Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Asante kwa kuiba post yangu instagram account yenye jina la @kelvinkibenje hata hivyo si mbaya kwani lengo ni kusaidiana. Aya wanaotaka machimbo zaidi na elimu ya biashara mnaweza kwenda instagram kuna post nyingi mtapata kitu. Serch @kelvinkibenje
Ni nani anakushonea suit jacket linakuwa linaning'inia kama la mtoto? Ungepata fundi mzuri ungeshona jacket la heshima siyo linalobembea juu juu utadhani umechukua la mdogo wako (jacket namaanisha nyie mnaloita koti) huwa lina vipimo vyake siyo mnavyo vaa siku hizi inakuwa kama umevaa kitop.
 
Nipe chimbo la mashati original au t shrts ,mfano wa heat gear fabrics au nike dri fit.
Sitaki midosho ambayo ukifua mara moja inapauka
Na mtaa wenye machimbo ya nguo za watoto
Ndugu wakati nataka kuanza likizo; nipo tayari kujitolea jambo hili kwa kushirikiana na mleta hoja na wengine wote wanaojua machimbo na wenye majitaji.

Kwa mwenye uhitajiwa wa bidhaa weka bei unayotaka kununulia. Weka picha ya bidhaa hiyo.

Mimi nitakwenda kulitafuta chimbo na nitawawekea hapa namba ya muuzaji moja kwa moja. No udalali
 
Asante mkuu ,Sasa Mimi nataka vitambaa vya vijora vile plain natengeneza mwenyewe vijora vya batiki Ila sipo dar natamani kujua Bei yake wanauzaje lile jora zima?
 
Asante kwa kuiba post yangu instagram account yenye jina la @kelvinkibenje hata hivyo si mbaya kwani lengo ni kusaidiana. Aya wanaotaka machimbo zaidi na elimu ya biashara mnaweza kwenda instagram kuna post nyingi mtapata kitu. Serch @kelvinkibenje

Post yako instagram imeandikwa 2days ago

Hii post nayo 11/11

Hapo nani kamwibia mwenzake? Au mnashare mawazo? Au ni ID Mbili mtu mmoja!?
 
Ni nani anakushonea suit jacket linakuwa linaning'inia kama la mtoto? Ungepata fundi mzuri ungeshona jacket la heshima siyo linalobembea juu juu utadhani umechukua la mdogo wako (jacket namaanisha nyie mnaloita koti) huwa lina vipimo vyake siyo mnavyo vaa siku hizi inakuwa kama umevaa kitop.

Ila weee jamaa [emoji119][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukifika Big bon vuka upande wa pili unaotazamana na Big Bon wa barabara kubwa ya mwendokasi na upite kichochoro chochote kuingia huo upande huo kuelekea Magharibi utaanza kuyaona maduka na utatokea upande barabara wa Daladala za kwenda SINZA Makumbusho,( zamani mbezi). Utaona Maduka yapo pande zote za barabara
Naomba kufahamu maduka ya jumla ya maziwa, pampers na vifaa/ vyombo vya watoto
 
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.
_
Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.
_
Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.
_
Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.
_
Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .
_
Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.
_
Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.
_
Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.
_
vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.
_
Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani
_
Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.
Umeupiga mwingi sana,hongera mkuu maana huu uzi utatusaidia wengi mno[emoji120]
 
Post yako instagram imeandikwa 2days ago

Hii post nayo 11/11

Hapo nani kamwibia mwenzake? Au mnashare mawazo? Au ni ID Mbili mtu mmoja!?
Angalia muda nani kaanza. Pia insta yangu kuonyesha machimbo ni zaidi ya mara moja, ni kawaida kushare ujumbe.

Hata hivyo hajafanya vibaya. Lengo ni kusaidiana
Ni nani anakushonea suit jacket linakuwa linaning'inia kama la mtoto? Ungepata fundi mzuri ungeshona jacket la heshima siyo linalobembea juu juu utadhani umechukua la mdogo wako (jacket namaanisha nyie mnaloita koti) huwa lina vipimo vyake siyo mnavyo vaa siku hizi inakuwa kama umevaa kitop.
Kweli. Hiyo ni kutokana na kipato. Suti unapata mzuri kulingana na bei.
 
Back
Top Bottom