwa na wanasiasa wenyewe, ikiwemo Hawa wa chama cha CHADEMA
Mfano, utakuta leo Lissu na Heche wako frontline ya mapambano, kesho tunasikia mjadala ndani ya CHADEMA ambapo wanachama makada na viongozi baadhi ya chadema wakishutumu uongozi wao kuhusu maslahi au tuhuma mbalimbali Mfano pesa za tone tone , ambazo nataka nikukumbushe pia zilichangwa na sisi Watanganyika wajinga..Mara utasikia Lema ameibuka na kutoa kauli ya kudai "njia Bora ni maridhiano bila kujali maumivu tuliyoyapata ", mara kauli . Ujakaa vizuri hao hao viongozi wa chadema ghafla wanaamisha ajenda inahamia kwenye swali la “Nchimbi yuko wapi?” Suala la kutokuonekana kwa Makamu wa Rais linageuzwa kuwa ajenda kubwa ya taifa na chadema wenyewe muda huo ccm wako kimya na wakati mwenyekiti wa chama chao ndugu LISSU yuko rumande akisubiri mchakato wake dhalimu wa kisheria.
Hata Lissu mwenyewe ameingia kwenye mjadala huo wa Nchimbi na kutoa kauli kuhusu hilo. Hivyo huwezi kuwalaumu wananchi kwa kubebwa na trend na wakati ndio umekua mfumo wa maisha wa taifa na hata wale wanao onekana kama wapigania Haki ndio wanaohamisha ajenda na attention za masuala mihumu. Huo ndio mfumo wa “siasa za matukio” na ndio mfumo wa maisha ya Watanganyika.
Kwa sababu kama leo watu wanajadili Dudu Baya, kesho Nchimbi, kesho nyingine maridhiano, halafu baada ya siku chache ajenda nyingine inachukua nafasi, tatizo si kwamba wananchi wote ghafla wamepoteza uwezo wa kufikiri. Tatizo ni kwamba tumekuwa taifa linaloendeshwa na matukio, na hata wanasiasa wetu pendwa wenyewe wanashiriki katika kulijenga hilo.
Na kusema Lissu angepewa airtime kama Dudu Baya basi Tanzania ingepiga hatua pia ni assumption. Airtime peke yake haileti mabadiliko. Kinachohitajika ni ajenda yenye mwendelezo, mikakati, taasisi, utekelezaji na matokeo.
Zaidi ya hapo, tusisahau kwamba hawa hawa Watanzania unaowaita wajinga na wafata mkumbo ndio hao hao waliowahi kujitokeza kwenye matukio ya kisiasa yenye hatari kubwa kama lile la October 29, 2025 na kuweka usalama na maisha yao rehani. Wakati huo wengi wetu tulikua mafichoni .Hivyo si sahihi kupima akili au ujasiri wa jamii nzima kwa kile kinachotrend kwenye mitandao siku moja ni kuwakosea Wengi wenye ujasiri wa kulipambania taifa lakini wakikwamishwa na mfumo wa kisiasa nchini.
Dudu Baya kuwa trending leo ni tukio la muda mfupi. Kesho linaweza kusahaulika na trend nyingine ikachukua nafasi. Hiyo peke yake haiwezi kuwa kipimo cha akili za taifa.
Kwa hiyo mkuu, mimi sioni tatizo likiwa kwa Mtanzania anayefuatilia Dudu Baya. Naona Dudu Baya ni Muenselezo wa mfumo mpana zaidi ambao tayari tumeujenga kama jamii.
Tusihukumu watu kwa trend ya siku moja; tuangalie mfumo unaotengeneza hizo trend. Na hata wanaharakati na wanasiasa wa upinzani wanapaswa kujielimisha zaidi katika hili.