"Ficha vyanzo vyako vya mapato. Waonyeshe matumizi."
Usiwe mwepesi wa kutoa toa misaada wakati bado uchumi wako haujakaa sawa,kwasababu hao unaowasaidia hawatakusaidia siku ukiyumba kiuchumi.
Usimuamini mtu kupita kiasi hata kama ni ndugu yako maana adui wa mtu ni wa nyumbani mwake mwenyewe.
Nakupa mfano. Kuna watu walitafuta taarifa zangu lakini wakazikosa, baadaye nikawa ninaona baadhi zinavuja, nikafuatilia na kugundua kumbe ndugu yangu ndiye anayezitoa, kuchimba zaidi nikajua huwa wanamlewesha sana kwasababu udhaifu wake uko kwenye pombe,kila akiulizwa swali anajibu kama anavyolijua.
Nilivyojua nikawa nampa za kawaida sana,kisha nikamuhamisha mkoa,huko aliko hawamjui na wala hajui kinachoendelea huku kwangu.
Kuwa makini na vyakula unavyokula hasa vya kupikiwa kibinafsi,kutengewa chakula chako mwenyewe wakati mpo wengi.
Kuweni wasiri wa mambo yenu,mishe zenu,michongo yenu,kazi zenu.
Mtu akikuuliza unafanya kazi wapi,na wewe muulize natafuta kazi ,vipi huko kwako naweza kupata nafasi?
Wengi ni 'masnitch' msiwaamini kazi yao ni kuharibia wengine.
Ukifanikiwa usiwasahau wazazi,watoto yatima,masikini ,wajane,ndugu na Mungu.