Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Ukali wa maneno ya Lissu ni dalili kuwa hawezi kuwa kiongozi wa watu. Hata angeshinda uRais 2020 sidhani kama angekuwa na muda wa kutawala.

..Samia ana kauli tamu kwelikweli, lakini ufisadi wake kama huu wa bandari ni mchungu kama shubiri.

..sidhani kama ukali wa kauli za mhusika ni kipimo sahihi cha uongozi au uadilifu wake.

..kinachomdhibiti kiongozi; matendo, na tabia zake, ni katiba na sheria nchi.
 
..mkataba wa Tz na Dp sio wa kifedhuli?

..kama sio wa kifedhuli kwanini serikali imelazimika kupeleka mswada wa kubadilisha sheria zetu ili kuwezesha mkataba na Dp kutekelezeka?

..Je, walioandaa na waliopitisha mkataba wa kifedhuli wanastahili kuitwa jina gani na wananchi?

..Je, hawastahili lawama na kukosolewa kwa mkataba walioingia?

..Je, walioingia mkataba mbovu wana haki ya kuwapangia wananchi kauli na namna ya kuukosoa mkataba mbovu na wakifedhuli walioingia?
Watu wengi including wewe mnakosoa na mnaeleweka pia. Ila Lissu amepindishwa ubongo na marisasi
 
Kama una accept kuwa Magufuli alikuwa mshenzi wahedi sasa tunaelewana. Ukiwa binadamu mwenye akili sawasawa utamtendea tofauti MSHENZI WAHEDI dhidi ya muungwana. Na hapo ndipo nina shida na Lissu
Muungwana nani sasa?

Samia? Huyo aliyesema askari wa CCM hawakosei kupiga risasi, wangemuua Lissu?

Huyo aliyesema watu wakimpigia kura au wasipompigia kura yeye hajali, kwa sababu ana uhakika wa kushinda?

Huyo anayesaini mikataba kama mtu asiyejua kusoma?
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Huihui umekuaje kwan? Naona kama haupo saw mkuu!!
 
Hawa kina Huihui ni baadhi ya Watanzania ambao wanaweza kutiwa vidole matakoni, halafu wakacheka kwa furaha na kusema "Nafurahi kwa sababu nimetiwa vidole matakoni tu, sijabakwa".

Na wanategemea wengine wafurahi hivyo hivyo.

Yani hapo ndipo upeo wao wa kufikiri ulipo.
 
Watu wengi including wewe mnakosoa na mnaeleweka pia. Ila Lissu amepindishwa ubongo na marisasi

..nadhani tu-focus kwa Ssh.

..yeye ndiye aliyeko madarakani.

..Ssh ndiye anayewajibika kurekebisha mkataba wa Dp na kuleta mkataba wenye maslahi na nchi.

..malalamiko kwamba Ssh ametukanwa, ni janja-janja ya kukwepa kutimiza wajibu wake.
 
..pia mkataba ni mbaya mno kiasi kwamba inahitaji utumie nguvu kubwa sana kuukosoa na kuwakosoa waliohusika bila kutumia maneno makali au lugha ngumu.

..kinachopelekea Ssh kusemwa vibaya, " kutukanwa, " au "kudhalilishwa,"ni ubaya na ubovu wa mkataba ulioko mezani, na sio ukorofi wa wanaomkosoa.

..binafsi namshauri Ssh aurekebishe mkataba wa Dp tuone kama hatasifiwa kwa nguvu zilezile au zaidi ya zilizotumika kumkosoa.

Cc Nguruvi3
 
Mkuu,

SSH ataurekebisha vipi mkataba uliopitishwa na bunge?

Ataurudisha mkataba bungeni, na kuliambia bunge lifute ratification ya awali, liufanyie mkataba uliorekebishwa ratification mpya?

Bunge litakubali?

Haya, tuseme atafanya hivyo, na bunge la rubber stamp ya CCM litakubali, huoni kwamba jambo hilo lita trigger arbitration clause na DPW? DPW atasema mkataba umepitishwa na bunge tayari, kwa nini mnaurudisha bungeni? Rightly so.

Samia alikuwa na wakati wa kurekebisha mkataba, kabla haujapitishwa na bunge, sasa hivi umeshapitishwa na bunge hawezi kuurekebisha bila ku trigger some arbitration clause with DPW.
 
Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Unataka kutuambia aliyafanya hayo ili ije kuwa kinga ya kutokosolwa!
 
Kwanza hakuna nchi iliyouzwa bali kuna mkataba wenye vipengere vya HOVYO. Kwa binadamu mwenye akili sawa ambaye ametendewa MEMA na Samia kama alivyotendewa Lissu angechagua lugha ya kutumia.
Mimi kuandika "maandishi yako ni matope" ni sawa na kuandika/kusema wewe ni matope"!!!???
 
..nadhani tu-focus kwa Ssh.

..yeye ndiye aliyeko madarakani.

..Ssh ndiye anayewajibika kurekebisha mkataba wa Dp na kuleta mkataba wenye maslahi na nchi.

..malalamiko kwamba Ssh ametukanwa, ni janja-janja ya kukwepa kutimiza wajibu wake.
Threads za kumkosoa Samia zipo hata mimi nimeweka pale kwenye post #1 nyuzi 2.

Hii thread ili focus kwenye kauli za lugha ya high tension ya Lissu. Usimu exonerate Lissu kwenye huu ufedhuli
 
Mkuu mbona wewe unaandika vizuri na tunaelewa!! Lakini huyu jamaa anamwita Rais ni akili au matope?? Sidhani hata kama familia yake inakubaliana kwenye hili
Amesema "kauli" zake na si yeye.
 
..pia mkataba ni mbaya mno kiasi kwamba inahitaji utumie nguvu kubwa sana kuukosoa na kuwakosoa waliohusika bila kutumia maneno makali au lugha ngumu.

..kinachopelekea Ssh kusemwa vibaya, " kutukanwa, " au "kudhalilishwa,"ni ubaya na ubovu wa mkataba ulioko mezani, na sio ukorofi wa wanaomkosoa.

..binafsi namshauri Ssh aurekebishe mkataba wa Dp tuone kama hatasifiwa kwa nguvu zilezile au zaidi ya zilizotumika kumkosoa.

Cc Nguruvi3
Wote tuko kwenye hoja hii na ndiyo tunaishi nayo.
 
Threads za kumkosoa Samia zipo hata mimi nimeweka pale kwenye post #1 nyuzi 2.

Hii thread ili focus kwenye kauli za lugha ya high tension ya Lissu. Usimu exonerate Lissu kwenye huu ufedhuli
Frankly, tatizo letu si kwamba kuna watu wana kauli kali dhidi ya rais.

Tatizo ketu ni kwamba hatuna watu hao wa kutosha.

Tunahitaji watu wengi zaidi watoe kauli kali zaidi dhidi ya rais.

Tunahitaji ku normalize hili.

Hizi staha staha za kijinga ni tatizo, ndiyo zinafanya watu waende ki kondoo kondoo na viongozi wajione wanaweza kufanya lolote.
 
Huihui umekuaje kwan? Naona kama haupo saw mkuu!!
Nimekerwa na kauli za Tundu Lissu ambazo hazina staha wala shukrani. Binadamu wa kawaida mwenye akili sawa sawa hawezi kuongea kauli zile kwa Rais Samia kwa mema aliyomtendea
 
Hizo staha zenu mara nyingi ni ujinga tu.

Rais yupo pale kufanya kazi yake, akikosea watu watamchana tu.

Staha atapata akijistahi mwenyewe.
 
Mimi kuandika "maandishi yako ni matope" ni sawa na kuandika/kusema wewe ni matope"!!!???
Kama akili yako inaona hizo ni kauli za kawaida, basi na wewe afya ya akili yako ina utata kama Lissu
 
Unataka kutuambia aliyafanya hayo ili ije kuwa kinga ya kutokosolwa!
Samia alifanya yale kama binadamu. Ila waswahili walisema "Tenda wema uwende zako, usingoje shukrani"

Na huyu aliyetendewa wema ni PUNDA tu
 
Back
Top Bottom