List ya wasanii wa Bongo ambao walipata umaarufu na mafanikio makubwa, lakini leo wako juu ya mawe

List ya wasanii wa Bongo ambao walipata umaarufu na mafanikio makubwa, lakini leo wako juu ya mawe

1) Mr Nice - huyu Afrika mashariki nzima na baadhi ya nchi za kusini kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia hakuna mtu ambae alikuwa hamjui. Mpaka watoto wadogo huko vijijini Malawi walikuwa wanaimba kidali poo. Miaka ya 2002 mpaka 2005 alipiga hela sana lakini akaishia kushusha zipu, leo hii anazurura tu mitaani hana mbele wala nyuma.

2) Ferouz - Nyimbo kama kamanda, barua, kwaherini aliyoimba na prof Jay zilimpa umaarufu mkubwa hadi kupelekea kutunzwa gari na aliekuwa raisi wa JMT wa wakati huo hayati Benjamin W Mkapa. Na yeye alishika sana hela enzi hizo. Lakini leo inasemekana mambo yake yamekwenda ndivyo sivyo kwahiyo ni kama vile ashapoteza

3) 20 Percent - Huyu nae alikuja vizuri japo kwa muda mchache. Alikuja na vibao vyake matata na ile style yake ya kukwaruza kwaruza sauti huku mistari akiwa kaipangilia vilivyo, pia ukijulimsha na movie yake iliyovunja rekodi. Akaendekeza endekeza mjani na togwa. Leo hii inasemekana ukikutana nae mtaani lazima akupige mkuki umuunge buku akanywe chai.

Wapo wengi lakini acha niwataje hawa wengine mtaongezea wenyewe wasanii waliopata umaarufu na mwisho kupaki juu ya mawe kama gari isiokuwa na matairi.



upande wako vipi mkuu?
 
Back
Top Bottom