Lissu: Watoto wangu wana uraia wa Marekani, mbona Makonda kama ana Wivu

Lissu: Watoto wangu wana uraia wa Marekani, mbona Makonda kama ana Wivu

Akifanya mahojiano na Mwanahalisi, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Tundu Lissu amejibu maswali kuhusu uraia wa watoto wake na pia kufunga ndoa na Mzungu.

Akijibu maswali hayo, Tundu Lissu amesema watoto wake ni Raia wa Marekani kwa kuzaliwa, na pia kuhusu kuoa yeye alimsikia Makonda "Makonda anawivu".

ANGALIA VIDEO HAPA
View attachment 2898774

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
Kama Lisu ni mzalendo Kwa nini asiwaombee Watoto wake uraia wa Tanzania?

Hawa vibaraka wa Mabeberu kamwe wasiruhusiwe kuja kushika Uongozi wa Nchi hii Ili wasombe Mali zetu wawapelekee raia wa Marekani,haitokaa itokee.

Hakuna Wivu hapo
 
Nimesema, CHADEMA wataenda kutuuza mapema.

Hukukataa hayo, ikiwa ina maana hayo yanawezekana ila hamtaki Wapiga kura wayafikirie au?

Kwani sio Lema aliyesema Canada mswano?

Tukija kwenye suala la Uraia, unaona kabisa nimeuliza maswali, hukuyajibu, badala yake umeshupaza shingo na mihemeko.

Unapata wapi haki ya kuhoji hoja zangu za msing?(ni zipi hizo?)kwani tunazungumzia faida za Uraia pacha hapa? Au majivuno ya Tundu Lissu?

Nye nye nye
Hao ccm wanaokabidhi mbuga Kwa waarabu na bandari bado Kwa Wachina si ndio wamewauza tayari!? Au hujui Hilo.!?
 
Lisu anambwela mbwela tu hapo.

Makonda ana hoja.

Huwezi kuwa mzalendo kwa nchi yako ukaachia watoto wako kuwa Raia wa nchi nyingine.

Lisu anatulaghai tu hapa.

Afanye siasa kama ajira basi maisha yaendelee ila kwa uzalendo hapo hana hata chembe.
 
Lisu anambwela mbwela tu hapo.

Makonda ana hoja.

Huwezi kuwa mzalendo kwa nchi yako ukaachia watoto wako kuwa Raia wa nchi nyingine.

Lisu anatulaghai tu hapa.

Afanye siasa kama ajira basi maisha yaendelee ila kwa uzalendo hapo hana hata chembe.
Uzalendo wa mtu unahusiana vip na watoto wake?.Kwani uzalendo niwawatoto au wakwake?.Ujinga mwingine bana.
 
Sasa watoto ni wamarekani.... yeye anautaka uraisi wa Tanzania wa nini?
Kwenye sifa zakikatiba za kugombea urais kuna mahali panamkataza asigombee kwasababu ya uraia wa watoto wake kua wamarekani?
 
Aliyekuwa mgombea urais kupitia chadema Ndg Tundu Antipas Lissu ameeleza katika mahojiano yake aliyofanya na MwanaHalisi Online ambayo yako pia YouTube kwamba watoto wake wote ni raia wa Marekani.


Lissu anataka urais lakini familia ipo nchi za watu
 
Mbona alishaeleza hili siku nyingi?
anyway...punguza wivu jombaa.
Utafariki
 
Watoto wapo marekani ni jambo zuri Kama watoto walivyo Magomeni tuache wivu hakuna MTU asiyependa watoto wake wasome shule nzuri na kuishi sehemu safi.
 
Back
Top Bottom