Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Lissu: Kauli ikiwa haina maana hata kama aliyesema ni Rais haitabadilika kuwa na mantiki

Nina declare interests. Hata mimi nina thread 2 zinazokosoa makubaliano ya DP WORLD na Tanzania kama:-

(1) Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD na thread nyingine ni kama ifuatavyo:

(2) Jebra, Mtobesya na Wanasheria wengine, fungueni kesi dhidi ya Mkataba wa DP World

Sikiliza hii clip ya dakika 5 halafu tathmini kama afya ya akili ya Tundu Lissu iko sawa. Kumbuka Rais Samia akiwa Makamu ndiyo kiongozi pekee wa nafasi ya juu aliyemtembelea kumuona Tundu Lissu akiwa Nairobi hospital.

Kisha akamtembelea Brussels baada ya kuwa Rais. Na akamlipa stahiki ambazo chini ya Magufuli asingeweza kupata. Akamfutia na kesi zake 2 mahakama ya Kisutu

View attachment 2692011
Sasa kumtembelea mtu hospitali na kumlipa stahiki zake kisheria inakuwa ndio kinga ya kumtetea katika kufanya mambo ya hovyo au vipi? 🤣

Unafiqi ni mbegu mbaya sana iliopandwa na chama cha mambuzi to an extent inataka kufanywa kuwa norm ya watanzania. Yani usipokuwa mnafiki you become a threat to other guys.
 
Hivi Lisu kulipwa stahiki zake, na kufutiwa kesi yake, vilikuwa ni rushwa ya kumfanya Lisu asiseme hata akiona mambo ya hovyo yanatendeka?
Shangaa wewe yani ilikuwa tiketi ya kununua uhuru wake wa hoja maybe🤣
 
Sasa kumtembelea mtu hospitali na kumlipa stahiki zake kisheria inakuwa ndio kinga ya kumtetea katika kufanya mambo ya hovyo au vipi? 🤣

Unafiqi ni mbegu mbaya sana iliopandwa na chama cha mambuzi to an extent inataka kufanywa kuwa norm ya watanzania. Yani usipokuwa mnafiki you become a threat to other guys.
Sijakataa kumkosoa bali naongelea kauli zisizo na staha tu. Rudi usome post yangu, mbona na mimi mwenyewe nimemkosoa Samia!!
 
Sijakataa kumkosoa bali naongelea kauli zisizo na staha tu. Rudi usome post yangu, mbona na mimi mwenyewe nimemkosoa Samia!!
Wakati anakosolewa Magu kauli zilikuwa za staha. Ila kwa mama sio za staha. 😀😀😀
 
Sasa imegundulika kuwa video clip hiyo, mleta mada ameitengeneza ili kumchafua Lisu. Muda si mrefu usishangae nduguyo kuwa banned.
Mbona ueleweki Mkuu wewe muda si mrefu ulikuwa unaisifia hiyo video sasa umebadilika unaona inamchafua Lissu?

Kwa mantiki hii nimegundua wewe kila analolisema Lissu ata kama la hovyo unalikubali kwa kifupi wewe ni mpinzani wa jambo lolote linalofanywa na Serikali

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
🤣 Naona zile zilikuwa kauli za staha maana walimsifu sana kuwa ni mwanasheria nguli. 🤣
Ulikuwa bado hujawa mkubwa! Aliyesema dictator uchwara alikuwa alikuwa nani kipindi mtu hata akilala na mkewe anamsifu Magufuli! Alipoeleza ripot ya Prof. Ossoro kwamba ni professorial rubbish iliyobebwa na utawala wa Magufuli bado ulikuwa unajifunza kuelewa mambo.
 
Kwa binadamu mwenye akili sawa ambaye ametendewa MEMA na Samia kama alivyotendewa Lissu angechagua lugha ya kutumia
Angechagua lugha kama yaliofanywa ni mambo ya kufurahisha. Huwezi kukasirishwa na jambo halafu ukatumia kauli za kusifu. Huko kutakuwa kukosa akili. Mtu timamu lazma akupe mbovu ukizingua.
 
Lugha kali ni kawaida ya Lisu, na hizo ndio lugha zinazoeleweka vizuri kwa viongozi wezi. Subiri siku Samia apigwe risasi kama Lisu ataacha kwenda kumtembelea, ama Lisu akiwa rais kama atamnyima Samia stahiki zake, hapo ndio utasema Lisu hana shukurani, sio kukalia kimya uuzwaji wa raslimali za umma.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Watu wanataka zitumike kauli za icing sugar kwenye mambo ambayo yamekaa hobela hobela.
 
Mkuu mbona wewe unaandika vizuri na tunaelewa!! Lakini huyu jamaa anamwita Rais ni akili au matope?? Sidhani hata kama familia yake inakubaliana kwenye hili
Raisi si ni binadamu na mtanzania mwenzetu. Hata yeye alichukia akaita watu stupid kabisa. Huwezi ku complain sababu ana hisia za furaha na hasira ni kama binadamu wengine tu. Sasa na watu wengine wakikasirishwa na mambo yake hawatakiwi kuitwa wahaini au kuchaguliwa cha kusema.
 
Back
Top Bottom