PreGE2025 Mabalozi watakaohudhuria kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu et al, Wafukuzwe kutoka nchini

PreGE2025 Mabalozi watakaohudhuria kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu et al, Wafukuzwe kutoka nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Acheni kuonea watu kwa visingizio kuwa ni mambo ya ndani, kuwabambikia kesi wapinzani kwa njia haramu za kishetani siyo mambo ya ndani ya ccm , acheni mabalozi wajionee uonevu wa ccm
Umesema vizuri.

Swali la msingi: Mbona hatukuwaona mabalozi kutoka nchi hizo za Ulaya wakikusanyika Paris kwenye kesi ya Marie Le Pen?

Kesi ya Le Pen sio ya kisiasa?
 
The recall of Diplomats in judicial meddling is not an overreaction-it is a logical repsonse to violation of sovereingnty.

We must assert our judicial independence. We must remain free from external pressure.
kiingereza unajua ila akili ndio huna. Unamtegemea baba yako akulishe halafu unauliza anaingiliaje ugomvi wako na mdogo wako...
 
kiingereza unajua ila akili ndio huna. Unamtegemea baba yako akulishe halafu unauliza anaingiliaje ugomvi wako na mdogo wako...
Onyesha hio akili yako basi, au ndio huu utumbo ulioandika?
 
Kwanini uhudhurio wa mabalozi hawa lazima upingwe.

Soma pia

Katika miaka ya hivi karibuni, mabalozi wa kutoka Ulaya wamekuwa wakivuka mipaka yao wakiingilia michakato ya kisiasa na ya kisheria, serikali na mahakama kwenye Taifa letu huru la Tanzania huku wakipuuzia yanayojiri katila nchi zao.

Umduminakuwili huu uliyoonyeshwa waziwazi na kesi iliyomkabili Marine Le Pen mchini Ufaransa-ambapo hukusikia ama kuona mabalozi ama wanadiplomasia wa kigeni wakihudhuria-inazua swali la msingi:

Kwanini Wanadiplomasia hawa hawa wanataka kuhudhuria kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu na wenzake?

Watanzania wenzangu na wananchi wote wazalendo: Kufukuzwa kwa mabalozi hawa watakaohusika katika uingiliaji huu wa kimahakama sio tu utawatumia ujumbe kwamba waheshimu Charter ya Umoja wa Mataifa-Principles of Non-interference in domestic affairs, na sheria na kanuni zingine zinazoongoza wajibu wa Mabalozi hao wakiwa nchi za kigeni. e.g Montevideo Convention on the rights and duties of states, bali ni hatua ya lazima ili kulinda uhuru wetu, uhuru wa mahakama, na utawala wa kitaifa.

Wananchi, kwa kuruhusu mabalozi hawa kutoka Ulaya kuwa na ushawishi juu ya masuala ya kisheria, tena ya ndani, serikali ya CCM inajiweka mkao wa kibra, na kudhoofisha taasisi zetu za mahakama na kuondoa imani ya umma.

Tujiulize tu, ikiwa mahakama za Ufaransa zilipewa heshima na uhuru wake, kwanini nchi yetu haistahili kuheshimiwa?

Hivi mnajua athari za kuingiliwa-uhudhurio wa mabalozi-Kidiplomasia?

Wananchi tukemee na kutoa msimamo mzito, kwamba:
ili kuondoa unafiki na unduminakuwili huu, Serikali ni lazima ichukue hatua madhubuti:

Kuwafukuza mabalozi wote watakao ingilia masuala ya mahakama kutatuma ujumbe kuwa-our National sovereignty is non-negotiable

Wazuiliwe kufika mahakamani kuhakikisha kwamba haki inatolewa bila giliba kutoka nje.

Serikali idai mabalozi hao kuzingatia kanuni za kutoingilia kati masuala ya nchi yetu.

Diplomacy should not be an Instrument of coercion, yani kama wanathamini " 'true diplomatic intergrity' ",respect for sovereignty must be upheld universally-not just when politicaly convinient.
Unawashwa Nini subiri dawa iingie vizuri mbona wakati mnataka maokoto husemi hayo?
 
Ukiona ushauri kama huu unatolewa jua hakuna haki inayotendeka kwenye hizo mahakama, bali sheria zinatumika silaha ya kukomoa wakosoaji wa serekali. Mbona hao mabalozi huwa wanashiriki kwenye hafla nyingine na hutaki wazuiwe? Sovereignity sio kwa ajili ya kuficha ukandamizaji wa madai halali.
Nauliza, mbona hawakuenda kwenye kesi inayofanana na hii ya Marie Le Pen wa Ufaransa?

Ukiweza kujibu nitafuta Uzi
 
Nauliza, mbona hawakuenda kwenye kesi inayofanana na hii ya Marie Le Pen wa Ufaransa?

Ukiweza kujibu nitafuta Uzi
Huko mahakama ni huru, hata wasipoenda kuna mazingira ya mahakama zao kuaminika.
 
Back
Top Bottom