Lissu: Watoto wangu wote ni raia wa Marekani

Kauli hii ameitoa Tundu Lissu wakati akichangia mada katika space huko Twitter.

Kumbe wenzetu wanataka kuleta vurugu hapa nchini, wao wameshatanguliza familia zao nje ya nchi! Wanahamasisha watoto wetu waandamane, wapigwe rungu, wa kwao wako Trump Hotels wanakula baga na pizza.

Kwa nini Lissu hawaambii watoto wake wakane uraia wa Marekani ili wafaidi matunda ya anavyopigania? Je, Lissu sio mpango wa C.I.A katika taifa letu?

Muda utasema. Kwa sasa hana kazi ya kumuingizia kipato, lakini anatalii majiji ya Ulaya na Marekani akila maisha kwa fahari kuu, hatujui chanzo cha mapato yake.

Napiga picha ikulu yetu imejaa raia wa marekani, wanazurura tu katika bustani, wanajisaidia vyooni, na kuoga, wanaleta marafiki zao, ambao pengine no majasusi wanapandikiza kamera na vinasa sauti, wanachomoa mafaili na kuondoka nayo, na kuhaki computer zetu, au ku-recruit staff wa ikulu dhidi ya nchi yetu.
Mpaka leo watu wazima tukae hapa tuongelee watoto wa watu! Kenya kuna topic kama hizi?? au ni sisi wa kushinda kuangaliana angaliana tu
 
I wish angekuwa kweli huo mpango wa CIA ili atusaidie kuiondoa ccm madarakani.

Baada ya hapo tutajua cha kufanya. Ila kwa sasa adui wetu namba moja kama Taifa, ni ccm! Na siyo Tundu Lissu, au hao CIA.
Ila badae huwaga mnajutaga na hizo kauli.... Watu mnapena sana vita utadhani sio watanzania.... Kwani jambo likifanyika bila kuathiri maisha ya watanzania wengi unapungukiwa nini?
 
Ww hata wakichomoa ma faili vote tubak bila kumbukumbu hakuna shida maaana CCM WANAIBA NA KUMBUKUMBU ZIPONA HAKUNA WA KUWAGUSA
 
Ila badae huwaga mnajutaga na hizo kauli.... Watu mnapena sana vita utadhani sio watanzania.... Kwani jambo likifanyika bila kuathiri maisha ya watanzania wengi unapungukiwa nini?
Watakaojuta ni wale wanufaika wa huu mfumo wa sasa! Sasa kwa mtu kama mimi, nitajuta kwa lipi?

Ashinde CCM, ashinde Chadema! Bado maisha yangu kwa sehemu kubwa, yatabakia kuwa yale yale tu. Ila ukweli lazima uwekwe hadharani; kwa sasa ccm siyo msaada kwenye nchi yetu.
 
Ada kwa vyuo vya marekani ni juu sana.

Na lazima mzazi alipe gharama za masomo za mwanae.

Sasa mzazi mtanzania toka nchi maskini anapata wapi mapesa ya kusomesha mtoto wake raia wa nchi tajiri duniani??

Si ndio lazima wizi na kulamba asali kufanyike ili kuziba hayo magap??
 
Kauli hii ameitoa Tundu Lissu wakati akichangia mada katika space huko Twitter.

Kumbe wenzetu wanataka kuleta vurugu hapa nchini, wao wameshatanguliza familia zao nje ya nchi! Wanahamasisha watoto wetu waandamane, wapigwe rungu, wa kwao wako Trump Hotels wanakula baga na pizza.

Kwa nini Lissu hawaambii watoto wake wakane uraia wa Marekani ili wafaidi matunda ya anavyopigania? Je, Lissu sio mpango wa C.I.A katika taifa letu?

Muda utasema. Kwa sasa hana kazi ya kumuingizia kipato, lakini anatalii majiji ya Ulaya na Marekani akila maisha kwa fahari kuu, hatujui chanzo cha mapato yake.

Napiga picha ikulu yetu imejaa raia wa marekani, wanazurura tu katika bustani, wanajisaidia vyooni, na kuoga, wanaleta marafiki zao, ambao pengine no majasusi wanapandikiza kamera na vinasa sauti, wanachomoa mafaili na kuondoka nayo, na kuhaki computer zetu, au ku-recruit staff wa ikulu dhidi ya nchi yetu.
Kwa hiyo ulitaka wawe raia wa tz waishie kunyanyapaliwa kama baba yao.
 
George Weah ni Rais wa Liberia mtoto wake juzi kafunga bao na timu ya taifa ya marekani

So na George ni C.I.A?
Muulize zile nchi zenye uraia pacha wale raia pacha wote mabeberu? Muulize hizo nchi zenye uraia pacha zimepata shida gani kwa hao raia pacha. Wamepindua nchi? Zaidi tunaona Morocco karibu 90% ya national team ni raia pacha....

Hii ni nothing zaidi ya ushamba na brainwashing, ilhali adui mkubwa wa waTZ na wapigaji wakubwa ni waTZ wenyewe wazalendo!!!
 
Ada kwa vyuo vya marekani ni juu sana.

Na lazima mzazi alipe gharama za masomo za mwanae.

Sasa mzazi mtanzania toka nchi maskini anapata wapi mapesa ya kusomesha mtoto wake raia wa nchi tajiri duniani??

Si ndio lazima wizi na kulamba asali kufanyike ili kuziba hayo magap??

..raia wa marekani wana mikopo na udhamini[ scholarship ] mbalimbali kusoma ktk vyuo vikuu.

..wanaolazimika kusoma kwa ada kubwa kubwa ni wanafunzi ambao sio raia wa marekani.
 
Ada kwa vyuo vya marekani ni juu sana.

Na lazima mzazi alipe gharama za masomo za mwanae.

Sasa mzazi mtanzania toka nchi maskini anapata wapi mapesa ya kusomesha mtoto wake raia wa nchi tajiri duniani??

Si ndio lazima wizi na kulamba asali kufanyike ili kuziba hayo magap??
huna akili.
 
Watakaojuta ni wale wanufaika wa huu mfumo wa sasa! Sasa kwa mtu kama mimi, nitajuta kwa lipi?

Ashinde CCM, ashinde Chadema! Bado maisha yangu kwa sehemu kubwa, yatabakia kuwa yale yale tu. Ila ukweli lazima uwekwe hadharani; kwa sasa ccm siyo msaada kwenye nchi yetu.
Sawa mkuu... Siwezi pinga hayo ni maoni yako...
 
Lissu waache watoto wako waishi huko huko, maana CCM walitaka kuuangamiza wewe na kizazi chako chote. Sisi watanzania tunajua magumu uliyopitia, ulivyoponyoka kwenye bonde la kifo, Zaburi ya 23 ya Mfalme Daudi wa Islael kwa Mungu wake ikakusimamia.
 
Wazazi waliuza n'gombe kusomesha n'gombe
 
Najuwa hamtaki kumfahamu mtoa mada.mtoa mada anamanisha Lissu anataka watu waandamane Tanzania Kwa ajili ya kumpigania maslahi yake na familia yake wakati yeye yupo nje analipa na wazungu wewe huna anaekulipa upo tz.umeingia barabarani umevunjwa mguu hivi Lissu anaweza toka nje akakuletea fedha mpk upone? Tafakari chukua hatua
giphy.gif
 
..ukiandamana viongozi wa CCM wanaagiza Polisi wapige mabomu, risasi, na kuvunja watu miguu.

..wanafanya hivyo wakijua kwamba watoto wao si miongoni mwa hao wanaoandamana.

..waandamanaji wangekuwa na mahusiano na CCM Polisi wasingetumika kuwasambaratisha na kuwaumiza.
 
Back
Top Bottom