Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
-SGR
-NDEGE
-DARAJA
-FLYOVER
-BWAWA LA UMEME

Vipi haya?
-Ruzuku kwenye Kilimo
-Masilahi ya Wafanyakazi
-Ajira kwa vijana wanao maliza vyuo
-Upatikanaji wa maji salama.
-Afya bora kwa kila Mtanzania.
-Elimu bora kabisa kabisa
-Mazingira ya ufanyaji biashara Tz
 
Serikali inafanya vipaumbele vya viongozi na siyo vya wananchi,matokeo yake ndiyo hayo.
Watanzania tujiongeze,tunapotea njia.
 
Wazee wa fursa wameshamjua mzee wetu anapenda kusifiwa sasa Kila mtu atajitahidi hata akipewa dakika moja asifie hayo vilivyo..ingawa kweli Kuna mambo mzee anapaswa kusifiwa.
 
-SGR
-NDEGE
-DARAJA
-FLYOVER
-BWAWA LA UMEME

Vipi haya?
-Ruzuku kwenye Kilimo
-Masilahi ya Wafanyakazi
-Ajira kwa vijana wanao maliza vyuo
-Upatikanaji wa maji salama.
-Afya bora kwa kila Mtanzania.
-Elimu bora kabisa kabisa
-Mazingira ya ufanyaji biashara Tz
Ukiongea kinyume na malaika mkuu utaonekana mpinzani na ni msaliti. [emoji26] [emoji26]
 
Leo kwa bahati mbaya nilipata nafasi ya kuangalia TBC nikiwa ofisi moja uzinduzi wa ujenzi wa daraja kule Mwanza.
Hakika TZ imepiga about turn ya kufa mtu. Kawaida katika hafla za namna ile zamani nyimbo zinazoimbwa na kuchezwa ni za hamasa kwa taifa, sifa kwa Tanzania na umoja wetu.
Lakini Leo mwanzo mwisho ni sifa kwa Magufuli tuu. Sio kwaya, muziki hata kila hotuba ni sifa zake tuu huku anachekelea hata zile za kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Hivi wale wasifiaji na wao hawajisikii aibu?
 
Sijawahi kukuunga mkono kuwa Rais wa nchi hii (nimefanya kazi nawe nikiwa TANROADS kwa mantiki hiyo naamini nakufahamu pamoja na madhaifu yako).

Ulipoteuliwa na Chama chako kugombea Urais kusema ukweli nilihuzunika mno (by then nilikuwa mwanachama ila nilidhani CCM ingemteua yule Judge as he was the best among the lots of you).

Tumefanya kazi wote ukiwa Waziri wangu; wewe ni msimamizi mzuri mno ila ukiwa na mtu mzuri anaekuongoza (huna tofauti na umeme; ni mzuri ukiongozwa ila sio unapoongoza).

Naam; kuna wanaokushangilia kwa kila jambo; ila naomba utambue jambo hili. Lissu mmoja ni bora kwako mara elfu kuliko kina Polepole 1000.

Una access na information; ila UJUE sasa hivi wanaokupa information WANAKUDANGANYA kwa kuwa wanafaidika kwa wao kukupotosha.

Sijawahi kukuunga mkono lakini hata hivyo siamini kuwa ni akili yako (ninayoifahamu) ndio inayokufanya uamue unayoyaamua leo.

Mkuu: UNADANGANYWA. Maamuzi yako mengi tangu uingie madarakani yako based on wrong information. Inawezekana una nia njema; ila wanaokuzunguka na kukushangilia leo hii wanafurahia unapokosea.

Ni kweli kulikuwa na wezi na wasiolipa kodi awamu iliyokutangulia lakini si kila mfanyabiashara alifanya hayo. Unadhani kwa nini rafiki yako toka nchi jirani (na alikuwa anachukiwa na kila mtu serikalini) leo hii anakumbatiwa?

Sababu ni WEWE. MAAMUZI YAKO YANAWANUFAISHA WAO KULIKO SISI.
Mnamala; misha!!!
 
Mbona kichwa cha uzi na content iliyomo sijaona uwiano wowote mkuu. Ila ushauri na yaliyomo yako vizuri
 
Mh. Rais usilegeze kamba, bado kidogo tu unawamaliza. Hawa ni wezi wa rasilimali zetu
 
ukisikia nashindwa niandike nini ndo hapa sasa maana kichwa ni tofauti na kiwiliwili yaani namaanisha kwamba samaki na maji vimechanganyikana nashindwa tofautisha

Yaani namaanisha kwamba magugu na ngano vyote kwa pamoja wema na uovu huwa havitengani ukweli kidogo uongo kidogo

Yaani ni kwamba kila mtu atakwambia jambo fulani na mwingine atakwambia hivi

Tofauti kati ya + na - hesabu ına maana yake kusoma ni kuelewa na sı kufaulu ahsante kwa Uzi huu 🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi
Anafanya mengi mazuri sana,Kazi nzuri,ajitenge na ubaguzi wa kisiasa u vywama, atakua kiongozi bora wa nyakati zote.Mfano leo ktk uzinduzi wa kitaifa ujenzi daraja,kafanya nywema! Tatizo kamalizia kwa salamu kupongeza ccm chaguzi za Jafo na kumalizia Wapinzani wataendelea kuisoma namba!
 
Mfiaukweli, Bila shaka Mkuu utakuwa Mhanga wa kumba kumba za Magufuli Maana Uzi Wako umejaa huzuni na hoja dhaifu zinazokinzana na kichwa Cha Uzi.

Pole bhana Acha mzee ainyoshe nchi Mlizoea vibaya Sana hasa nyie TANROADS. Mlisababisha vifo vingi sana vya kina mama kwa kujenga barabara mnavyotaka.

Ngoja Tuendelee kuwasubiri wengine Awamu hii mtajitokeza Sana.
 
Hongera kwa kazi nzuri Rais wetu...panapobidi kusifia tufanye hivyo..lol
 
Back
Top Bottom