Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 4,240
- 10,561
- Thread starter
- #321
Kipindi cha el ninyo miaka ya 2000 tulikua na mision fulani singida huko.si tukachomoka Dar hadi Dom,siku ya pili Bus hamna daraja limekatika pale bahi.
Akatokea jamaa na londo lake anawai shybush hakutaka hata nauli.
Tukaunga nae border kwamtoro.
ikawa twenzetu,humo njiani mi mvua na mimaji njia nzima,mpk tukafika kati pale kwa wasandawi daraja limezolewa na mafuriko tukasanda.
Wakatokea wanajeshi nao wanakula border.
Tukaungana kuingia msituni kata miti jaza pale mpk pakajaa.
Wao wakapita na sisi tukapita.
Hatukufika mbali gari ikatereza ikakwama,tukawa tuko pale hadi giza linaingia.
Hawa wahadzabe sijui hata walitoka wapi.
Wakaja km 12 hivi.
Wanabeba gari dere anagonga 4wheel linasogea
Wanaacha wanasema ongezeni hela.
Walikula km buku 20.
Tulitoka kesho yake,
Sasa pale tulimpata mwalimu mmoja,tukamwambia tuna njaa sana, akasema twendeni home kwangu juu kule.
Dah tulikua katikati ya pori giza haswa.
Ikabidi mimi na libwege limoja hivi tulikua nalo liko benki lina kitambi hivi,nia ni kwamba achinjwe kuku na ugali turudi nao.
Kweli tumeenda likaangushwa bonge la jogoo,
Tukala tukashiba.
Mchuzi ukabaki na nyama nyingi tu.Ugali kibao.
Namwambia jamaa tushuke chini kule kupeleka msosi kwa wenzetu.
Duh lile pimbi ndo kwanza likaomba mkeka lilale lishashiba.
Dah mi nilikataa aisee nikikumbuka wale kwenye gari hawajala toka juzi tumekwama pale.
Nikaona isiwe tabu,funga ugali,funga kuku napeleka.
Tulikua 6.
Siku ile ni Mungu tu,Simba na leopard naamini bin adam usipowachokoza hawakugusi.
Nilifika salama ila nilipishana nao sana tu.
Walikua wananiangalia tu.
Lile pimbi silisahau ,alikua anaenda Bukoba huko.
Anyway ni story tu hii.
Mchuzi ukabaki na nyama nyingi tu.Ugali kibao.
Namwambia jamaa tushuke chini kule kupeleka msosi kwa wenzetu.
Duh lile pimbi ndo kwanza likaomba mkeka lilale lishashiba
😋😋😋, Hii story ni unyama sana, mkuu jaribu kuandaa yote,