Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Huyu mama sijui ni usahulifu ama hawez ku handle pressure ya matukio makubwa sielew kabisa, juz tu hapa wakat anamsagia kungun Job alitueleza kwamba kuna mawzir wanafikiria 2025 hivyo anaenda kufanya reshuffle ili wakajipange vizur wakiwa nje leo hao hao aliowatuhumu wanamkwamisha anawapamba kupita kiasi
Mzee wa upako alisema kuna jini ikulu
 
Samia kweli amedhihirisha jinsi alivyo mweupe, na jinsi alivyochagua matango porini yake yamebuma hata kabla hayajaanza kazi, hivi unawezaje kumtoa Lukuvi ukaweka Ridhiwan Kitwete? baada ya aibu kubwa ndio kajitokeza masikini kusema ana kazi nao, jamani tuna Rais kweli Tz? Taifa letu limepatwa , kupatwa kwa jua.
Kupatwa kwa jua na nyota kabisa...mama hamna kitu kabisa
 
Samia kweli amedhihirisha jinsi alivyo mweupe, na jinsi alivyochagua matango porini yake yamebuma hata kabla hayajaanza kazi, hivi unawezaje kumtoa Lukuvi ukaweka Ridhiwan Kitwete? baada ya aibu kubwa ndio kajitokeza masikini kusema ana kazi nao, jamani tuna Rais kweli Tz? Taifa letu limepatwa , kupatwa kwa jua.
Ridhiwani ana tatizo gani!? Mfano akifika Lukuvi hiyo wizara ndio haitokuwa na wakuiweza tena
 
sukuma gang wanampelekea moto mama hadi 1 haikai wala 2 haikai, japo anajaribu kuwapoza kinafiki ila bado kazi anayo, mpaka 2025 tutashuhudia mengi.
 
Njia nzur ya kupoza hali, ngoja tuone upande mwngne watajibu vip
 
Rais Samia Suluhu Hassana amesema amewapa kazi mpya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 10, 2022 muda mfupi baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri, makatibu na naibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Rais Samia amesema “Nataka niseme jambo moja tu nina kaka zangu, Lukuvi na Kabudi mko wapi? Kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu wanisaidie ili waje kunisimamia ninyi, kwa hiyo kuwaacha kwangu kwenye hiyo listi watakuja kwangu tuwasimamie ninyi” amesema Rais Samia.

Rais Samia alisifia kazi nzuri aliofanya Kabudi kuhusu mazungumzo ya serikali na mashirika .

‘Ila kazi yake kwa sababu haiko kwenye muundo haitangazwi wala nini lakini atasimamia hiyo kazi ..mashirika yote kazi zote zitakazoingia ubi ana serikali,Kabudi ataongoza hiyo team’

Kuhusu Lukuvi rais alisema ;

‘Kaka angu Lukuvi yeye ana kazi na mimi. Mtaisikia baadaye lakini namvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi’.
 
Mtu yeyote mwenye akili iliyotulia ni yule mwenye subiri anapopata taarifa Kinzani. Unapokuwa na Subira itakusaidia Kupata Ukweli au kujua Kusudi la jambo husika.

Taarifa kuhusu Lukuvi na Kabudi kwenda Ikulu kumsaidia Mh Rais zimetolewa leo hii. Pamoja na aliyoyaongelea Mama, lakini huenda kipo kikubwa kinachofuata. Na sio kila kitu kitatolewa kwa Uma.

Wapo watu humu japo ni wachache ukiangalia comments zao zinawatafsiri jinsi walivyo na UELEWA MKUBWA. Lakini Majority humu ukiangalia comments zao yaani moja kwa moja utakumbuka yale madaraja ya UELEWA ktk Psychology.
 
Basi apewe mumeo hiyo nafasi
Utakuja kupelekwa guest house na mwanaume mwenzako kwa tamaa ukiendekeza njaa mjini.

Ofisi ya mwanasheria mkuu ipo chini ya wizara ya katiba na sheria na wanakitengo maalum cha kuangalia mikataba nchi inayoingia na boss wao alikuwa Kabudi.

Sasa umtoe waziri kwenye nafasi rasmi ya kukushauri kwa kitengo anachosimamia tayari umpe nafasi isiyo rasmi halafu ndio useme umemtoa aje kukusaidia.

Ni hivi hizi ni paranoia za 2025 mama afanye kazi itaongea na watanzania watakua nae sio kuwaza mbele kwa namna yoyote. Ni kama mtu ambae keshawaza tume itatamtangaza mshindi kilichobaki ni kuwadhibiti wafuasi ndani ya CCM.

Maana hakuna ata logic waziri ni mshauri wa raisi tayari, tena Kabudi alikuwa wa sheria umfute kazi halafu utetee kwa kusema umemchukua kukushauri.Kuna mshauri wa raisi zaidi ya waziri.

Wamemtoa Mwambe na Kabudi ili waingie mikataba yao ya ovyo bandari na kuficha uozo wa mkataba wenyewe.

Tetea maslahi mapana ya nchi acha kuendekeza njaa utapakatwa shauri zako.
 
Rais Samia Suluhu Hassana amesema amewapa kazi mpya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 10, 2022 muda mfupi baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri, makatibu na naibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Rais Samia amesema “Nataka niseme jambo moja tu nina kaka zangu, Lukuvi na Kabudi mko wapi? Kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu wanisaidie ili waje kunisimamia ninyi, kwa hiyo kuwaacha kwangu kwenye hiyo listi watakuja kwangu tuwasimamie ninyi” amesema Rais Samia.

Rais Samia alisifia kazi nzuri aliofanya Kabudikuhusu mazungumzo ya serikali na mashirika .

‘Ila kazi yake kwa sababu haiko kwenye muundo haitangazwi wala nini lakini atasimamia hiyo kazi ..mashirika yote kazi zote zitakazoingia ubi ana serikali,Kabudi ataongoza hiyo team’

Kuhusu Lukuvi rais alisema ;

‘Kakangu Lukuvi yeye ana kazi na mimi.Mtaisikia baadaye lakini namvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi’.
Mmh!! Hzo position hazina title??

Anyway,, kwa Lukuvi nilishangaa na kusikitika,, ila najua baada ya wadau wengi kusikitika Kama mim hadharan,, ndo maana wamepewa backup option!!
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.

View attachment 2075769

Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.

Huu ni uvunjaji wa katiba,
NB: Mwinyi alimteua lyatonga Mrema kuwa naibu Waziri mkuu, alivunja katiba.
 
Back
Top Bottom