Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Ajira zilipatikana sekta zote za umma na binafsi.Sekta ya umma peke yake si chini ya elfu 35 Kila mwaka. (Udaktari,Ualimu,uhandisi,polisi,jeshi n.k)
 
Kila Kiongozi anastahili Pongezi katika mazuri aliyofanya pia kukosolewa ila sio kumdhihaki,kumsema hovyo au kumtukana.Kila awamu na Mambo yake..Tuongeze tu juhudi na kasi ya maendeleo.
 
Jk hakuwahi kulazimisha watu wakajiandikishe ili wapige kura bali watu walivutiwa na siasa safi iliyokuwepo kipindi hicho,,,,,,,,,,Magufuli afanye yake kujilinganisha na Jk ni sawa na mlima Kilimanjaro ulingane na kichuguu,,,,jk was the best hapana wa kumfata iwe mkapa hata magufuli
 
F
Kumekuwepo na vijembe na lugha za kejeli zinazotolewa na baadhi ya viongozi kutuhumu awamu zilizopita hasa awamu ya tano kana kwamba wao waliiba na hakuna maendeleo waliyoyafanya.

Orodha ni ndefu mimi nayakumbuka haya.

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
24. Kuvusha Umeme Zanzibar
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29. Ajira kila mwaka
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka
34. Aliwagomea CCM na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.
Hayo ni machache ya Mwamba Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa hakufanya chochote zaidi ya wizi na ufisadi walikuwa wanaishi nchi gani?

Hivi huyo wanaemtukuza amefanya jambo gani kubwa linalofikia hata robo ya mkubwa aliyoyafanya Kikwete?

Kwakuhitimisha Kikwete alifanya makubwa na Mikopo aliyokopa kila mmoja ananufaika nayo na vitu vinaonekana.

Naomba nawe utukumbushe Mambo makubwa yaliyofanywa enzi za Jakaya.

Tiririka .....
Naona mmeanza kasifiaa sabiri sindano ndo ipo inaingia tuliza kalio ndugu
 
Unalinganisha kwa mizani gani? Miaka minne kea miaka kumi?
Tuache ubabaishaji
Kasome deni la taifa la miaka minne ya jiwe halafu uje ulinganishe na deni la miaka 10 ya jk.halafu uludi hapa.
Kama hujatamani kukimbia nchi.
 
Kikwete Kilichomponza Ni Mtandao Uliojipenyeza Kwenye Serikali Yake Na Kutengeneza Corrupted Ruling System. Kwa Kuwapa Fadhira Waliomuweka Madarakani, Ndio Maana Alipambana Kumzuia Lowassa Kwenda Ikulu Ili Yasijirudie Yakwake.

All In All Aliyoyafanya Mazuri Ni Mengi Kuliko Mabaya Yake Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni"
Huo Mtandao uliomsumbua Kikwete ulikuwa wa Lowasa.Ulimsumbua kipindi chote Cha utawala wake.Akalipa kisasi kwa kumpiga chini Lowasa kiongozi wao na Magufuli akaja kupigilia msumari kwa kuusambaratisha uliokuwa umebakia serikalini na mashirika ya umma na vyama vya siasa ikiwemo CCM ,UKAWA akina chadema na CUF na ACT wazalendo
 
Kasome deni la taifa la miaka minne ya jiwe halafu uje ulinganishe na deni la miaka 10 ya jk.halafu uludi hapa.
Kama hujatamani kukimbia nchi.
JK hakukopa? Alichofanya ni nini zaidi ya kula bata majuu mpaka kuku wakaona wivu?

Halafu hela zinazokopwa zinaenda kwenye miradi ya maendeleo. Kama tunataka kwenda vizuri mikopo nayo lazima itumike vizuri.

Nina shaka kama huu ni muda muafaka wa kuanza kulinganisha. JK, kama Rais mstaafu ana heshima yake kubwa tu. Tuilinde. Hii milinganisho isije ikafungua makabati yenye siri
 
Nilishasema humu jf kama kinywa changu kiliwahi kumsema vibaya JK naomba Mungu anisamehe
Kikwete akisimama kutaka kugombea uraisi atapita bila kupingwa na chama chochote Upinzani hauwezi simamisha mgombea washashika adabu washamuomba samahani Sana mbona kuwa walimwonea awasamehe.

Kila sehemu Kikwete akiwepo anashangiliwa Sana na wananchi.
 
JK hakukopa? Alichofanya ni nini zaidi ya kula bata majuu mpaka kuku wakaona wivu?

Halafu hela zinazokopwa zinaenda kwenye miradi ya maendeleo. Kama tunataka kwenda vizuri mikopo nayo lazima itumike vizuri.

Nina shaka kama huu ni muda muafaka wa kuanza kulinganisha. JK, kama Rais mstaafu ana heshima yake kubwa tu. Tuilinde. Hii milinganisho isije ikafungua makabati yenye siri

Ukitaka kufungua makabati anzia JKN, AM, BWM na JK halafu uone kama kuna atakayebaki salama..
 
Tumenunua ndege
Stiglers
Korosho tumpandisha bei
Elimu bure

Mijamaaa mijinga sana
hakuna elimu bure Tanzania serikali inatoa ruzuku kwenye elimu tu. msituchoshe na viswahili vyenu vya kishamba
 
Maccm kazini yakichambua udhaifu wa Wenyeviti wao. Mkimaliza tuambieni pia ni nani mwibaji mzuri wa kura kati ya hao wawili
 
Wewe kweli ni kitomfyo...
sema kisukuma nikuelewe
jibu lako hili limakutosha
Jk hakuwahi kulazimisha watu wakajiandikishe ili wapige kura bali watu walivutiwa na siasa safi iliyokuwepo kipindi hicho,,,,,,,,,,Magufuli afanye yake kujilinganisha na Jk ni sawa na mlima Kilimanjaro ulingane na kichuguu,,,,jk was the best hapana wa kumfata iwe mkapa hata magufuli
[/QUOTE]
 
Walau nilikuwa mtu mzima wakati wa kikwete na sasa, sielewi hawa wanaoimba sana sifa za awamu ya tano wanaona miujiza gani ambayo haikuwahi kuwepo huko nyuma, binafsi naona Jk alifanya makubwa sana kwa awamu yake na kikubwa uchumi wana wananchi ulitengemaa sana kwa sabbu yeye alidili zaidi na kukusanya misaada toka nje kuliko huyu wa sasa, wananchi wenye kipato cha chini hawakusumbuliwa na kodi na pia alijitahidi kuruhusu uwekezaji kiasi ajira zilikuwa walau zinaonekna kuliko sasa, waalimu na udaktari ilikuwa ukimaliza unasubiri ajira lakini sasa hayo mambo yamepungua kama sio kwisha kabisa na wakati huohuo shule za binafsi zimeshaanza kuonja joto
 
Na kikubwa zaidi aliruhusu hoja mbadala na uhuru wa maoni, kuwa hata nikikosea muwe huru kunisema. Sasa huyu malaika wetu mkuu ambaye ana makosa LUKUKI KULIKO wote waliomtangulia yeye anataka asifiwe tu...
 
JK hakukopa? Alichofanya ni nini zaidi ya kula bata majuu mpaka kuku wakaona wivu?

Halafu hela zinazokopwa zinaenda kwenye miradi ya maendeleo. Kama tunataka kwenda vizuri mikopo nayo lazima itumike vizuri.

Nina shaka kama huu ni muda muafaka wa kuanza kulinganisha. JK, kama Rais mstaafu ana heshima yake kubwa tu. Tuilinde. Hii milinganisho isije ikafungua makabati yenye siri
Aliweza kuonge mshara kila mwaka,lakini sasa mnashindwa kufanyahivyo.
Matokeo yake mnajitangaza na makamera kuzindua miradi iliyotengenezwa na jk unaemsema alikua anakula bata.hovyo kabisa!!.
 
Back
Top Bottom