Nadhani anafanya yote hayo kwa mikopo itakayotupa tabu baadae na dhulma ya promotion za wafanyakazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani anafanya yote hayo kwa mikopo itakayotupa tabu baadae na dhulma ya promotion za wafanyakazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ikiwa ni mikopo ambayo tunaona kwa macho yetu kinachofanyika ni vema na haki kabisa ! Maana zilipazwa sauti enzi za tawala zilizopita kuwa mikopo iliingia mifukoni mwa wajanja wachache na hata mingine kurudi kinyemela kwa wakopeshaji ! Kwa sasa no way ! Go! go ! go ! Genius JPM !
 
Sasa vilaza ndo wanalalamika wanaona maajabu. Jamani ni kawaida tu msishangae tunachapa kazi. Na zote zitakamilika kwa 100% tumpe nafasi rais wetu achape kazi vilaza acheni kulalamika.
Hivi bado hujagundua tu ni jinsi gani ulivyo kilaza?! Wenzake walitumia vyanzo vya ndani kujenga UDOM ambayo imeongeza sana idadi ya Watanzania wanaojiunga vyuo vikuu, Magu anatumia vyanzo vya ndani kununua ndege; biashara ya hovyo kabisa! Ikiwa mashirika yenye routes kibao ndani na nje ya nchi zao yanaendesha biashara kwa hasara, huyo Magu ana nini cha ziada cha kuifanya ATCL iwe inafanya biashara kwa faida kama lengo si kuwapiumbaza vilaza aina yako muone anavyonunua ndege?! Kama biashara inafanya vizuri, mbona waligoma kukaguliwa na CAG?!

Angalia unavyothibitisha ukilaza wako!!! Kama SGR inajengwa kwa pesa za ndani, mbona deni ka taifa linaendelea kukua mwaka hadi mwaka?! Kama pesa zinazotumika ni za ndani, deni linakua kutokana na nini?! Hilo la barabara; si huyo huyo Magufuli enzi akiwa waziri wa ujenzi alikuwa anatamba kwamba wamejenga barabara 11,000 km kwa pesa za ndani?! Sasa kama alichokuwa anasema na JK ni kweli, nini hapo kipya?! Isitoshe barabara nyingi JPM kaingia madarakani kakuta zinajengwa, na nyingi zikiwa zimeisha!

Ujenzi wa viwanda nchi nzima ni ujinga unaoweza kuamini na vilaza tu! Nina uhakika ukichukua viwanda vilivyoanza kujengwa enzi za Magufuli, unaweza kuchanganya vyote na bado thamani yake isifikie thamani ya kiwanda kimoja tu cha Dangote! Sasa kutamba eti anajenga viwanda nchi nzima kama si uzwazwa tuite nini?! Btw, hivi zaidi ya porojo za "Tanzania ya Viwanda" nikikuuliza utaje strategy za serikali kuhakikisha tunakuwa na Tanzania ya Viwanda unaweza kutaja mikakati ya serikali?! Hivi unaamini kabisa kuna mtu hakuwa na ndoto ya kuanzisha kiwanda lakini akaja kuwa inspired na Magu Administration kuanzisha kiwanda? Magu yule yule ambae amekaza kuua sekta binafsi?!

Halafu angalia ulivyo lofa! Eti ujenzi wa Vituo vya Afya umekamilika nchi mzima!! July mwaka jana PM anasema serikali imejenga vituo vya afya (ingawaje ki ukweli vingi ni zahanati tu) 108!

Sasa ikiwa ndani ya miaka 2 unusu serikali inadai imejenga vituo vya Afya 108, kwa akili yako unaamini ndani ya mwaka mmoja unusu serikali hiyo hiyo inaweza kujenga vituo vya afya kwenye kata zote zilizobaki! Au hujui Tanzania kuna kata ngapi?! Hebu jialimishe hapa:-
Kata kwa nchi nzima ziliongezwa kutoka 2,802 mwaka 2009 hadi 3,337, vijiji vikaongezeka kutoka 11,795 hadi 12,423 na mitaa ilitoka 2,995 hadi 3,741 huku vitongoji vikiongezeka kutoka 60,359 hadi 64,616.
Kwavile umeonesha wazi ni kilaza, wacha niishie hapa manake am sure hauna ubavu wa kushika yote nitakayoandika kwa maeneo mengine niliyoacha kuyaelezea!!
 
Nimeishia viwanda 4000!! labda kama salon za nywele nazo ni kiwanda hapo sawa.
Kati ya hivyo ni vile 3000 vya Mwijage vya cherehani nnenne ingawa navyo havijulikani viko wapi kama ilivyo miradi mingi ya Awamu hii inayoimbwa kila siku na kila mpambe. Mwaka huu peke yake miradi mingi has a ya ujenzi iliyokuwa izinduliwe na Mwenge haikuzinduliwa ilikuwa chini ya kiwango.
Nimeishia viwanda 4000!! labda kama salon za nywele nazo ni kiwanda hapo sawa.
 
NI malofa tu ndio wanaamini hivi sasa huko serikalini watu hawaibi!! Kila kitu kinafanywa siri, CAG kataka kuikagua ATCL, kwa hali ya ajabu kabisa, hakupata ruhusu ya kufanya hivyo!!! Btw, hivi huyu Magufuli huo Umalaika ameanza nao lini?! Si ni Magufuli huyu huyu ndie wizara yake ilinunua kivuko cha hovyo kwa mabilioni ya pesa na kwa hofu ya kusakamwa, akaamua kukipeleka Navy ili watu wasihoji!!

Magufuli mwizi tu kama majizi wengine wa CCM!
 
Kama ni hivyo mbn waliiba katika uchaguzi serikali ya mtaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeishia viwanda 4000!! labda kama salon za nywele nazo ni kiwanda hapo sawa.
Rais wangu WA majukwaani saizi ni muda wa kitembea na Pacha lako ili kupunguza stress za watu Tutahakikisha tunamjazia strategies za kuboresha maisha ya watanzania...





Saizi Maprinter tayari ndege ikitua Tu na dhana ya ujamaa itatumika ni Raha tupu kuanzia na serikali ya VIWANDA kufufua vyote Kwa fedha zetu wenyewe wenye viwanda vya stress watatujoin wenyewe..





Saizi ni kuchota hela (BOT/HAZINA) kila MTU alipwe laki 500000 Kwa mwezi fungua viwanda vyote vilivyokufa walipe Kodi na gawio KAZI imeisha pokea mishahara usifanye KAZI umetaka mwenyewe..



 
Shida ni mtoa Mada hawezi tena kujitokeza kujibu hoja za wachangiaji bali atoa like kwa wenzake wanaotoa matusi then wanafurahia. Unaposema viwanda 4000 bila kuonesha ni wapo na wapi unatukosea sana sisi tunaosubiri hizo viwanda vijengwe ili tupatepo ajira.
 
Hii , ndiyo Tanzania ngumu sana kukubalina.


Wapinzani walipodai nchi inaibiwa yafanyike mabadiliko waliitwa WAONGO.


Mabadiliko ya " kweli" yamefanyika SERIKALI inaita kuwa IMEBUNI yenyewe hakuna aliyeistua. Mkuu anatumia serikali YANGU.

UPINZANI kwa kuwa hauthaminiki kwa kuamini kelele zao ndiyo zilizoiamusha CCM ikateua mtu MAKINI anayeotendea haki nafasi yake.

Imebidi wakejeli kama wanavyokejeliwa.

Tukiijua kweli, nayo kweli itatuweka HURU.


HEKO UPINZANI, HEKO MAGHUFULI
 
Tanzania huenda tunaongoza kwa ujinga Africa. Hili deni la Taifa linalokua kwa kasi amekopa kwa bibi zenu. Mnashindwa hata iujua source ya fedha zinazohudumia huo miradi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani ukikopa mbwa ndo zitalipa au wewe mwenyewe uliekopa? Na hizo pesa utakazolipa sio zako au huelewi unachoongea? Kukipa ni kulahisisha kazi yako kisha utalipa pesa yako unayozalisha wewe mwenyewe, cha kusikitisha utakuta wewe nae umeenda shule kidha unasema hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…