Madaktari wa Bongo washindwa kutema yai

Sio poa.

Madaktari walitakiwa kuongea Kingereza muda wote wa kaziπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Ni kweli kabisa kiongozi, wengi hawajui tatizo liko wapi na hatutaki kujifunza kwa wengine kama china na india. Tumekalia ulimbukeni wa kiingereza bila mafanikio. Ni muda wa kutumia kiswahili katika kupata maarifa kiingereza iwe kama somo la lugha tu.

Hii itasaidia kutuhamasisha katika kujitafutia maarifa na kufanya tafiti wenyewe na sio kuwa tegemezi kwa nchi za magharibi.
 
Mkuu kwamba MD walioko vituoni wanashindwa kuwasiliana na hao wanafunzi kwa kigezo cha lugha ya kiingereza? hii haiwezi kuwa kweli maana masomo na hata mawasiliano ya kidaktari ni kwa lugha ya kiingereza, labda utuambie muhimbili wameanza kufundisha degree ya udaktari kwa lugha ya kiswahili.
 
Hata mimi nilibisha kama wewe Lakin tulikuja kuupata ukweli English haipandi Kwa ma daktari wetu
 
Hata mimi nilibisha kama wewe Lakin tulikuja kuupata ukweli English haipandi Kwa ma daktari wetu
Lugha ya mawasilino ya kidaktari siyo sawa na hii inayotumiwa kwenye mazungumzo ya kawaida mitaani, yenyewe inakuwa imejikita zaidi kwenye mambo ya kiganga na hivyo ni rahisi madaktari wenyewe kwa wenyewe kuwasiliana. Miaka mitano usome udaktari kwa kiingereza ushindwe kuwasiliana na daktari mwenzako kwa lugha hiyo hiyo ni jambo lisiloingia akilini. Inawezekana hao siyo madaktari bali ni vishoka...​
 
Mkuu kila course chuo inafundishwa kiingereza.
Hao wasudani wasitujazie inzi hapa na kama vipi watupishe tu na kiinglishi chao.
 
Mkuu nchi imegeuzwa kuwa ni wachuuzi watupu viwanda ni vichache,
Mchuchuma wanataka kuumpa mchina achimbe na kusepa badala ya kuichakata hapahapa Bongo,
Bukoba wamempa UK achimbe Tu πŸ˜‚ bila kujenga kiwanda cha battery, ili vijana wapate ajira.
Gairo nako kapewa Australia nako ni kuchimba Tu hakuna kungeneza final product ya kuuza.

Ni kuchimba Tu πŸ˜‚ na kubaki na mashimo
 
Kujifunza kiswahili for that period of time ya practical ni uongo, is why english ipo, even madkatari wetu entire syllabus ni english, sasa kama wamefuzu na hawajui, i doupt kiwango cha elimu yetu
Mwenye shida ndio unajifunza kama Umekuja Bongo kwa Waswahili jifunze lugha...; Unadhani ukienda Russia huko hautajifunza lugha yao ?

Kujua na kuongea lugha au confidence ya kuongea lugha nyingine ni vitu viwili tofauti kabisa; In short Doctors prowess is not measured by mastering a certain lingo...; kuelewa syllabus na masomo huitaji kuwa mahiri wa language; english ya kuunga unga haikufanyi hushindwe kuelewa human anatomy
 
Kiswahili hakitoshi, kina mapungufu mengi, hata ukisema tukitumie kufundishia bado kuna mengi sana ya kukopa.
 
Hata mimi nilibisha kama wewe Lakin tulikuja kuupata ukweli English haipandi Kwa ma daktari wetu
Sio madaktari tu mkuu, Wahitimu wa vyuo vikuu wengi lugha ya kingereza ni tatizo, Tafuta hata mwalimu wa English wa Sekondary uone.

Kifupi Kingereza sio lugha yetu wakuu ili tuijue vizuri inatakiwa nguvu ya ziada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…