Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Kipindi cha el ninyo miaka ya 2000 tulikua na mision fulani singida huko.si tukachomoka Dar hadi Dom,siku ya pili Bus hamna daraja limekatika pale bahi.
Akatokea jamaa na londo lake anawai shybush hakutaka hata nauli.
Tukaunga nae border kwamtoro.
ikawa twenzetu,humo njiani mi mvua na mimaji njia nzima,mpk tukafika kati pale kwa wasandawi daraja limezolewa na mafuriko tukasanda.
Wakatokea wanajeshi nao wanakula border.
Tukaungana kuingia msituni kata miti jaza pale mpk pakajaa.
Wao wakapita na sisi tukapita.
Hatukufika mbali gari ikatereza ikakwama,tukawa tuko pale hadi giza linaingia.
Hawa wahadzabe sijui hata walitoka wapi.
Wakaja km 12 hivi.
Wanabeba gari dere anagonga 4wheel linasogea
Wanaacha wanasema ongezeni hela.
Walikula km buku 20.
Tulitoka kesho yake,
Sasa pale tulimpata mwalimu mmoja,tukamwambia tuna njaa sana, akasema twendeni home kwangu juu kule.
Dah tulikua katikati ya pori giza haswa.
Ikabidi mimi na libwege limoja hivi tulikua nalo liko benki lina kitambi hivi,nia ni kwamba achinjwe kuku na ugali turudi nao.
Kweli tumeenda likaangushwa bonge la jogoo,
Tukala tukashiba.
Mchuzi ukabaki na nyama nyingi tu.Ugali kibao.
Namwambia jamaa tushuke chini kule kupeleka msosi kwa wenzetu.
Duh lile pimbi ndo kwanza likaomba mkeka lilale lishashiba.
Dah mi nilikataa aisee nikikumbuka wale kwenye gari hawajala toka juzi tumekwama pale.
Nikaona isiwe tabu,funga ugali,funga kuku napeleka.
Tulikua 6.
Siku ile ni Mungu tu,Simba na leopard naamini bin adam usipowachokoza hawakugusi.
Nilifika salama ila nilipishana nao sana tu.
Walikua wananiangalia tu.
Lile pimbi silisahau ,alikua anaenda Bukoba huko.
Anyway ni story tu hii.
Mchuzi ukabaki na nyama nyingi tu.Ugali kibao.

Namwambia jamaa tushuke chini kule kupeleka msosi kwa wenzetu.

Duh lile pimbi ndo kwanza likaomba mkeka lilale lishashiba

😋😋😋, Hii story ni unyama sana, mkuu jaribu kuandaa yote,
 
Mbona sijaona Dar mtwara? Vyakula havitupwi na havina ladha mpk unataman kulia
 
Mbona sijaona Dar mtwara? Vyakula havitupwi na havina ladha mpk unataman kulia
Mkuu hiyo ilikuwa ni mfano tu, Maana hii kero ipo Tanzania yote, Mamlaka imevaa miwani ya mbao.
 
Hii bwana natamani sio Siri
Hivi timetable Yao ikoje?
Na gharama yake sh ngapi 1st class?
J4 sa kumi na ijumaa mida hiyo first 50 second 45 haifiki.
First mtu 2 tu,second km una watoto familia ni vitanda vi4.
Huna utakutana na majirani humo ndani mnagawana vitanda.
Hiyo safari ni bonge la adventure,unalala unapotaka,kinywaji mda wowote,chakula kipo ukitaka unawapitia 3rd class kusalimia utawakuta mle km magunia ya viazi wanaenda kapiri mposhi.
Njiani hapo ukitoka mlimba mbele mlimani udzungwa pale ndio utajua kwamba kuna sehemu tuko vizuri.
Treni inaenda speed ndogo sana kupanda juu kule,sasa ukichungulia chini unaweza kuruka kwa woga.
Ni midaraja mikubwa na matreni yaliyodondoka ya mizigo yapo.
Cha ajabu mbele kidogo kuna wanakijiji wanakaa milimani,utaona vijumba vyao kule juu baada ya hiyo shughuli baas treni utaipenda.
Inakamata mteremko na tambarare.
Hapo utaskia honi tu.
Hiyo view sasa huku nje.
Jaribu one day utashukuru.
 
Tena hizo sehemu za vyakula zinakuwa mbali na mji hakuna alternatives.

Nakumbuka wakati natoka Morogoro kwenda Mwanza tukikuwa tukishushwa Singida, chakula bei af sina imani nacho. Awamu zilizofuata nilikuwa nachukua zangu broiler na chips kavu Morogoro kwa 3000 take away, ilikuwa wakishuka kwenda kula mimi natoa take away yangu wakirudi wanakuta nakula chips kuku taratibuu. Nasubiri wanaouza soda nachukua nashushia
Singida Stendi ya zamani kuna misosi balaa pale,walipohamishia kule sabasaba ndio kuna ujinga mwingi.
Ila pale town ilikua nyama choma nyingi sana,mikuku ya kienyeji bei bwelele,vbanda mama ntilie kibao na wanapika km wamelogwa.
Mi nilikua muuza BigG na karanga pale stend.
Paketi zangu 2 tu nna faida sh 800😆😅😅😅.
Narudisha hela ya Manji Dewji pale ili kesho anipe mzigo mwingine.
Na hapo nakua nishauza kuku kienyeji na mayai yao mapema tu.
Ila maisha haya,tumetoka mbali sana
 
Hizi ni story za vijiweni. Hivi wewe unadhani kuna mtu mwenye uwezo wa kukamata ndege wengi mpaka afikie hatua ya kuuza nyama yao? Au humjui tai wewe? Wanapatikana kwa wingi kiasi hicho?
Kabisa mkuu naonaga ni safe kula nyama ya kuku kuliko hizi zingine kama ngombe n.k maana kuku anajulikana ila hzo nyama zingine unaweza lishwa nyama ya mbwa au paka
 
Kabisa mkuu naonaga ni safe kula nyama ya kuku kuliko hizi zingine kama ngombe n.k maana kuku anajulikana ila hzo nyama zingine unaweza lishwa nyama ya mbwa au paka
Hapo usichoelewa nini?hao alikua anauza huyo jamaa ni mipaja na vidari vya ndege tai.
Anakwambia ni kuku kienyeji.
Mtu una njaa utauliza tena? unakula tu.
 
Sasa basi zima kila mtu abebe hotpot, Inakuja kweli hiyo?
Mshukuru tu kwa mchango,hata yeye ni mwenzetu.Mapendekezo yake yawezekana kawaza muda mrefu sana,hadi kufikia kuandika hivyo.Yaani eti.... aisee.
 
Sijui wanatuchukuliaje wasafiri sababu hatuna option nyingine🤔 ila kuna siku nilienda Moshi na Kilimajaro Express sijui ni hotel yao ile atleast wanajitahidi chips safii nikashangaa maana nishazoea Mbeya kwetu mwendo mdundo chips zimepoaa 😀(sijui ni ulafi ila lazima nile njiani)
Duuuh! body liko well structured kweli.... au TAMBI lipo?
 
Mshukuru tu kwa mchango,hata yeye ni mwenzetu.Mapendekezo yake yawezekana kawaza muda mrefu sana,hadi kufikia kuandika hivyo.Yaani eti.... aisee.
Naujua hilo mkuu, huu ni mjadala tuhh, hakuna ugomvi wowote ule, 🙏🙏,
 
Iambie serikali ndio ijenge hizo sehemu za kula watu masikini inawezekana kama inaweza Jenga stend haishindwi.
Hizo hotel wamewekeza pesa nyingi na kila dereva na makonda wanakula Bure.
Cha msingi beba chakula chako.
Njiani sio sehemu za kula kula,kale kwako.
 
Back
Top Bottom