Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Nashukuru kwa kugundua Lukuvi ni jembe, aendelee kusimamia vijana waliopewa ardhi kwani ni ngumu sana. Hongera baba Lukuvi kwa kusimamia vizuri ardhi.
 
Huku ni kumdharau Waziri Mkuu, maana msimamizi mkuu wa mawiziri ni waziri mkuu
 
Hapa inabidi Mama ashauriwe vizuri na mwanasheria mkuu on the way forward, kwasababu hao ni wabunge kutoka mhimili mwingine hawawezi kuwa watendaji wa serikali isipokuwa kupitia title ya mawaziri, ambayo imeainishwa kikatiba kuwa lazima wawe wabunge.sasa bila kuwa mawaziri watachezaje double role? kwa mihimili tofauti? Amewapa heshima ila kusijetokea mgogoro wa kikatiba, na pia isije ikaingiliana na role ya PM etc.
Sahihi kabisa mkuu.
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.
View attachment 2075769
Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.
Kitengo Cha Government Think Tank
 
Mheshimiwa A. Lyatonga Mrema, alipoteuliwa kuwa naibu waziri Mkuu, mbona swali hili ulilificha mfukoni?
sikumbuki kama niliuliza au la!🙄🙄
ila mimi nadhani ingekuwa vema eneo la akina mkuchika wangepewa wao na kisha akina mkuchika wakapaewa kwingine au wakapumzishwa.
 
Back
Top Bottom