Namanga Islamic Centre ni kituo cha mafunzo ya siasa kali na mafunzo ya mapigano(KARATE, Judo, Taekwando n.k) kilichokuwa chini ya Dini ya Kiislam katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha.
Kituo hiki ni cha pili kufungwa baada ya kile cha Dodoma ambapo mabinti wasiopungua 150 walikuwa wamefungiwa kituoni na kupewa mafunzo mbalimbali ya kidini.
Vituo vyote viwili vimefungwa rasmi na kamati za ukinzi na usalama za Mikoa na Wilaya husika kwani vipo kinyume na utaratibu na vinatishia usalama wa nchi.
Hali kama hii ilikuwa nchini Nigeria ambapo serikali iliacha pale ilipokuwa ikipewa taarifa kuhusu mafunzo yanayotolewa na Boko haram kwa vijana wa nchi hiyo. Madhara yake ni kuanzishwa kwa kundi la kigaidi la Boko Haram lililosumbua na kuharibu usalama wa nchi ya Nigeria.
Hapa Nchini, kulitokea vuguvugu za itikadi kali na ugaidi kule Pwani pamoja na Mtwara. Sisi kama watanzania, tuna wajibu wa kutoa taarifa kuhusu vyuo au vituo hivi vinavyotoa mafunzo ya mapigano na itikadi kali.
Mimi kama Mtanzania, ninaanza kukitaja kituo cha mafunzo ya mapigano na itikadi kali kilichopo kwenye Msikiti wa Ipogolo pale Iringa Manispaa pamoja na Msikiti uliopo kwenye Kijiji cha Kitayawa njia panda ya Nyabula Wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Misikiti/Vituo hivi hufundisha vijana wa kiislam itikadi kali na mapigano na mara nyingi kama unaenda kule Nyabula toka Iringa Mjini, utakuta vikundi vya vijana hao waliovaa kanzu na viremba kichwani wakitembea kwa miguu na wakifanya mazoezi.
Naamini JF ni Platform kubwa nchi hii, kutaja kwako vituo hivi vitasaidia kulinda usalama na amani ya nchi yetu. Ewe mwana JF, funguka kwa ajili ya Mama yetu Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania, Eeehh Mungu ilinde na itetee Mama yetu Tanzania.