Lowassa aliwezaje kumvumilia Nape bila kumtamkia jambo hadi anafariki? Nape aliwezaje kutokuomba radhi hadi Lowassa amefariki?

Lowassa aliwezaje kumvumilia Nape bila kumtamkia jambo hadi anafariki? Nape aliwezaje kutokuomba radhi hadi Lowassa amefariki?

Unajichosha hiyo ndio siasa wanachoangalia ushindi ili waendelee kula peaa....
 
Nape aliweza kwenda Ikulu kumwomba radhi Magufuli kwa lengo la kupata madaraka. Lakini alishindwa kwenda kumwomba radhi Lowassa baada ya kumdhalilisha na kumtakia kifo kwenye mkutano wa adhara 2015.

Alitamka maneno ambayo katika hali ya kawaida huwezi kusema yametoka kinywani kwa mwanadamu anayemwabudu Mungu. Kumtakia Lowassa mbele ya watoto kwamba anaji.....a na akapata carrage ya kutokumwomba msamaha wala kujutia kauli ile ni jambo la kishetani sana. Ni nafsi katili sana inaweza kufanya ukatili ule aliofanya Nape just kwa ajili ya siasa.

Leo Lowasa amekwenda, si ajabu kumsikia Nape akihojiwa na kusifia Lowasa. Si ajabu kumwona anashiriki kwenye mazishi yake na si ajabu kumwona akijifanya ni rafiki wa familia ya Lowasa.

Just imagine alivyomtukana jukwaani mkewe akimwona anajisikiaje? Then , kiumbe wa aina hii anakwenda kufungia vyombo vya habari na kuhukumu watu kwa utovu wa nidhamu! Hawa wanadamu wa aina ya Nape si wema hata kwa Mhe. Rais, ni watu ambao kwao maisha ni familia yake au yeye kuteuliwa.

Clip ya Nape naamini ni moja ya clip ya kisiasa iliyoonyesha ukomavu wa Lowasa, kabla na baada ya kuacha jukwaa la siasa. Kwamba alimsamehe sijui
Nape amedanganya kwamba walikutana chobingo na Lowassa na akamsifu kuwa anafanya vizuri kuwa na misimamo ya kisiasa mbali na tofauti walizonazo. Bahati mbaya hatuwezi tena kusikia ukweli wa kauli hii kutoka upande wa pili wa Lowassa.
 
Watawafukuza wangapi?

BTW: JF inatumia vigezo gani kufunga mijadala?
Wanasiasa sifa yaoa kubwa ni UNAFIKI.

Wale wa CHADEMA na wa CCM wote walimtukana sana huyu Mzee.
 
Nape aliweza kwenda Ikulu kumwomba radhi Magufuli kwa lengo la kupata madaraka. Lakini alishindwa kwenda kumwomba radhi Lowassa baada ya kumdhalilisha na kumtakia kifo kwenye mkutano wa adhara 2015.

Alitamka maneno ambayo katika hali ya kawaida huwezi kusema yametoka kinywani kwa mwanadamu anayemwabudu Mungu. Kumtakia Lowassa mbele ya watoto kwamba anaji.....a na akapata carrage ya kutokumwomba msamaha wala kujutia kauli ile ni jambo la kishetani sana. Ni nafsi katili sana inaweza kufanya ukatili ule aliofanya Nape just kwa ajili ya siasa.

Leo Lowasa amekwenda, si ajabu kumsikia Nape akihojiwa na kusifia Lowasa. Si ajabu kumwona anashiriki kwenye mazishi yake na si ajabu kumwona akijifanya ni rafiki wa familia ya Lowasa.

Just imagine alivyomtukana jukwaani mkewe akimwona anajisikiaje? Then , kiumbe wa aina hii anakwenda kufungia vyombo vya habari na kuhukumu watu kwa utovu wa nidhamu! Hawa wanadamu wa aina ya Nape si wema hata kwa Mhe. Rais, ni watu ambao kwao maisha ni familia yake au yeye kuteuliwa.

Clip ya Nape naamini ni moja ya clip ya kisiasa iliyoonyesha ukomavu wa Lowasa, kabla na baada ya kuacha jukwaa la siasa. Kwamba alimsamehe sijui
LOWASSA ni mtu mwenye HOFU ya MUNGU alimsamehe kama alivyomsamehe ALIYEMKATA JINA wakati wa kugombea Urais ndani ya CCM na wale waliojichimbia Masaki kuchakachua Matokeo ya Tume ya Uchaguzi
 
Binadamu wengine ni wavumilivu sana maisha yao yote
Hata humu Kuna mtu anaweza akakutukana bure kisa hakubaliani na mawazo yako
Lakini unamuombea tu awe mwema maana hii Dunia ya kupita
 
Nape amedanganya kwamba walikutana chobingo na Lowassa na akamsifu kuwa anafanya vizuri kuwa na misimamo ya kisiasa mbali na tofauti walizonazo. Bahati mbaya hatuwezi tena kusikia ukweli wa kauli hii kutoka upande wa pili wa Lowassa.
Huyo mpumbavu asingekaa kimya siku zote hizo ndio aje aseme leo
 
Yashapita hayo, Acheni ujinga wa kugeuza misiba vijiwe nongwa. Yatatusaidia nini mema na mabaya ya Lowassa. Atakaeropoka upuuzi saivi ndo tunaruka naye ila walioropoka zaman hatuna shida nao maana marehem alikua na nafasi ya kujitetea mwenyewe na hiyo ndiyo siasa. Ahya wewe mleta mada madai yako yataisaidia nini Familia ya marehem?
Tunaweka kumbukumbu sawa Ukitaka kujua unakokwenda angalia ulikotoka, tabia ni kama ngozi ya mwili.
 
Tunaweka kumbukumbu sawa Ukitaka kujua unakokwenda angalia ulikotoka, tabia ni kama ngozi ya mwili.
Nachojua Lowassa hakua mtu wa manenomaneno, Alikua mtu wa kuamua na kutekeleza kisha kukaa kimya. Hicho ndo kitu ninajifunza kwake.
Si ajabu aliamua kumpuuza Nape.
 
Nape hana kosa ukizingatia pale alikuwa jukwaani...Sasa wale wamatumbi wenzangu pale angewaambia kipi cha kuwa furahisha zaidi ya kile?
Mambo yale wale ndio wanapenda.
 
Eti nape Nate Waziri.

Watu wa ovyo ndio wanapewa dhamani kuongoza sekta adhimu kama hizi.

Nchi ya ajabu Ile.
 
Nakaaaa hapa naendelea kufuatilia
List ya wasio wanafiki kabaki
Mnyika
Dr slaa
 
Hapa bumunda limekaa kama zombie
 
Attachments

  • 20240214_140246.jpg
    20240214_140246.jpg
    113.5 KB · Views: 2
Kila ubaya utalipwa
Tayari ubaya wake ulishalipwa na Mwenyezi Mungu.

Nape ni kati ya vijana wa CCM ambao nyota yake ilikuwa inang'ara sana na alionekana kuaminika sana ndani ya chama na jamii, ninaamini njia yake ilikuwa imenyooka sana na huenda angepata moja ya nafasi za juu ndani ya chama au ndani ya serikali hata waziri mkuu kwa sasa au baadae. Lakini ghafla Nape hana nguvu na hana ushawishi ndani ya Chama. Hata kidogo anachokipata ni kwa hisani + huruma na struggling. Angalia yaliyomkuta kipindi cha Magufuli, kwa jicho la nje tutasema ni ajali za kisiasa lakini kwa jicho la rohoni YALE NI MAPIGO.

Siku zote Mungu huwainua WAFALME lakini pia HUWAADHIBU AU KUWASHUSHA WENYE VIBURI, DHULUMA nk.

Hata Makonda na Sabaya wanatakiwa kumlilia sana Mwenyezi Mungu awaodolee laana kwa waliyoyafanya na yaliyoumiza haki za watu.

Bahati mbaya sana watawala wengi waliotumikishwa na ibilisi na kuumiza watu huwa mioyo yao huwa migumu sana kuungama na huwa hawajutii kwa mabaya waliyofanya bali hujutia tu kupoteza nafasi zao.

Nchi hii inahitaji viongozi wenye UTU KAMA MAMA SAMIA, Huyu Mama pamoja na Siasa lakini ana ubinadamu sana. Pia hii nchi inahitaji viongozi kama Dr Nchimbi na bwana Kinana, sijawahi kumsikia Nchimbi au Kinana akidhalilisha watu, halafu ni viongozi ambao akili zao zimetulia sana na hawana Mihemko.
 
Je, kama Nape aliongea vile ili kuwapumbaza tu wapinzani?
Unakumbuka Kikwete alivyokuwa akimnanga SUMAYE alipohamia CHADEMA?
Nachotaka kusema,siasa ina ghiliba nyingi sana ambazo zinachosha.

Hata ukisikia wanatukanana usijiaminishe kwamba huo ni ugomvi %
 
Back
Top Bottom