Yesu Kristo, muujiza wake wa kwanza Duniani ulikuwa ni kugeuza maji kuwa mvinyo na watu walikunywa na kufurahi. Hadi leo tunamkumbuka kwa tendo hilo.
Kabla hajaenda kuteswa na kuuwawa aliwaalika Mitume wake kwenye karamu ya mwisho.
Alitwaa mkate akaumega, akasali akasema twaeni mle wote, huu ndiyo mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu. Vivyo hiyo baada ya kula akatatwaa kikombe akashukuru akasema twaeni munywe wote, hiki ni kikombe cha Damu yangu, damu ya agano jipya la milele itakayomwagika kwa ajili yenu kwa maondoleo ya dhambi na ufufuko wa mwili. FANYENI HIVI KWA KUNIKUMBUKA MIMI.
Katika sala ya Bwana Tunasali. Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
Kwa maneno hayo utagundua kuwa Mwanadamu hitaji lake pekee la kumfanya amkumbuke Kiongozi wake ni kumfanya au kumwezesha apate chakula chake cha kila siku.
Makonda ameleta maendeleo makubwa mkoa wa DAR lakini pengine wanainchi wake wananjaa.
Hajaweza kuwaondolea njaa.
Watanzania hawajali maendeleo makubwa aliyoleta Rais Makufuli bali wanasikitika kukosa maisha ya kula na kusaza ya wakati wa Rais Kikwete.
Huenda Rais Kikwete akakumbukwa zaidi kwa sababu tu aliwaacha watu wakala na kusaza na akaifanya Serikali kuwa fukara.