Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Mzee Mwinyi alimteua Lyatonga Mrema kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hakipo kikatiba ili tu kumdhibiti na mbio zake(wanavyodai wazee).

Leo Mama kawapa kazi Lukuvi na Kabudi kazi ambazo hazipo kwenye katiba wala muundo wa Serikali.
Kama leo hii nafasi hizo hazipo kwenye muundo, kesho Raisi si anaweza kuingiza hizo nafasi kwenye muundo? Kwani akisema ni mshauri wa raisi mambo ya mikataba mtabisha? Au, akisema ni mshauri wa raisi mambo ya ardhi na miundo mbinu mtabisha? Cha muhimu wazee wetu watapatiwa kazi zenye utulivu, na wanaweza kuwa wa manufaa zaidi kuliko huko kwenye active politics
 
the sukuma gang member unajipa hope ila tayari umeshapiga u-turn hujui unapoelekea [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sukuma gang ndio hao umeambiwa na mama ana kazi nao pale ikulu!

Na moja ya kazi hiyo ni kufanya maandalizi ya kuwapelekea moto 2025.

Kalaga baho na sukuma gang yako
 
Kweli Rais ana madaraka makubwa. Kwa hiyo anacreate ajira special kwa hawa wazee wawili. Halafu Samia yupo addicted na mitandao. Anasoma sana mitandao. Lukuvi atakuwa mshauri wa Rais ama?Kabudi tumeambiwa anaongonza majadiliano ya mikataba. Stupid.Wakifa na kaburini awafuate. Maana as if bila wao nchi haiendi. Stupid
...hivyo vyeo walivyopewa hata kwenye katiba yetu havipo....

Ina maana watakuwa wabunge na wafanyakazi maalum wa Rais?
 
Kinachomponza Samia ni kusoma sana mitandaoni!

Alafu sasa ile sababu ya kuwatoa aliyoisema kumbe ilikuwa ya uongo?

Ok.. Swali kwa machadema, je hao tena si sukuma gang
Wale wanaowaza 2025 hawakutajwa?
 
Mmmh! Kuitwa kuwasimamia Mawaziri? Hiki nacho ni cheo gani hiki? Si Mawaziri huwa wanasimamiwa na Waziri Mkuu,au? Mmmh..ngoja niishie kuguna utafikiri nakunya.
Katibu mkuu kiongozi huwasimamia mawaziri...huenda wakasaidiana nae.
 
Mama kaona kuna mamilioni ya watu nyuma ya Lukuvi. Ila pia anaona wazi sababu ya kumtoa pale ni too personal kwani msela hakuwa na nia ya kugombea 2025 ila ni wivu tu. Sasa kaona nyomi ya watu wakimpongeza Lukuvi kwa kazi nzuri aliyofanya ardhi na hata kumtaka agombee uspika mama kapaniki.
Siasa ni hesabu na siri sasa yeye yake yako wazi yote-anapiga hesabu vibaya sana kiasi kwamba harufu ya kuoneana inaonekana hata na vipofu.
Sitashangaa kuona mambo mengi anayarudia mfano lile la kuunganisha umeme kisa tu hakufikiri kabla ya kunena
 
Hapa inabidi Mama ashauriwe vizuri na mwanasheria mkuu on the way forward, kwasababu hao ni wabunge kutoka mhimili mwingine hawawezi kuwa watendaji wa serikali isipokuwa kupitia title ya mawaziri, ambayo imeainishwa kikatiba kuwa lazima wawe wabunge.sasa bila kuwa mawaziri watachezaje double role? kwa mihimili tofauti? Amewapa heshima ila kusijetokea mgogoro wa kikatiba, na pia isije ikaingiliana na role ya PM etc.
Tulieni watoto wa mjini wafanye mambo.

Siasa ni sayansi mzee baba.

Watakwenda ikulu ya Dar halafu kuna vyumba pale vina meza na makabati matupu watakaa humo.

Mshahara wao ni ule ule wa wabunge maana huko wanakwenda tu "kumsaidia" mama.

Viva Mama Samia Viva
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.

View attachment 2075769

Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.
Mkuchika hali yake inaendeleaje? Amezeeka sasa. Sidhani kama ana nguvu za aina ile
 
Tulieni watoto wa mjini wafanye mambo.

Siasa ni sayansi mzee baba.

Watakwenda ikulu ya Dar halafu kuna vyumba pale vina meza na makabati matupu watakaa humo.

Mshahara wao ni ule ule wa wabunge maana huko wanakwenda tu "kumsaidia" mama.

Viva Mama Samia Viva

Kwa hiyo kama kizuizini ama [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wameshapigwa na kitu kizito kichwan

Back
Top Bottom