Sasa vilaza ndo wanalalamika wanaona maajabu. Jamani ni kawaida tu msishangae tunachapa kazi. Na zote zitakamilika kwa 100% tumpe nafasi rais wetu achape kazi vilaza acheni kulalamika.
Hivi bado hujagundua tu ni jinsi gani ulivyo kilaza?! Wenzake walitumia vyanzo vya ndani kujenga UDOM ambayo imeongeza sana idadi ya Watanzania wanaojiunga vyuo vikuu, Magu anatumia vyanzo vya ndani kununua ndege; biashara ya hovyo kabisa! Ikiwa mashirika yenye routes kibao ndani na nje ya nchi zao yanaendesha biashara kwa hasara, huyo Magu ana nini cha ziada cha kuifanya ATCL iwe inafanya biashara kwa faida kama lengo si kuwapiumbaza vilaza aina yako muone anavyonunua ndege?! Kama biashara inafanya vizuri, mbona waligoma kukaguliwa na CAG?!
Angalia unavyothibitisha ukilaza wako!!! Kama SGR inajengwa kwa pesa za ndani, mbona deni ka taifa linaendelea kukua mwaka hadi mwaka?! Kama pesa zinazotumika ni za ndani, deni linakua kutokana na nini?! Hilo la barabara; si huyo huyo Magufuli enzi akiwa waziri wa ujenzi alikuwa anatamba kwamba wamejenga barabara 11,000 km kwa pesa za ndani?! Sasa kama alichokuwa anasema na JK ni kweli, nini hapo kipya?! Isitoshe barabara nyingi JPM kaingia madarakani kakuta zinajengwa, na nyingi zikiwa zimeisha!
Ujenzi wa viwanda nchi nzima ni ujinga unaoweza kuamini na vilaza tu! Nina uhakika ukichukua viwanda vilivyoanza kujengwa enzi za Magufuli, unaweza kuchanganya vyote na bado thamani yake isifikie thamani ya kiwanda kimoja tu cha Dangote! Sasa kutamba eti anajenga viwanda nchi nzima kama si uzwazwa tuite nini?! Btw, hivi zaidi ya porojo za "Tanzania ya Viwanda" nikikuuliza utaje strategy za serikali kuhakikisha tunakuwa na Tanzania ya Viwanda unaweza kutaja mikakati ya serikali?! Hivi unaamini kabisa kuna mtu hakuwa na ndoto ya kuanzisha kiwanda lakini akaja kuwa inspired na Magu Administration kuanzisha kiwanda? Magu yule yule ambae amekaza kuua sekta binafsi?!
Halafu angalia ulivyo lofa! Eti ujenzi wa Vituo vya Afya umekamilika nchi mzima!! July mwaka jana PM anasema serikali imejenga vituo vya afya (ingawaje ki ukweli vingi ni zahanati tu) 108!
Sasa ikiwa ndani ya miaka 2 unusu serikali inadai imejenga vituo vya Afya 108, kwa akili yako unaamini ndani ya mwaka mmoja unusu serikali hiyo hiyo inaweza kujenga vituo vya afya kwenye kata zote zilizobaki! Au hujui Tanzania kuna kata ngapi?! Hebu jialimishe hapa:-
Kata kwa nchi nzima ziliongezwa kutoka 2,802 mwaka 2009 hadi 3,337, vijiji vikaongezeka kutoka 11,795 hadi 12,423 na mitaa ilitoka 2,995 hadi 3,741 huku vitongoji vikiongezeka kutoka 60,359 hadi 64,616.
Kwavile umeonesha wazi ni kilaza, wacha niishie hapa manake am sure hauna ubavu wa kushika yote nitakayoandika kwa maeneo mengine niliyoacha kuyaelezea!!