Mabadiliko NHIF kama huna uwezo utakufa, hakuna nafuu yoyote zaidi ya kutafuta pesa kwa nguvu kutoka kwa wananchi

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
NHIF wamefuta Najali ambayo mtu mmoja alikua analipa 192,000/=, Wekeza 384,000 na Timiza 516,000/=

Wametambulisha vifurushi vipya ambavyo ni Serengeti Afya 660,000 na Ngorongoro Afya 240,000 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Wamebadili kifurushi cha watoto ambacho awali kwa mtoto ambaye bado hajaanza shule alikua analipiwa 50,400 na sasa atalipa 150,000 na anatakiwa kusubiri miezi 3 ndio aanze kutumia huduma.

Kwa watoto walio shule wanalipa 50,400 na hakuna muda wa kusubiri, anaanza huduma pale pale.
20241218_111057.jpg
 
Kwa nchi zinazo jielewa sekta ya afya ni muhimu naya kuzingatiwa zaid lakini Useless breather walio juu wanafia india .
 
Siku mkiacha kupeleka kundi la watu 70 wa Bongo Muvi Korea, Msafara wa Rais kuwa na utitiri wa V8 au kununua magoli ya Simba, Yanga na Taifa stars kwa mamilioni na pesa hizo zikawekezwa kwenye afya labda tutapata unafuu wa michango
 
Kama Taifa tuna safari ndefu sana , hospital zenyewe hazina madawa ,wahudumu wachache halafu suluhisho ni kuongeza gharama za matibabu kutoka 50,400 Hadi 150000,huku wakubwa wakiwa wanatibiwa nje ya nchi.Maskini wa kitanzania wataendelea kufia kwenye milango ya zahanati kama MARIAM ZAHORO wa Handeni.Alipofariki kwa kukosa 150,000 ili afanyiwe operation,wameona kumbe 150,000 unaweza kumfisha mtu ,wameamua kuweka kifurushi hicho ili raia washindwe kulipia na hatimaye wafariki wakiwa wanajiona.Eeee Mungu wetu tunakuomba Kila mkubwa alipelekwe India kwa ajili ya matibabu basi asirudi nchini na akirudi arudi akiwa maiti.
 
ujinga ni mzigo, inakuwaje mtu afikieie matibabu yatakuwa rahisi au bima kwawote kwa nchi isiyo na viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba... tafuteni pesa
 
Hii nchi naona kama IMEOZA..sjawah kuona nchi inayotafuta pesa nyingi kwa nguvu kwa maskini.
 
Hongera kwa NHIF kwa kuzidisha gharama za kuchangia, na huo mfuko IPO siku utajitangaza kwamba unajiendesha kwa hasara

Wachangiaji watabaki kuwa ni wafanyakazi wa serikali ambao wanakatwa michango kwa lazima
 
ujinga ni mzigo, inakuwaje mtu afikieie matibabu yatakuwa rahisi au bima kwawote kwa nchi isiyo na viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba... tafuteni pesa
Kwani wakati wa Nyerere wa sera za tiba bure na elimu bure kwa umma, ilikuwaje akaweza?
 
Kama Taifa tuna safari ndefu sana , hospital zenyewe hazina madawa ,wahudumu wachache halafu suluhisho ni kuongeza gharama za matibabu kutoka 50,400 Hadi 150000,huku wakubwa wakiwa wanatibiwa nje ya nchi.Maskini wa kitanzania wataendelea kufia kwenye milango ya zahanati kama MARIAM ZAHORO wa Handeni.Alipofariki kwa kukosa 150,000 ili afanyiwe operation,wameona kumbe 150,000 unaweza kumfisha mtu ,wameamua kuweka kifurushi hicho ili raia washindwe kulipia na hatimaye wafariki wakiwa wanajiona.Eeee Mungu wetu tunakuomba Kila mkubwa alipelekwe India kwa ajili ya matibabu basi asirudi nchini na akirudi arudi akiwa maiti.
MAOMBI yako makalii sanaa
 
Back
Top Bottom