Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Wamefanywa kuwa desk officers, huyu mama kweli anatuvurugia nchi yetu. Yaani kweli Nape, Makamba, na Ridhiwani anawaona wa maana?
Hapo kwenye ardhi sijui itakuwaje! Unamkabidhi wizara ya ardhi bepari! Atajimilikisha ardhi yote, yeye, na jamaa zake!

Muda ni msema ukweli!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Prof. Kabudi kapigwa changa la macho. Naamini Rais kawalaghai hawa wazee. Soob watajikuta hawapelekewi mafaili wala kuitwa ikulu kwenye vikao rasmi. Watajua laghai ya wajanja.

Ushauri wa bure, wakakae bungeni kama wabunge wengine wasiokuwa na wizara. Wakajikite kwenye kuichambua serikali kwa kuisimamia, kuikosoa na kutunga sheria zenye faida kwa nchi.
Ndivyo ilivyo. Wamepigwa changa la macho!

Ogopa mwanasiasa anayeongea kwa upole. Anakupiga pini bila wewe kujijua. Ila hata wao wanajua wametemwa!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Acha makasiriko Mama kaamua najua mnaumia sana ila ndo hakuna namna!
Mkuu hakuna maamuzi yasiyofuata sheria, Kanuni na taratibu... naomba niambi3 uamuzi wake based kwenye sheria ipi, muundo upi? Ulipitishwa lini na Bunge?
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.

Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.

Ameambiwa awapige Pini kama Nyerere alivyoagizwa kuipiga Pini Zanzibar mpaka sultan akose pa kwenda ili aombe kwenda Uingereza.Yulebwa Oman aliagizwa asimookee hata kama ni ndugu yake.
 
Nani alikwambia ili(sio hili) uwe spika ni lazima uwe mbunge?Unapokuwa hujui jijulishe kwanza Ili uweze kujadili logic...
31AA7859-B02A-49F9-9311-5969C49A037E.jpeg

Kubishana na watu kama nyie ni shida.

Umeshawahi kuona kuna bunge lolote duniani, senate, congress; au chombo chochote kinachosimamia serikali kinaongozwa na outsider?

Na unajua kwanini kimantiki ya siasa hilo aliwezekani?
 
Nani alikwambia mwanasheria mkuu wa serikali yupo chini ya wizara ya katiba na
Wewe ni mpuuzi kasome website yao kama ata simple logic ya kutambua taasisi za serikali zipo chini ya wizara gani inakushinda unata kuongea siasa kweli.
 
Wameshuka au wamepanda?
Wamepotezwa ili wasije zuia MWANAMKE KUKAMATA MUHIMILI MWINGINE, amini usiamini ukweli ndio huo. Na wangeachwa kwenye nafasi zao 2025 ingeweza sumbua kiushindani kwa kiti kama wangeamua kugombea.
 
View attachment 2076877

Kubishana na watu kama nyie ni shida.

Umeshawahi kuona kuna bunge lolote duniani, senate, congress; au chombo chochote kinachosimamia serikali kinaongozwa na outsider?

Na unajua kwanini kimantiki ya siasa hilo aliwezekani?
We boya, kila mtu mwenye sifa ya kuwa mbunge ni mbunge?Unajua kusoma?
 
Wewe ni mpuuzi kasome website yao kama ata simple logic ya kutambua taasisi za serikali zipo chini ya wizara gani inakushinda unata kuongea siasa kweli.
Unapenda kutaja neno logic lakini huna akili.Yaani bado unakomaa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali yupo chini ya waziri wa katiba na sheria?Hivi unajua bunge lina sehemu kuu ngapi we bwege?

Umesoma mpaka "choo" kikuu wewe,sio bure.
 
We boya,kila mtu mwenye sifa ya kuwa mbunge ni mbunge?Unajua kusoma?
Speaker atakuwa miongoni mwa wabunge

Atachaguliwa na wabunge au watu wenye sifa ya kuwa wabunge.

Unaweza badili mchakato wa kumpata speaker asipigiwe kura na wabunge; ukatafuta namna nyingine ya kuchaguliwa na watu wenye sifa za kuwa wabunge.

Lakini uwezi badili sifa ya speaker kuwa mmbunge au hata naibu wake; ndio maana Magufuli alimteua Dr Tulia kuwa mmbunge kwanza halafu akawa naibu speaker.

Ni ili kugombea tena unaibu speaker Tulia alihitaji jimbo maana teuzi za raisi sio guarantee; wewe na hao viazi huko Lumumba wanaowapa form watu kama kina Masele akili zenu sawa.

Hivi ata kusoma hujui.

Na niliikuliza unajua political logic behind that? Au unadhani sheria zinatungwa tu.
 
Unapenda kutaja neno logic lakini huna akili.Yaani bado unakomaa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali yupo chini ya waziri wa katiba na sheria?Hivi unajua bunge lina sehemu kuu ngapi we bwege?

Umesoma mpaka "choo" kikuu wewe,sio bure.
Nenda kasome website yao uone wapo chini ya wizara gani.

Nilishakwambia wewe ni mpuuzi hujui kitu unapayuka tu.
 
Unapenda kutaja neno logic lakini huna akili.Yaani bado unakomaa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali yupo chini ya waziri wa katiba na sheria?Hivi unajua bunge lina sehemu kuu ngapi we bwege?

Umesoma mpaka "choo" kikuu wewe,sio bure.

Ndio ujue ulivyo mjinga kusumbua kichwa kidogo uwezi kujiridhisha, kabla ya kuandika upuuzi.

Soma hiyo link yao uone ni taasisi ya wizara gani.

Again unajua kwanini AG wanaingia bungeni, kwenye nchi zote ambazo katiba yake ni unitary systems?

Maana inaonekana ukimuona AG bungeni unadhani na ofisi yake ni sehemu ya bunge.

Hii mifumo sisi tumeiga tu walioitunga wana principles behind mngekuwa mnasoma vitabu vya siasa huu upuuzi mnaoandika ungepungua.
 
We mpuuzi nimekuuliza unajua sehemu kuu za bunge?
 
Speaker atakuwa miongoni mwa wabunge

Atachaguliwa na wabunge au watu wenye sifa ya kuwa wabunge.

Unaweza badili mchakato wa kumpata speaker asipigiwe kura na wabunge; ukatafuta namna nyingine ya kuchaguliwa na watu wenye sifa za kuwa wabunge.

Lakini uwezi badili sifa ya speaker kuwa mmbunge au hata naibu wake; ndio maana Magufuli alimteua Dr Tulia kuwa mmbunge kwanza halafu akawa naibu speaker.

Ni ili kugombea tena unaibu speaker Tulia alihitaji jimbo maana teuzi za raisi sio guarantee; wewe na hao viazi huko Lumumba wanaowapa form watu kama kina Masele akili zenu sawa.

Hivi ata kusoma hujui.

Na niliikuliza unajua political logic behind that? Au unadhani sheria zinatungwa tu.
We fala,hatuongelei naibu spika.Naibu spika yes ni lazima awe mbunge.Spika anaweza kuwa mtu yeyote mwenye sifa za kuwa mbunge.Hivyo anaweza kutoka ndani au nje ya bunge.Hiyo katiba uliyoiweka hapo juu ndo inasema hivyo.

Unajua kusoma lakini huelewi mantiki.... pole..Ndivyo mlivyo wasomi wa vyoo vikuu!!Steven Masele ni mbunge wa wapi?Sasa mbona amechukua fomu ya kugombea uspika?Unajua kuwa chadema waliwahi msimamisha Mabere Marando agombee uspika kupitia chadema na hakuwa mbunge?
 
We mpuuzi nimekuuliza unajua sehemu kuu za bunge?
Bunge lina sehemu nyingine yeyote zaidi ya kufanya kazi ya kutunga sheria (realistic kupitisha) na kusimamia serikali.

Hakuna siri nyingine yeyote ya majukumu ya bunge.
 
Bunge lina sehemu nyingine yeyote zaidi ya kufanya kazi ya kutunga sheria (realistic kupitisha) na kusimamia serikali.

Hakuna siri nyingine yeyote ya majukumu ya bunge.
Ok nimeshajiridhisha kuwa hatuwezi kujadili hilo suala.Kama hujui sehemu kuu za bunge huwezi kuelewa mantiki yangu ya kukataa kuwa Attorney General hayupo chini ya kawizara chochote ..Uwe na wakati mwema
 
Haya
 
We fala,hatuongelei naibu spika.Naibu spika yes ni lazima awe mbunge.Spika anaweza kuwa mtu yeyote mwenye sifa za kuwa mbunge.Hivyo anaweza kutoka ndani au nje ya bunge.Hiyo katiba uliyoiweka hapo juu ndo inasema hivyo.

Unajua kusoma lakini huelewi mantiki.... pole..Ndivyo mlivyo wasomi wa vyoo vikuu!!Steven Masele ni mbunge wa wapi?Sasa mbona amechukua fomu ya kugombea uspika?Unajua kuwa chadema waliwahi msimamisha Mabere Marando agombee uspika kupitia chadema na hakuwa mbunge?
Na hapa pia upo sawa, ila kuna nchi yoyote duniani unaweza tutajia yenye katiba yoyote federal au unitary; Kiongozi wa house sio member.
 
Back
Top Bottom