Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Lugha unazotumia zinaonyesha hauko smart, acha ushabiki maandazi, jikite kwenye hoja yako.
 
Hatutaki porojo mkataba umesha kuwa na mashaka upelekwe bungeni watu wapewe muda kuusoma then wajadili vinginevyo ni uhujumu uchumi full stop.
Kama ulivyowahi kupelekwa bungeni mkataba upi?
Akili ya kawaidatu inakataa kukubali kwamba mchina ataruhusu bandari nyingine zifanye kazi, mchina hataruhusu maana patakuwa na ushindani na itapelekea kuchelewesha kurudisha garamazao za uwekezaji.
Na kwanini basi Dar es salam Maritime Gateway Project ilikuwa inaenda sambasamba na miradi mingine, ukiwemo Mradi wa Bandari ya Bagamoyo?

Unajua nyie watu sijui vp! Yaani Mchina aigope bandari hii hii moja wakati kuna nchi zina msururu wa bandari na bado watu wanawekeza kwenye projects mpya!
Vinginevyo bandari zote zitakufa zenyewe kwakuwa zitakosa mbinu za kushindana na hiyo bandari ya kisasa ya bagamoyo kwenye viwezeshi, pia wanaweza kuzielekeza melizao na nyingine watakazoweza kupitisha mizigo bagamoyo na kuathiri bandarizetu.
Kwanini zife? Nimekwambia role kubwa ya Bandari ya Bagamoyo ilitarajiwa kuwa transshipment port, na pia kuhudumia industrial park iliyokuwa inarajiwa kujengwa sambamba na mradi!

Kwa sasa kuna bandari ipi TZ inayofanya hizo roles hadi uamini zitakufa?
Mkataba uwekwe wazi, ujadiliwe.
Kama hatutaweza kupata kodi inayolingana na mapato tunayo pata sasaivi katika bandarizetu na yanayo kuwa kila mwaka, itakuwa ni ujuha wakiwango cha lami kukubali huo mradi.
Hilo la mkataba kuwekwa wazi litakuwa limeandika historia mpya Tanzania kwa sababu hata watunga sheria wenyewe (Wabunge) ni nadra sana kupata fursa ya kuiona hii mikataba!!
 
Mkuu je ni mkataba upi umewahi kuwekewa wazi ukaujadili? Songas? SGR? Manunuzi ya ndege? JNIA T3? NK. Jikite kwenye mada...
 
Lugha unazotumia zinaonyesha hauko smart, acha ushabiki maandazi, jikite kwenye hoja yako.
Unaweza kunikumbusha ni wapi hasa nimewahi kusema kwamba "I'm smart"!

Btw, umeangalia hiyo mada ilikotokea? Umeangalia huyo jamaa alivyoibuka from nowhere na kuanza kunimwagia matusi?!

Umejaribu kumwambia huyo mmwaga matusi kwa watu hayo unayosema hapa? Kama sio, sasa ni nani shabiki maandazi kama sio wewe mwenyewe?!
 
Mkuu 1000, unajitahidi sana kuniondoa kwenye mada hii nzuri ya mkuu Chige, na kiukweli unashawishi hasa, kwa sababu mawazo hayo yako napingana nayo kwelikweli.
Lakini, hayo tuyajadili siku nyingine. Leo ni hii mada ya Bagamoyo na ushawishi alionao mkuu Chige juu yake.

Bado sikubaliani kamwe na hiyo dhana yako katika maandishi hayo hapo juu.
 
Lugha unazotumia zinaonyesha hauko smart, acha ushabiki maandazi, jikite kwenye hoja yako.
Umejisahaulisha kuwa hata Spika alisema "Walishauriwa vibaya kuhusu mradi huo..." je hukumbuki kuwa anataka waujadili...?"
Kujitoa akili ni jambo moja ila kujitoa ufahamu ni jambo jingine...
 
Mkuu hawezi kuona hayo wala kumkemea "yule.." ni WALEWALE ukitazama vyema "nyayo na visigino vyao"
 
SGR haiwezikuwa ndio sababu ya kuruhusu huo mradi.
Watu wana njiazao nyingine za kusafirisha mizigoyao, usijifanye mgeni na hii nchi Pasco, kumbuka SGR ni ya serikali ikitokea ukapata viongizi ambao sio wazalendo wata ihujumi hiyo reli ili maroliyao na ya washirika wao yafanye kazi, tunauzoefu wa mambo hayo.

Hapa tuangalie mkataba kama utatufanya kupata mapato sawa na tunayo pata sasaivi kwenye bandarizetu vinginevyo tumeliwa.
 
Kwa kifupi ni WANAFIKI wanaotaka kuvaa joho lisilowatosha UZALENDO...
Mada imezidi upeo wao...
 
Mkuu "hatupendi vitu vyenye akili wala kufikirisha.." ndio maana hatujibu hoja bali kushangilia kila msala upitao HUO NDIO UZALENDO WETU!!
 
Mkuu je ni mkataba upi umewahi kuwekewa wazi ukaujadili? Songas? SGR? Manunuzi ya ndege? JNIA T3? NK. Jikite kwenye mada...
Huu wa bandari ya bagamoyo ukiwa wa kwanza sita shangaa sababu unaleta utata kwakuwa mkuu wa nchi aliupinga waziwazi na sasa baada ya kifochake tunautaka urudi ndio maana tunataka uwekwe wazi tujue nini kiko sahihi.
 
Mkuu Chige,, hii ni mada uliyoifanyia kazi. Ni wazi uliweka muda kuiandaa na kuiwasilisha.

Kwa hilo nakupongeza sana, kwani ni nadra sana hapa JF kusoma mada zilizoandaliwa vyema; zikafanyiwa utafiti na kukusanya ushahidi juu ya yanayowasilishwa. Hii imekuwa nadra sana siku hizi hapa JF.

Baada ya kusoma sehemu zote ulizoziweka hapa, mawazo yangu ya mwanzo kabisa niliyochangia katika bandiko langu la mwanzo yanabaki vile vile, na pengine kuyatilia mkazo zaidi.

Bagamoyo ni yetu, tutaamua vyovyote tutakavyo ona ni vya manufaa kwa taifa letu.

Hatuwezi kuingia tu kwenye mradi, eti kwa sababu tu tusichelewe, na fursa hiyo ikanyang'anywa na watu wengine. Huo hauwezi kuwa msingi wa maamuzi yetu.

Maendeleo ya Tanzania hayawezi kutegemea mradi mmoja tu, kiasi kwamba usipotekelezwa hatuwezi kujiletea maendeleo kwa kufanya mambo mengine.

Tatizo tu na andiko lako refu vile, kwanza inakuwa vigumu kwa wasomaji wengi wa hapa JF kulihimili. Wengi wetu hapa ni wa vi-mistari miwili, sana sana mistari mitano.
Kwa hiyo, hata katika kujibu inabidi labda kila sehemu ijibiwe kivyake, bila kuangalia ujumla wa mada nzima.

Labda nichukue tu sehemu moja ndogo inayomhusu Kakoko.

Wewe ume-'dismiss' mno aliyokuwa anasema na yote kuyasema kuwa ni uongo! Na badala yake, umechukulia ya huyo Mchina kuwa ndiyo ya ukweli, hata kama umefanya 'deductions' tu katika matamshi yao. Huna ushahidi wowote wa moja kwa moja kutoka pande zote mbili.

Mi nadhani, ingesaidia pia, kama ungechukua mifano mingine, zaidi ya hizo bandari za Greece na Sri Lanka kuongeza uzito katika mada yako. Tuna mfano mzuri sana wa mradi wa mchina hapa jirani yetu, huo wa SGR hapo juu. Kuna mambo mengi yanayojulikana juu ya mradi huo, na hata yale yasiyotakiwa kufahamika (mchina hataki yafahamike); lakini yamekuwa yakitoka taratibu na kujenga taswira isiyopendeza.

Ya pembeni: Mchina aliwahi kutujengea TAZARA, safi kabisa, bila ya masharti magumu wala nini. Tumeshindwa tu sisi wenyewe kuitumia na jirani zetu Zambia kwa manufaa. Hiyo ilikuwa enzi hizo, hizi ni enzi hizi. Mchina na "Mabeberu" siku hizi hawapishani sana!

Hata hivyo, tuonbe atuimarishie reli yetu hiyo ili tuitumie kwa ufanisi, huku tukiangalia ni jinsi gani tutakavyoshiriki kwenye BRI.
 
Story ndefu aina kichwa wala miguu ujajibu hoja za Kakoko hata moja.

Hakuna mahala Kakoko kaongelea mabeberu yeye alijikita purely on financial aspect za mradi na concession ambazo wachina wanataka wapewe.

Halafu huko kwenye kodi ndio salalee umeboronga hatari. Vitu vingine tuwaachie wataalamu serikalini au tuone terms za mradi wenyewe.

Not sure ata kama unaelewa at what point capital allowance is claimed and it has nothing to do VAT.
 
Watu wa JK mnapoteza muda, hakuna asiyeona umuhimu wa huo mradi; Tatizo masharti ya mradi
 
Watanzania wengi tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii hili ni tatizo kubwa sana. Leo hii mizigo mingi inakwenda Rwanda, Uganda, Congo inapitia Kahama kwa ya barabara na kusababisha barabara zetu zisidumu kwa muda mrefu bado tu mnaona hakuna mzigo wa kuirisha Sgr? Bado hamuoni kuwa Sgr itasafirisha mzigo mkubwa kwa muda mfupi na gharama nafuu?
 
Sawa...
Ila unapomlaumi Kakoko wakati yeye aliyarudia maneno ya JPM ndo sikuelewi...
 
Sio mbaka useme kama wewe ni smart ama sio, watu watakupima tu haijalishi.

Mi nimekushauri ujikite kutetea hojayako maana umeandika sana, tuliza akiliyako.
 
Kwanini unamiamini kakoko ?upi uhakika wa kile alichokisema?
 
Nimegindua kuwa wengi wetu tunapinga au kukubali utekelezaji wa mradi wa bandari ya Bagamoyo huku tukiwa hatujui chochote ila ima tutapinga au tutakubali Cha ajabu pia hatuingizi akili zetu katika kuchambua Mambo ya msingi yanayoambatanishwa ktk mradi huu zaidi ya kuzishabikia propaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…