Mabadiliko NHIF kama huna uwezo utakufa, hakuna nafuu yoyote zaidi ya kutafuta pesa kwa nguvu kutoka kwa wananchi

Mabadiliko NHIF kama huna uwezo utakufa, hakuna nafuu yoyote zaidi ya kutafuta pesa kwa nguvu kutoka kwa wananchi

Mimi awali nilikua natumia Ile ya kulipia 50400 ambayo wanafunzi wengi vyuon wanatumia, vip kwa Sasa inatakiwa ni update au nikate bima nyingne maan sipo chuoni tena
 
Halafu ukienda na kadi ya NHiF hospital kuna huduma nyingi tu unaambiwa ulipie cash mwenyewe maana hiyo bima haihusiki

Upo sahihi, hospitali wanasema vipimo au dawa fulani hazipo ktk orodha ya kugharamiwa na bima, huu ni utapeli

Na zipo baadhi ya hospitali mwanachamq wa bima ana dharauriwa na kupata tabu kuliko yule anayelipa kwa cash
 
ujinga ni mzigo, inakuwaje mtu afikieie matibabu yatakuwa rahisi au bima kwawote kwa nchi isiyo na viwanda vya kutengeneza madawa na vifaa tiba... tafuteni pesa

Kaa kmya maana ujui maana ya bima

Inapaswa huduma zao ziwe nafuu ili wachangiaji wawe wengi ili wale wachache wanao umwa waweze kugharamiwa

Kuongeza gharama za michango kutapunguza wachangiaji, na gharama za kuendesha huo mfuko zitakuwa vilevile au kuongezeka
 
Kaa kmya maana ujui maana ya bima

Inapaswa huduma zao ziwe nafuu ili wachangiaji wawe wengi ili wale wachache wanao umwa waweze kugharamiwa

Kuongeza gharama za michango kutapunguza wachangiaji, na gharama za kuendesha huo mfuko zitakuwa vilevile au kuongezeka
wewe ndo hujui chochote unalalama tu ..kenge
 
Kama Taifa tuna safari ndefu sana , hospital zenyewe hazina madawa ,wahudumu wachache halafu suluhisho ni kuongeza gharama za matibabu kutoka 50,400 Hadi 150000,huku wakubwa wakiwa wanatibiwa nje ya nchi.Maskini wa kitanzania wataendelea kufia kwenye milango ya zahanati kama MARIAM ZAHORO wa Handeni.Alipofariki kwa kukosa 150,000 ili afanyiwe operation,wameona kumbe 150,000 unaweza kumfisha mtu ,wameamua kuweka kifurushi hicho ili raia washindwe kulipia na hatimaye wafariki wakiwa wanajiona.Eeee Mungu wetu tunakuomba Kila mkubwa alipelekwe India kwa ajili ya matibabu basi asirudi nchini na akirudi arudi akiwa maiti.
"Blaza" kwani kwenu hakuna WAKUBWA...!? au wapo ila India unahisi kama hawawezi kwenda...!?😁
 
Natamani niandike hapa jinsi serikali kupitia mlango wa nyuma wanachofanya pesa za wanachama, na wakati huo huo wakurugenzi wanatumiwa vimemo "tunaomba michango kwa ajili ya ziara ya @#** hapa Wizarani" naye ili kulinda uteuzi wake anatoa Tu pesa, watumishi mfuko nao wanaomba fungu kwa ajili ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfumo, wahamasishaji ni Amisa Mobeto na Gigy Money" uchafuzi ni mwingi acha tu nisiharibu siku yangu bure, nimeshiba michembe yangu ya majani ya kunde,
 
Siku mkiacha kupeleka kundi la watu 70 wa Bongo Muvi Korea, Msafara wa Rais kuwa na utitiri wa V8 au kununua magoli ya Simba, Yanga na Taifa stars kwa mamilioni na pesa hizo zikawekezwa kwenye afya labda tutapata unafuu wa michango
Hii nchi inapesa ya kuchezea na kula bata ila siyo ya kufanyia maendeleo.. Pesa ya maendeleo ni mikopo ya Ughaibuni/IMF/ WB n.k
 
NHIF wamefuta Najali ambayo mtu mmoja alikua analipa 192,000/=, Wekeza 384,000 na Timiza 516,000/=

Wametambulisha vifurushi vipya ambavyo ni Serengeti Afya 660,000 na Ngorongoro Afya 240,000 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Wamebadili kifurushi cha watoto ambacho awali kwa mtoto ambaye bado hajaanza shule alikua analipiwa 50,400 na sasa atalipa 150,000 na anatakiwa kusubiri miezi 3 ndio aanze kutumia huduma.

Kwa watoto walio shule wanalipa 50,400 na hakuna muda wa kusubiri, anaanza huduma pale pale.View attachment 3179380
Tutafuteni hela tu hakuna namna. Dunia ya sasa inanufaisha wachache sana.
 
Hapo hiyo huduma siyo ya mwaka tena, ni miez 9, uhun!
si miezi 9 usipotoshe, mfano umelipa desemba mosi 2024 utaanza kuitumia machi mosi 2025 na mwisho wa matumizi ya kadi yako ya nhif utakuwa februari 28 mwaka 2026.
 
Okay, kwan hizo zinawahusu wafanyakaz au sis tu wengine?

Ujui hata hiyo NHIF inajiendeshaje kwa mapato kutoka wapi

Kwa kifupi hakuna mfuko una hoja za mkaguzi wa mahesabu CAG kama huo unaitia tu hasara serikali na kuwaibia wanachama wake
 
Back
Top Bottom