PreGE2025 Mabalozi watakaohudhuria kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu et al, Wafukuzwe kutoka nchini

PreGE2025 Mabalozi watakaohudhuria kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu et al, Wafukuzwe kutoka nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wajinga ndio waliwao.
Wapo wengi tu
unamkomoa Lissu ili iweje?
Unataka kusema hao mabalozi ndio watakaoenda kumuokoa Lissu kutoka lupango?
...hatahivyo namkomoa kivipi tena? Duh

Je familia yako itaendelea kuneemeka baada ya Tundu Lissu KUNYONGWA?
Hilo ni swali? Familia yangu ni Watanzania, Waafrika. Nani kasema anaenda kunyongwa?
Ujinga ni mzigo.
Kweli Ujinga ni mzigo, usiongeze mzigo huo.
 
Free to oppress others.
Why don't they monitor All trials including those in their own countries?

Wamemuacha Marie Le Pen akiangamizwa kwa style hii hii wanayodai ya mahakama na sheria kutumiwa kama silaha, mbona hawakutokea mahakamani. Na sio Ufaransa tu....Ulaya yote sasa hivi mwenendo ni huu huu.

Iweje watake kuja kujitokeza huku Mkuu?

Non-Interference SHOULD be Absolute.
 
Zamani nilikuwa nakuona mtu wa maana sana😂😂😂
Kwahiyo sasa, wewe ndio mtu wa maana.

Wewe umeshasema humu Jamiiforums kuwa ni Mshabiki kindakindaki wa Wamarekani.

Sishangai maoni yako.
 
Their mere attendance signals "International scrutiny", potentially swaying outcomes.

Ni kwamba vyombo vya serikali teyari vimefanya maamuzi ya kumtuhumu na kumpeleka mahakamani. Tunaweza kubaliana? Na kama wakihudhuria, hio teyari itakuwa wanaingilia masuala yetu ya ndani na hapa Mahakama

100%
Kwani hiyo international community ina impact gani? Sudan, Burkina Faso, Congo DR, South Sudan wamekuwa na impact gani mpaka muwatumie kuitisha Serikali yetu?
Au na wao ni dhaifu sana ndio maana wanajua Watanzania ni wapole basi watajitutumulia kwa Tanzania wakati kwingine watu wanakufa n hawafanyi chochote!??
 
Una laani unasema Mahakama itaingiliwa Mbona Daily Serikali ya Ccm inaingilia Uhuru wa Mahakama na hujawahi kukemea??
 
Chini ya kifungu gani cha sheria?
Montevideo Convention on the Rights and Duties of States ya 1993

UN General Assembly Resolution 2131 ya 1965-Declaration on the Inadmissability Of intervention

Vienna Convention on Diplomatic Relations...
...itoshe, zipo sheria mama za nchi husika zinazoweza kutumiwa kuwaondoa mabalozi ikiwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi.
 
Una laani unasema Mahakama itaingiliwa Mbona Daily Serikali ya Ccm inaingilia Uhuru wa Mahakama na hujawahi kukemea??
Nimesema, uhudhurio wao mahakamani ni kuingilia masuala ya ndani ya nchi.

Uhudhurio wao, uko politically motivated, yani unaviashiria vya kisiasa

hatahivyo siongelei CCM.


...mbona na wao hawakuonekana Ufaransa mahakamani? kama sio Unduminakuwili na unafiki wa kisiasa?
 
...na wale mahakimu wa Ufaransa hawakupigiwa simu?

Marie Le Pen kafungiwa kuingia kwenye chaguzi, na ukiwasikia wafaransa, wanasema Mahakama zimetumiwa na Serikali kumzima kisiasa.

Yale yale, na Lissu inasemekana amefunguliwa kesi kuzimwa kisiasa.

Kesi bado hazifanani?

Hayo yakiwa yanaendelea, sikusikia na wala sikuona Mabalozi kutoka nchi yeyote ile kutoka Ulaya wakihudhuria kesi ya Le pen.

Sasa kama waliheshimu mahakama zile, wanashindwa nini iuheshimu zetu?

Uwe unakuja kuandika Ukweli.

Ati sina akili? Kasome Uzi wako tena. Huu ni moto

huwezi kuwa na akili kubwa kama hii
Unafananisha tuhuma za Marie le pen na Lisu?
Le pen yeye ameapa kuwafukuza waislamu na wahamiaji kote ufaransa sasa lisu amesema anaingia msituni na silaha au analeta unasma kwenye jamii?
 
Watu gani.

Mabalozi sio watu wa kawaida tu, ni wawakilishi wa kigeni. Ni Nchi!

Kusikiliza ili iweje?
Ufaransa mahama zipo huru ndio maan rais wao wa zamani Nicolas Sarkozy pia katiwa hatiani kwa rushwa na sasa anapelekwa gerezani hwana sheria ya kulinda viongozi waovu kama Tanganyika eti rais hashtakiwi.
 
Kwanini uhudhurio wa mabalozi hawa lazima upingwe.

Soma pia

Katika miaka ya hivi karibuni, mabalozi wa kutoka Ulaya wamekuwa wakivuka mipaka yao wakiingilia michakato ya kisiasa na ya kisheria, serikali na mahakama kwenye Taifa letu huru la Tanzania huku wakipuuzia yanayojiri katila nchi zao.

Umduminakuwili huu uliyoonyeshwa waziwazi na kesi iliyomkabili Marine Le Pen mchini Ufaransa-ambapo hukusikia ama kuona mabalozi ama wanadiplomasia wa kigeni wakihudhuria-inazua swali la msingi:

Kwanini Wanadiplomasia hawa hawa wanataka kuhudhuria kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu na wenzake?

Watanzania wenzangu na wananchi wote wazalendo: Kufukuzwa kwa mabalozi hawa watakaohusika katika uingiliaji huu wa kimahakama sio tu utawatumia ujumbe kwamba waheshimu Charter ya Umoja wa Mataifa-Principles of Non-interference in domestic affairs, na sheria na kanuni zingine zinazoongoza wajibu wa Mabalozi hao wakiwa nchi za kigeni. e.g Montevideo Convention on the rights and duties of states, bali ni hatua ya lazima ili kulinda uhuru wetu, uhuru wa mahakama, na utawala wa kitaifa.

Wananchi, kwa kuruhusu mabalozi hawa kutoka Ulaya kuwa na ushawishi juu ya masuala ya kisheria, tena ya ndani, serikali ya CCM inajiweka mkao wa kibra, na kudhoofisha taasisi zetu za mahakama na kuondoa imani ya umma.

Tujiulize tu, ikiwa mahakama za Ufaransa zilipewa heshima na uhuru wake, kwanini nchi yetu haistahili kuheshimiwa?

Hivi mnajua athari za kuingiliwa-uhudhurio wa mabalozi-Kidiplomasia?

Wananchi tukemee na kutoa msimamo mzito, kwamba:
ili kuondoa unafiki na unduminakuwili huu, Serikali ni lazima ichukue hatua madhubuti:

Kuwafukuza mabalozi wote watakao ingilia masuala ya mahakama kutatuma ujumbe kuwa-our National sovereignty is non-negotiable

Wazuiliwe kufika mahakamani kuhakikisha kwamba haki inatolewa bila giliba kutoka nje.

Serikali idai mabalozi hao kuzingatia kanuni za kutoingilia kati masuala ya nchi yetu.

Diplomacy should not be an Instrument of coercion, yani kama wanathamini " 'true diplomatic intergrity' ",respect for sovereignty must be upheld universally-not just when politicaly convinient.


Wafukuzwe then utakula nini?
 
Kufukuzwa kwa mabalozi hawa watakaohusika katika uingiliaji huu wa kimahakama sio tu utawatumia ujumbe kwamba waheshimu Charter ya Umoja wa Mataifa-Principles of Non-interference in domestic affairs, na sheria na kanuni zingine zinazoongoza wajibu wa Mabalozi hao wakiwa nchi za kigeni.
 
Umduminakuwili huu uliyoonyeshwa waziwazi na kesi iliyomkabili Marine Le Pen mchini Ufaransa-ambapo hukusikia ama kuona mabalozi ama wanadiplomasia wa kigeni wakihudhuria-inazua swali la msingi:
 
Back
Top Bottom