Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Kwa uhalisia inatekelezeka, kwa kuwa wanafunzi hupanda pamoja na watu wazima, tena huwapisha watu wazima katika viti iwapo gari lina abiria wengi. Cha muhimu kufahamu ni kuwa, LATRA inapopanga nauli za daladala huzingatia kuwa kuna watu wazima na kuna wanafunzi watakaotumia huduma hiyo, hivyo watu wazima hulipa nauli kubwa ikiwa ni pamoja na kufidia nauli ndogo wanayolipa wanafunzi. Kwa mfano, kabla ya Novemba, 2023 nauli ya mtu mzima ilikuwa Sh. 500 hadi 1100 kulingana na urefu wa safari, mwezi Novemba 2023 ilipandishwa kuwa Sh. 600 hadi 1400. Hii ililenga kuwawezesha wasafirishaji kufanya biashara kwa faida. Changamoto ni baadhi ya makondakta na madereva wasio waaminifu hupenda kuvunja Sheria ili wajipatie kipato zaidi ya wanachostahili, abiria wakiwa wengi hudiriki hata kutangaza nauli za juu zaidi hata kwa watu wazima, hukatisha ruti na kulazimisha abiria kugeuka na basi. Makosa hayo hutendwa sambamba na makosa ya kuwakataa wanafunzi. Cha muhimu kukumbuka ni kuwa wanafunzi ni wenye uchumi wa chini na safari zao kwenda shuleni haziwaingizii vipato, hivyo jamii ina wajibu wa kuwapa ushirikiano ili watimize ndoto zao.
 
😹😹😹 umenichekesha mpk machozi yani nilikua na hekaheka jamani..!!
Na kwenye hizo hekaheka usisahau zile hekaheka za kusaka walimu wa tuition,mara mchikichini,mara pale Nakiete kwa nyuma mara Tambaza nyieeee ilikuwa ni oyaoya halafu jumapili mchana unazamia disco Billicanas kuna mashindano ya kushake mama anajua umeenda discussion aweeee....ila hapo wewe ulikuwa primaryπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Uwachomeshe gari yako? Nunua gari afu uwe unapakia wanafunzi, wee vipi? Una wapangia watu mali zao watumie vipi? Lol
Msafirishaji anapopewa leseni na LATRA hupewa masharti ya leseni, hii ni pamoja na kutobagua abiria. Serkali hutekeleza jukumu la kuwalinda watoa huduma, hii ndiyo sababu wasafirishaji wamepandishiwa nauli za watu wazima kutoka sh. 500 hadi sh. 600 - 1400 ili wasifanye kazi kwa hasara.
 
Je hamfikirii kununua mabuss ya wanafunzi Kama wanavyofanya wenzenu Kenya ?
 

Nadhani hapo awali nimesema kuwa, huu uzi unasomwa hata na taasisi husika moja kwa moja. Hata kama hujaona wakijibu hapa, wanasoma.

Nilichojaribu kuweka sawa ni kuwa, mimi mwananchi akinitag, nitajibu na kumuongoza wapi apate majibu ya kina zaidi. Mfano, wengi wananiTag kuhusu ukatili mbalimbali wa kijinsia, najibu na kuwaongoza au kuwakumbusha kuwa, wafike Dawati la jinsia polisi, wapate PF3 na RB, nawapa na namba ya IGP aliyotangaza kuwa ni 0699998899 kisha wanaendelea mbele kwenye hatua. Wengine wanakwama tena wanarudi, nawapokea nawapa elimu kadri niwezavyo wanaenda tena wanabaini kumbe ilikuwa uelewa tu kuhusu utaratibu.

Hivyo, katika spirit hiyo hiyo, sasa nimepokea tag ya kuhusu haya ya LATRA... nikafanya kama ninavyofanya siku zote. Hivyo, tuendelee kushirikiana, uzi huu unasomwa na LATRA, msiwe na shaka, kama kufika sehemu sahihi, maoni yamefikaβœ…
 
Hapo kwenye bango kuna namba za LATRA, hebu katoe maoni tafadhali. Uwe na jioni njema ya Baraka βœπŸ»πŸ™πŸ½
Sasa Mheshimiwa, with due respect, kila mtu hapa unamwambia apige namba atoe maoni kwenye hiyo namba, sasa nini maana ya wewe kuanzisha huu mjadala na wakati unajua namba ipo public kila mtu anayo???

Ni vipi unakwepa majukumu yako ya kijamii hata kujibu tu kisiasa kwamba "nitafatilia" pia hutaki, na unajua ninyi viongozi wetu mmezoea kutudanganya watanzania miaka yote tangu uhuru na hakuna wa kuwawajibisha.

Anyway mimi naomba nikupe ushauri, you opt to digest it, take or leave it, but it's workable... Tangu nasoma shule za katikati ya jiji miaka ya tisini, changamoto ya usafiri kwa wanafunzi imekuwepo, ilikuwepo ipo na itaendelea kuwepo. Serikali haijawahi na haioneshi nia ya kushughulikia hili tatizo zaidi ya siasa tu na ahadi miaka yote (unless kuna plans ambazo bado hamjaziweka wazi kwetu) zaidi watoto wanazidi kuteseka kila uchwao. Inauma sana unapoona awamu zote za uongozi hakuna aliyetatua hili swala.

1. Kama serikali imeweza kujenga SGR na BRT na NYERERE DAM na other Mega projects, inashindwaje kuanzisha Shirika la usafiri wa wanafunzi Tanzania liwe na ma'bus ya kutosha kila kona?? Shirika hilo liendeshwe kwa ruzuku ya serikali na wapakie wanafunzi tu na watu wenye ulemavu tu. Na muda wa kazi (public buses) iwe ni asubuhi kuanzia saa moja mpaka saa tatu na jioni kuanzia saa tisa mpaka saa 12. Kama Chama Tawala kina ma'bus tena ya kifahari, ni maajabu kukosa ya wanafunzi.

2. Kwa kua serikali imejitahidi kwa asilimia kubwa kusogeza huduma za elimu karibu kabisa na makazi ya wahitaji (kata) basi Wizara yako na Wizara ya elimu na zingine zote husika, zishiriki kuhamasisha wazazi kupeleka watoto wao katika shule zilizo karibu na mazingira yaliyopo, umbali ambao ni walking distance kwa mwanafunzi. Na kama imetokea wizara ya elimu imempangia shule mtoto iliyo mbali na makazi yake labda kwa sababu ya kuhama makazi au mfumo tu, basi utaratibu wa mtoto kuhamishwa kwenda shule ya jirani usigubikwe na urasimu iwe ni rahisi.

3. Magari yote ya serikali na mashirika yake ambayo yanabeba wafanyakazi wao yaamriwe mara moja na wizara ya uchukuzi kuanzia hivi sasa yasimame kila kituo kuchukua wanafunzi. Hayo sio ma'bus binafsi ni ya watanzania wote wakiwemo wanafunzi hivyo hayapaswi kua na ubaguzi. Hii iwe amri na sio ombi.

4. Serikali iwape ruzuku wamiliki wa Daladala kila mwezi au iwaondolee kodi kabisa kwenye uendeshaji kwa minajili ya kubeba wanafunzi bila idadi. Kinyume na hapo ni uonevu kwa wenye magari kwa kigezo cha leseni yako inasemaje. Kumbuka leseni haibadiliki ili hali ya uchumi inabadilika. Leseni iliyochukuliwa miaka 20 nyuma ina utaratibu ule ule wakati bei ya mafuta imeshapanda.

5. Kwa leo naishia hapa wadau wataongeza..
 
Mkuu unakwepa hoja kuu kwenye reply zangu

Hoja kuu ni kuwa hayo maoni yapo yalishatolewa na yanaendelea kutolewa na wahusika wanayasoma ila hawayafanyii kazi miaka nenda rudi hadi leo tatizo lipo

Hivyo tunakuomba wewe kama waziri wetu na muwakilishi wetu ukiwa katika vikao vya bunge na mikutano na raisi utufikishie hoja zetu kuwa;

1. Serikali inunue magari kwa ajili ya wanafunzi kama wafanyavyo sekta binafsi

2. Magari ya serikali kama vile mwendokasi na magari ya jeshi yawe yanabeba wanafunzi asubui na jioni

3. Wamiliki wa daladala wapewe ruzuku ili waweze kubeba watoto wa shule bila kuathirika na kodi na matozo yanayowabana

4. Hizo sheria za kubeba wanafunzi kwa sh 200 kwa ulazima kana kwamba wazazi wamechangia kwenye ununuzi ziondolewe

Ukifikisha hayo kwenye vikao vyenu vya bunge na vikao vya mawaziri utakuwa umelisaidia sana hili kundi la watoto wanaoteseka na usafiri kuliko kushurutisha sheria ambazo hazitekelezeki
 

Kumbe awali mkishatoa, basi nitauliza walifikia wapi huenda mrejesho ulishatolewa ila haukuwafikia wengi. Ahsante Sana
 
Maana ya kuanzisha mjadala ilikuwa ni jamii ijue kuwa, badala ya kuniTag mimi kwenye hoja za eneo hili, waijue namba ya taasisi yenye dhamana watag moja kwa moja au wapige. Wangeijua hiyo namba hata wasingeniTag. Nikaona nitangaze na namba kabisa. Piga makofi sasa pongeza na namba imejulikanaπŸ€—
 
Kumbe awali mkishatoa, basi nitauliza walifikia wapi huenda mrejesho ulishatolewa ila haukuwafikia wengi. Ahsante Sana
Ahsante Dr, natumai maombi manne ya reply yangu umelipata na utalifanyia kazi

Nakutakia uwasilishaji mwema wa hoja za wananchi kwenye vikao vyako
 
Reactions: Lax
Hujambo? Sasa Kila nukta ujibu? Si utazimia kwa uchovu.... Maswali na majibu mengine ni cross multiplication, unakumbuka hizi hesabu lakini 😁
Mkuu maswali yanaobana serikali unayaruka kwa kuleta jokes🀣 anyway tunakuelewa na kuipongeza serikali ya awamu .. inayoongozwa na ..

Utani pembeni, endelea hivi mkuu mawaziri wengine wakifata hivi itakua poa
 
Ahsante Dr, natumai maombi manne ya reply yangu umelipata na utalifanyia kazi

Nakutakia uwasilishaji mwema wa hoja za wananchi kwenye vikao vyako
Nakushukuru Sana wewe na wote mliochangia mjadala na kuwezesha nami kupata mwanga mkubwa, ningeishia kusema nimepokea huenda maoni mengi yangebaki mioyoni kwa watu. Hivyo, mijadala kama hii husaidia pande zote kufahamu mafanikio, changamoto na mapendekezo. Sasa, niwaombe kwenye kipindi hiki uchambuzi wa maoni ukifanyika, tutekeleze miongozo ya kisheria watoto ni wetu wote jamani. Mungu awabariki Sana πŸ™πŸ½ πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
 
Ulishawahi kuwa kondakta mdau??
Kama hukuwahi pitia ukondakta usilete ujuaji kwenye gari za watu
 
Mkuu maswali yanaobana serikali unayaruka kwa kuleta jokes🀣 anyway tunakuelewa na kuipongeza serikali ya awamu .. inayoongozwa na ..

Utani pembeni, endelea hivi mkuu mawaziri wengine wakifata hivi itakua poa
Jamani unataka nichangie mjadala nikiwa na hasira Kali hivi 😬😬😬, hee tutafika kweli 🀣, huku wewe hapo unaachilia spana πŸ”§ konki plus, si tutapata stroke 🀣
Naamini mijadala yetu inaweza kuwa rafiki na ujumbe ukaenda vilevile maana kikubwa ni Nia zetu wote mioyoni mwetu kwenye kutimiza wajibu wa Maendeleo na ustawi wa jamii πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
 
Reactions: Lax
Kwa nauli ya miambili ni hasara tu mdau kununua gari kwa ajili yao

Iwekwe tu idadi maalumu ya kuwapakia
 
Oooh kumbe.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…