Kalamu unaamini uchaguzi unaweza usiwepo kwa sababu kuna watu hawataki uwepo kwa sababu hakuna katiba mpya?
Swali lako sijalielewa mkuu 'macho'.
Ngoja nijieleze kidogo ili unielewe ninaposimamia:
Uwepo wa Katiba Mpya katika muda uliopo kabla ya uchaguzi, sasa hivi haiwezekani. Hili limesababibshwa na CCM hao hao, wanaodai sasa kwamba inahitajika zaidi ya miaka mitatu kufundisha watu!
Kwa hiyo Katiba Mpya Haiwezekani.
Marekebisho ya sheria je zinazohusiana na uchaguzi huru?
1. Tume Huru ya uchaguzi
2. Matokeo kuhojiwa Mahakamani na mambo mengineyo.
haya nayo CCM sasa hivi wanapiga danadana ile ile kama ya Katiba Mpya.
Kiufupi ni kwamba CCM sasa hivi wanayofanya ni kutengeneza mazingira ya kuwabakisha madarakani.
Kwa hiyo, kinachotakiwa sasa hivi ni kwa wananchi kuandaliwa vyema kuzijua mbinu wanazofanya CCM. Hata uchaguzi ukifanyika katika mazingira mabovu, ijulikane wazi kwa wananchi, na wawe tayari kukabiliana na hujuma hizo.
Hii ndiyo kazi inayotakiwa kuwa inafanyika huko ndani ya CHADEMA.
Kuzuia uchaguzi inawezekana sana iwapo maandalizi mahsusi yatafanyika, na tutachangia mbinu za kuyawezesha hayo ndani ya sheria zetu.
CCM ni wahalifu. Wavunja sheria. Ni lazima pawepo na njia za kuwazuia kufanya uhalifu huo.
Dola haipo kwa minajiri ya kutumika kuvunja sheria.