Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Hivi watu huwa wanasikiliza sababu au basi wao wanafuata maneno ya marehemu tu. Hakuna nchi duniani itakayoendelea bila kuwa na uwekezaji. Port ya Dar tumeshaambiwa mara alfu haina wala haitakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa za kisasa Bagamoyo ni perfect na itachochea sana ukuwaji wa kiuchumi nje ya Dar hasa Bagamoyo. JK alisema Bagamoyo, JPM akasema hapana sio kwa kuwa mradi mbaya ila masharti, Mama anasema mradi mzuri na maongezi yafanyike kwa hapo majority wins. JPM kishaondoka na hata yako Nyerere aliyakataa lakini yakaja kufanyika sio kwamba kila alichokataa JPM ndio sawa yale yalikuwa maono yake na zama zake zimeisha. Bagamoyo port naunga mkono 100% mwekezaji yoyote anafanya biashara haji kutoa sadaka. Mikopo mkipewa wa China ndugu zetu wakitaka biashara wa China wabaya.
Ni Bora wawekezaji wengne siyo mchina
 
Tuna bunge bovu lililopo madarakani kupitia tume ya uchaguzi isiyo huru kutokana na katiba mbovu .

Haya machozi tutalia sana , siku za mbele
 
Mkataba wa ununuzi wa ndege uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa waTz?

Mkataba wa bwawa la Nyerere uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa waTz?

Mkataba wa SGR (segments zote) uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa waTz?

Usiwe bendera fuata mkumbo. Hii nchi mikataba haijawahi kuwa na ahueni. Mikataba yote huwa tunapigwa mjomba. Ishu huwa ni nani ananufaika na kupigwa kwetu, nakuhakikishia hata mikataba enzi za Jiwe ilikuwa tunapigwa mno!

Tuungane kudai katiba itakayotaka mikataba yote kuwekwa hadharani kabla haijasainiwa

NB
Sina maslahi na bandari ya Bagamoyo wala siungi mkono mkataba unless uwekwe wazi
JUMAMOSI ya Novemba 15, 1884, Kansela wa Ujerumani, Otto von Bismarck, aliitisha mkutano mkubwa kwa ajili ya kuligawa Bara la Afrika.
Mkutano huo uliofahamika kama Berlin Conference, ulifanyika kwenye makazi yake huko Wilhelmstrasse, Berlin.
Mkutano huo ulilenga katika kuwaepusha wababe wa Magharibi kutumbukia vitani wakati wakigombania mali za Afrika.
Mataifa 14 yalihudhuria, wakiwemo Ujerumani wenyewe, Uingereza, Marekani (wakiwakilishwa na Henry Morton Stanley), Himaya ya Ottoman (Dola ya Mtukufu Sultan , Denmark, Ufaransa, Muungano wa Austria na Hungary, Urusi, Ureno, Hispania, Muungano wa Sweden na Norway, Ubelgiji, Italia na Uholanzi.
Mkutano huu ndio uliosababisha ukoloni barani Afrika, kwani uliazimia katika kuligawa bara hili miongoni mwa wababe waliohudhuria, kwa faida yao.
Baada ya mkutano huo, mataifa hayo yakatuma wawakilishi wao kuja Afrika kuchukua maeneo na mali.
Ujerumani ikamtuma kijana wa miaka 28, aliyeitwa Karl Peters, akiwa na vijana wenzake watatu; Dk. Karl Juhlke, Pfeil na August Otto.
Vijana hawa wakafunga safari hadi Afrika na kutia nanga Zanzibar na baadaye kuanza safari ya bara hadi walipofika Usagara ambako walikutana na Chief Mangungo katika Ikulu yake ya Msovero. Usagara kwa sasa ndio Kilosa.
Karl Peters akatumia ujanja, hila na ulaghai kuingia mkataba na kiongozi huyo wa kiafrika uliosababisha Ujerumani kuchukua eneo lake lote pamoja na watu wake.
Mkataba huo uliandikwa kijerumani na Chief Mangungo akamtumia mkalimani wake kutoka hapo hapo Msovero (Ramazan) ambaye na yeye wala hakuijua lugha hiyo.

Mkataba huo ulisomeka kama ifuatavyo.
“Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani, kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.
Dk. Karl Peters, kwa niaba ya jina la Umoja wa Ukoloni wa Ujermani anatangaza dhamira yake ya kuitwaa himaya yote ya Sultan Mangungo na haki zote kwa ajili ya Koloni la Ujerumani inayohusisha kila kona na amali za Mwenyi Sagara.”
Baada ya mkataba huu, Karl Peters akalichukua eneo lote lililokuwa chini ya Mangungo na kuliweka chini ya kampuni yake ya Deutsch-Ostafrika (German East Africa) ambayo ilikuwa ikimiliki eneo lote ambalo leo hii ni Tanzania Bara na Rwanda na Burundi.
Wakati machifu wengine, kama Mkwawa, walipigana na Ujerumani kukataa maeneo yao kuchukuliwa, Mangungo alilitoa eneo lake kirahisi kabisa.
Hayo yalitokea mwaka 1884. Hayo yalitokea karne ya 19. Hayo yalitokea kwa sababu Mangungo hakusoma, hivyo asingeweza kufua dafu mbele ya msomi, Daktari wa Falsafa, Karl Peters.
Lakini leo hii, zaidi ya miaka 130, katika karne ya 21, inashangaza kuona mikataba ya aina hiyo ikiendelea kusainiwa kinachoendelea leo ccm ni Ramazan sisi watanzania ni Chief Mangungo kilatunachoambiwa na Ramazan kwamba mikataba ni siri tunakubali wachina ni Dk. Karl Peters,yote tisa aliwaingiza chaka ni Ramazan alikula cha juu kisha akauza ramani,kama Chief Mangungo angejua kilichokuwemo kwenye Mkataba na kwakua alimuamini sana Ramazan angekinukisha ilibi awempole ,hata sisi pia tutakuja kuandikwa kwenye vitabu vya histori ya nchi hii kama watu wanjinga sana
 
Ni unafiki kuupigia kelele mradi wa bandari ya Bagamogo kama hauipigia kelele miradi yote ya mwenakuzimu, miradi yake yote kuanzia wa reli, bwawa la umeme, ndege na mingineyo yote ilajaa utapeli ndiyo maana haikuwa wazi.
Mwendakuzimu pamoja na kuwa katili muuaji pia alikuwa ni tapeli la kimataifa, alifanikiwa ku brainwash mazezeta wengi ambao sasa wanaupinga mradi wa bandari kwa kutumia references za tapeli mwendakuzimu wakati miradi yake hawakuwahi kuipigia kelele. Imagine miradi yote iliyokuwa ikifanywa Chato iliidhinishwa na nani, kila kitu ilikuwa ni one man show wakati wa awamu ya tano.
NB: Ni haki kujua yaliyomo ndani ya projects zote lakini bila ya katiba mpya hilo jambo haliwezekani kwani kwa katiba tuliyonayo rais ni Supreme leader na maono yake ndiyo muelekeo wa nchi.
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Miradi iliyopelekwa chato mliwahi kuhoji?team magu wengi ni vichaa sema hamjui kma nyie vichaa
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Tuliwacheka wenzetu sasa zamu yetu.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
When I heard this today I just felt a chill creeping my spine
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi. the

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.

Isije kuwa umelia machozi ya mamba. Inafahamika kuwa mamba nao hulia tena sana tu!
 
Sikuwahi kudhani Tanzania tuna uhaba wa Port mpk tuwauzie wachina Bagamoyo tumekarabati Bandari ya Dsm na Bandari zingine kwa gharama kubwa kabisa lakini leo tunakwenda kuziua bandari zote

Namuona Yuda ila sijui alimsaliti mwenzie kwa vipande 30 vya fedha au kwa ahadi ya kupewa kitu!!
Hivi mkuu unafahamu malengo hasa makubwa ya hiyo bandari?kwani mnalishwa matango poli tu na kuyamumunya !!bandari ya bagamoyo shughuri zake wala haitahusiana kabisa na bandari nyingine, kama mi meli mikubwa tena mikubwa kweli ya kuanzia mita 400 urefu, yanatoa bidhaa china kwa ajiri ya masoko ya afrika na sehemu nyingine, yanaileta hapo bagamoyo, kuanzia hapo ina bebwa na meli za kawaida na kuipeleka sehemu hizo, na bidhaa nyingine zitakuwa zinatengenezwa hapo.sasa kwa shughuri hizi hizi bnadari zetu nyingine zitakufa vipi?!!
 
Wewe ulikuwa segerea nn wkt wanasema vifungu vilivyomo kwenye mkataba? Kama huyo mama yenu ni mkweli na mwenye kutaka mema kwa watu wake apeleke Bungeni huo Mkataba ukachambuliwe
Sasa ilikuwaje ukaamini maneno ya magu bila mkataba kwenda Bungeni pia hata hujauona
 
YES MKUU...
Sikuwahi kudhani Tanzania tuna uhaba wa Port mpk tuwauzie wachina Bagamoyo tumekarabati Bandari ya Dsm na Bandari zingine kwa gharama kubwa kabisa lakini leo tunakwenda kuziua bandari zote

Namuona Yuda ila sijui alimsaliti mwenzie kwa vipande 30 vya fedha au kwa ahadi ya kupewa kitu!!
This is Afrika na Afrika haiwezi kuwa afrika kama viongozi wa kisiasa wa nchi zinazounda bara la afrika kufanya jambo linaloenda kumgarimu raia mzarendo wa nchi husika.

Mtwara Port.
Dar Port.
Tanga Port.
... although kuna Zanzibar free Port (japo siyo ya muungano) but ipo Tanzania.

Kwa ukiwapa bandari ya mtwara waindeleze kuna tutakosa nini?.
 
Kwa hiyo wewe tatizo lako ni jina bagamoyo?daaa!!pathetic kumbe ndio wale wale ambao wanapinga mambo bila kujua hasa hiyo bandari ni ya aina gani?hiyo bandari ya mtwara/dar kuna eneo hpo la kutosha aina hii ya bandari?!!
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Utamkumbuka wewe na mama yako
 
Sasa ilikuwaje ukaamini maneno ya magu bila mkataba kwenda Bungeni wakati hata hujauona
Alafu sikia usiwe mpuuzi hv unajua Tanzania tuna bandari ngapi? Unajua Tanzania tunapokea meli ngapi kwa Mwaka au mizigo tani ngapi? Ulishawaza au kusikia Tatizo la Bandari ni kukosa Gati (Sehemu za kupaki meli bandarini) Tatizo letu si Upungufu wa Bandari Tatizo letu ni efficient tu na swala hili linafanyiwa kazi Tumechimba berth zote 11 yani kwa mpigo bandari ya Dsm inaweza kupark meli 11 kwa wakati mmoja na zenye ukubwa mbali mbali why tusiboreshe miundombinu ya kuingia na kutoka bandarini kwa malori ,gari moshi kuliko kwenda na huu upuuzi wa POB?

Nisije kuwa naongea na jitu la Morogoro ambalo hata meli alijawahi kuiona.
 
Back
Top Bottom