Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Mkuu hapo umeongea jambo la msingi sana nitalizingatia pia
kuna kosa dogo hapo..usitafute pesa kuwa bora pesa itakutafuta wewe.. wekeza kwako (mind,body/energy and spirit) kiasi kwamba ukitokezea,ukiongea nk you can't be ignored...thats how you become money ,thats how you become great.Goodluck 🙂
 
Uchumi mzuri ndo
Uchumi mzuri ndo makeup ya mwanamme. Usitafute pesa wala kusubiri kupewa. Jijengee mifereji ya mafanikio kupitia mfumo wa mzunguko mzuri wa thamani. Utajiri hauji kwa kazi kubwa wala kuiba, bali kwa kutatua shida za jamii.

Jifunze kutumia pesa pungufu ya kile unachokipata. Embrace the 5 to 25 money principle.

Kuwa na mifereji mingi ya kipato.

Punguza muda na TV.

Kuwa na familia ni bora kuliko kuwa single. Ukipata mwanamke mzuri, mshukuru Mungu. Ila usimtwishe mzigo wa punda na kumfanya kuwa begi la mgongoni.

Ukipata unayedhani ni mbaya (na hili ukagundua baada ya kuoa. Bora asiwe muuaji), komaa na msaidie kuimprove. Usihangaike kumtafuta Mrs perfect (labda akuache). Utatawanya mibaraka yako. Na epuka nyumba ndogo.

ACHANA na picha za uchi na kupiga punyeto. Hazitakusaidia.

Jenga Imani yako. Maisha ina panda shuka za ajabu. Mungu ndo gundi ashikaye vyote (the center that glues everything together).

Usihesabu rafiki zako kwa Idadi, bali kwa thamani (count your friends by value not quantity). Epuka wasindikizaji. Utawajua maisha yanapogeuka.

Tafuta mentors. Hujui kila kitu. Watakusaidia kufika uendako haraka.

Jali afya yako. Usile wala kunywa wala kuvuta chochote Cheney atari. Jali hasa afya ya akili. Acha kujihurumia hurumia na kuwa na mawazo hasi. Wewe ni mtu wa thamani.
Amini hivyo. Utajiri huanza akilini.

Embrace failure. Kubali kufeli. Ni mchakato wa kukua. Jaribu tena na tena mpaka utoboze.

Mwisho, education is overrated. Watu huchanganya shule (schooling) with elimu (education). Tafuta elimu ya kweli. Usipumbazwe na nadharia ya kusoma sana shule dhidi ya kutafuta elimu ya kudumu.

Maisha yote dhamiria kujifunza (embrace lifelong learning). Soma vitabu kadhaa vinavyoendana na unachotaka kukifanya. Halafu apply. Rinse and repeat.
 
Barikiwa kwa hekima nzuri mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…