Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Wafanyakazi hewa kawamaliza
Cheti feki kafagia
Hapa mzee alichemka, kwani zoezi la vyeti feki lilijaa ulaghai na upendeleo wa hali ya juu. Kuna Taasisi hazikuguswa na kuna kanda flani hawakuguswa.

Hii inanikumbusha ajira 13000 za walimu, ni walimu wa kanda ya Ziwa, Pwani na Mkoa wa Lindi hasa Ruangwa ndio walifanikiwa wengi wao kuajiriwa.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kufufua reli ya kutoka Dar es salaam-Tanga-Kilimanjaro-Arusha

Upanuzi wa Bandari ya Dar, Tanga, Mtwara

Ujenzi wa gati Mafia

Mradi wa rada airport ya Dar, Mwanza, Songwe,....

Elimu bila ada

Vituo vya afya vya kila halmashauri

Hospitali za wilaya, mikoa, na kanda

Barabara za mitaa Dar na katika majiji mengine, na miji

Ujenzi wa kota za gorofa Magomeni

Ujenzi wa masoko makubwa (Soko la Job Ndugai Dodoma, Morogoro, soko la Kisutu, soko la Magomeni, soko la Mbagala, na miko mengine)

Ujenzi wa standi za kisasa (Mbezi, Dodoma, Morogoro, Korogwe, na nk.)

Ujenzi wa majengo ya makao makuu ya Halmashauri

Daraja la mto Kilombero, na mengine mengi

Madaraja ya waenda kwa miguu (Dar na Mwanza)

Ukarabati shule kongwe na vyuo (Pugu, Galanos, na nk.)
Stendi ya Morogoro umeongeza chumvi.
 
Kwakweli vituo vya afya kila kata ni msingi mzuri wa community health. Vikipata maji ya uhakika na umeme, mafridge ya kuhifadhia dawa na wataalamu wenye sifa. Mzigo mkubwa kwenye hospitali za rufaa utapungua.
RIP Magufuli.
Sky Eclat leo nikwambie tu ukweli. Nakupenda sana, najua wewe ni mdada. Jua tu nakupenda. Huwa najiskia vibaya sana ukimpondea magufuli. Kwa sababu the man is my hero.
 
alafu unaweza kuta hujui umesimliwa tu,nawe unashupaza shingo kuwa ndivo,jamaa kafanya mpeni stahili yake
Kila mwaka nakuja likizo bongo na najua kabisa kwamba sumitomo company na TANROADS walishamaliza kila kitu kabla hata uchaguzi wa 2015. Kilichobaki ilikuwa ni kuangalia watu wakisimamisha kitu baas.
 
1. Mabweni ya Chuo Kikuu Cha DAR ES SALAAM
2. Tazara flyover
3. Ubungo flyover
4. Mv. Hapa Kazi TU
5. Mv Mbeya
6. Daraja la Mkupita
Jamani leo ikiwa ni siku ya mazishi yake haki yake tumpeni kila mradi alioukamilisha tuutaje
Mradi wa kuuwa vyama vya upizani (lengo ilikua ukamilike kabla ya 2020) umefikia hatua gani?
 
Back
Top Bottom