Mahakama ilimkutaje Lissu ana kesi ya kujibu kwenye kosa lisilokuwepo Kisheria?

Mahakama ilimkutaje Lissu ana kesi ya kujibu kwenye kosa lisilokuwepo Kisheria?

Tujipe muda kidogo tusublie submission ya upande wa mashitaka nayo kwa sababu hayo ni maelezo ya Lissu kulingana na alivyo itafsiri sheria.Je ukiambiwa kile kikundi cha watu waliokua wamehudhuria kwenye ule mkutano wa hadhara pale mbinga ndo umma,au huko kote ambako utetezi ulipita kufafanua kauli mbiu yao ya no reforms,no election ndo vikundi vyenyewe vya watu?. Kubwa zaidi ni 29 october ndo itatia uzito.
Ushahidi wa October 29 ulikataliwa na mahakama ya Rufaa usitumike kwenye kesi hii maana wakati wa commital hauletwa na jamhuri. Hata kama ungeruhusiwa, hayo yalifanyika baada ya kesi kuanza. Utamshtakije mtu kwa jambo lililotokea wakati tayari kesi imeanza kusikiliza mahakama kuu. Pia akina DCI, IGP na CDF wakiitwa mahakamani wakakimbia, wao walikuwa na nafasi nzuri kufafanua namna uhaini ulivyofanyika.

Pia, Issue sio Umma, issue ni kosa lipo kisheria?. Sheria haijataja umma bali, kikundi au mtu binafsi. Sasa wewe unalazimisha umma iwe kwenye kosa. Lazima shtaka lioneshe kosa kisheria. Yani usijitungie kosa laki Bali lioanishe na Sheria inavyo sema.

Nikukumbushe, wakati kesi inaanza mahakama kuu, Lissu aliweka pingamizi ya kwamba shtaka halioneshi kosa la Uhaini, ila mahakama ikadai ya kwamba tuendelee na kesi tutajua huko mbele.

Halafu tujiulize, baada ya hiyo kauli ya Lissu huko mbinga, Mbeya na Jambo TV machafuko yalitokea instantly? Yani pale Mbinga watu walifanya fujo dhidi ya serikali? Au pale Jambo TV?
 
Nimefuatilia submission ya Lissu na nimeshangaa ya kwamba ilikuwaje mahakama ikaona Lissu ana kesi ya kujibu. Kosa analoshtakiwa nalo Lissu halipo kisheria hasa kwenye kosa la Uhaini. Jamhuri inamshtaki Lissu kwa kosa la kuchochea umma ili kuitisha serikali. Ila ukienda kwenye Sheria ya kanuni ya Adhabu kifungu/ Sec.39(2)(b) yenyewe inatambua uchochezi kwa mtu binafsi au kikundi cha watu.

Ina maana Jamhuri inadai Lissu alichochea umma wote wa Tanzania ili kuitisha serikali. Sasa swali langu inakuwaje mahakama ikadai Lissu ana kesi ya kujibu kwenye kosa lisilokuwepo Kisheria?. Kwa maana nyingine Lissu hakuchochea mtu au kikundi cha watu kama inavyosema. Jamhuri imemshtaki Lissu kwa kosa lisilokuwepo kwenye Sheria za Jinai za Tanzania.

Hili ni jambo la kutafakari sana kuhusu uhuru wa mahakama zetu Tanzania.
Mahakama na Majaji wetu ni wa kupigiwa simu moja tu (ROSTAM AZIZ)
 
Huwezi kuchochea Umma, that's is practically impossible

Umma ni Kila mtu.. yaani mtoto wa miezi 6, wagonjwa hospitalini, wakulima mashambani,.. yaani watu wote, haiwezekani kwa kuwa sio wote waliosikiliza speech hiyo..

Ila unaweza kuchochea kwa mtu mmoja, au kikundi Cha watu
Kikundi Cha watu hapa inamaana mnakuwa mna lengo Moja na mikakati
Na hili ndilo Lissu alilisema Jana. Ila naona Kuna baadhi ya watu hawataki kuliona uzito wake. Wamebaki kusema atanyongwa.
 
Tunasubiri submission ya Upande mwingine, Ila neno Umma ...maana yake ni Kila mtu katika eneo ..Sasa unaweza kuchochea Kila mtu ? Je Kila mtu alisikiliza hotuba hiyo kwa nchi nzima ?

Ila mtu au vikundi unaweza kuchochea na ile Sheria iliweka malengo hayo kwa kuwa uhaini unafanywa kwa Siri ..na washiriki ni baadhi tu ya watu (mtu au kikundi)

Ila ukichochea Umma, ambapo ni watu wote..Kunakuwa hakuna Siri Tena

Majaji watalinganisha ..
Issue ya October 29, wakina Katuga wanajaribu kuileta Mahakamani..ila kiufupi haipo.. Majaji hawatoi hukumu kwa kuangalia Tv, au magazeti..
Wanaangalia kilichopo mezani kwao na ushahidi kujitosheleza..

Unakumbuka Mwezi February 2026 Jamuhuri walitaka kuongeza ushahidi Mpya ukakataliwa? Ule ushahidi ulikuwa na mambo ya October 29 (picha na ripoti za uchunguzi)...walitaka kuweka mezani kwa Majaji ili waonyeshe kilichotokea.. ili kuongeza nguvu ya ushahidi wao
Kweli kabisa mkuu
 
Aliyeuwa watanzania 518 amepata hukumu gani Hadi huyo atakayemhukumu MTU mmoja apate hukumu kubwa?
Kuna watu kama Polepole na Nchimbi wamepotezwa watanzania wako kimya ndo huyo Lissu akinyongwa ndo watanzania wataamka?
Yeye ana nini zaidi ya hawa wanaouawa kila siku?
Hivyo shida sio Lissu ni watanzania kukubali uonevu kama sehemu ya maisha yao.
 
Hawezi kunyongwa

Watanzania wengi hawataki Lissu kunyongwa lkn
Wanataka afungwe miaka mingi kidogo japo 20+ ili
Kumtendea haki ya kufanana na Nelson Mandela
Tunajua Lissu anapenda sana kujifananisha na Nelson sasa kifungo ndio njia pekee ya kumfanya Tundu Lissu kuwa Nelson mpya
wa Singida
Kinyume chake yeye ni mpenda kula Ubwabwa tu kama wengine
🫎🫎🫎
 
Lissu ana nafasi ya kushinda, lakini sio rahisi.

Hivi ndivyo mahakama nyingi duniani huangalia kesi kama hii:

Kwa nini anaweza kushinda:

1. Sheria ya uhaini ni ngumu kuthibitisha. Duniani kote, lazima uonyeshe mtu alikuwa na mpango wa kutumia nguvu, silaha, au jeshi kupindua Serikali. Kusema kwenye jukwaa "hatutaingia uchaguzi bila mabadiliko" - hata kama ni kauli nzito - bado ni kauli. Mahakama nyingi huona hiyo ni uhuru wa kujieleza, sio uhaini.

2. Upande wa mashtaka umekuwa ukisuasua. Tangu Aprili 2025 kesi imeahirishwa mara nyingi kwa kisingizio "uchunguzi haujakamilika". Hiyo ndiyo ilifanya hata Jaji amwambie Lissu ajitetee, na ndiyo ilifanya UN iseme ni kesi ya kisiasa.

Kwa nini bado ni hatari kwake:

1. Tafsiri ya sheria Tanzania ni pana. Kifungu cha 39 cha sheria ya uhaini kina maneno "kuchochea uasi". Serikali inaweza kujaribu kusema "No Reforms, No Election" na kauli ya "tutaifanya nchi isitawalike" ni kuchochea wananchi wasitii mamlaka. Kama Jaji akikubali tafsiri hiyo pana, basi atapatikana na hatia.

2. Kesi za kisiasa huwa na shinikizo nje ya mahakama. Haijalishi hoja ni nzito kiasi gani, Jaji pia anaangalia mazingira.

Maoni yangu halisi:

Kama mahakama itaamua kwa sheria ilivyoandikwa kitabu, Lissu ana nafasi kubwa ya kuachiwa huru, kwa sababu Serikali imeshindwa kuleta ushahidi wa silaha, kikao cha mapinduzi, au mawasiliano ya kupindua nchi. Kauli pekee haitoshi kwa uhaini.

Lakini kama mahakama itaamua kwa tafsiri ya kisiasa ya "kulinda utulivu wa nchi", basi anaweza kupatikana na hatia.

Kwa kifupi: Hoja za kisheria ziko upande wa Lissu, lakini uamuzi wa kesi za uhaini mara nyingi sio wa kisheria tu.
 
Kesi ya kisiasa
Chuki
Hasara
Uonevu
Husuda
Misuse of power
Wajinga wachache waliopewa madaraka
Mahakama zinafuata Serikali inasema nini
Ingekua kesi km hizi majaji wanachukua rushwa ingekua ishaisha ila kwa sababu Serikali na wenye maamuzi huwamua uendeshaji wa kesi hizi za kisiasa basi tusubiri na kuona
Ndio maana sisi waislam tunaamini kuna hukumu siku ya hukumu. Yaani final submission. Wasiomini wanakuuliza umewahi kwenda ukarudi? Sasa mfano ushalawitia hapa duniani halafu mbabe anakwambia fanya unalofanya ndio basi tena? No
 
Nimefuatilia submission ya Lissu na nimeshangaa ya kwamba ilikuwaje mahakama ikaona Lissu ana kesi ya kujibu. Kosa analoshtakiwa nalo Lissu halipo kisheria hasa kwenye kosa la Uhaini. Jamhuri inamshtaki Lissu kwa kosa la kuchochea umma ili kuitisha serikali. Ila ukienda kwenye Sheria ya kanuni ya Adhabu kifungu/ Sec.39(2)(b) yenyewe inatambua uchochezi kwa mtu binafsi au kikundi cha watu.

Ina maana Jamhuri inadai Lissu alichochea umma wote wa Tanzania ili kuitisha serikali. Sasa swali langu inakuwaje mahakama ikadai Lissu ana kesi ya kujibu kwenye kosa lisilokuwepo Kisheria?. Kwa maana nyingine Lissu hakuchochea mtu au kikundi cha watu kama inavyosema. Jamhuri imemshtaki Lissu kwa kosa lisilokuwepo kwenye Sheria za Jinai za Tanzania.

Hili ni jambo la kutafakari sana kuhusu uhuru wa mahakama zetu Tanzania.
Kama Mahakama ikiona kuna mashaka kidogo ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka,huwa inatoa fursa kwa mshtakiwa kujitetea ili aweze kuondoa mashaka hayo.
Kwa mfano,kwenye kesi ya Lissu Mahakama ilisema kuwa kwa hatua ile haikulazimika kuchambua kwa undani ushahidi uliotolewa na waendesha mashtaka ili kumpatia fursa Lissu ajitetee kuhusiana na maneno aliyotamka ambayo anashtakiwa nayo.

Kwa kifupi Mimi niliielewa Mahakama kwa hatua iliyochukua kwa sababu ya yale maneno ambayo hata Lissu anakiri alitamka.Lengo ni kutoa fursa kwake kuondoa utata.
Na Lissu ameifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.
 
Tunasubiri submission ya Upande mwingine, Ila neno Umma ...maana yake ni Kila mtu katika eneo ..Sasa unaweza kuchochea Kila mtu ? Je Kila mtu alisikiliza hotuba hiyo kwa nchi nzima ?

Ila mtu au vikundi unaweza kuchochea na ile Sheria iliweka malengo hayo kwa kuwa uhaini unafanywa kwa Siri ..na washiriki ni baadhi tu ya watu (mtu au kikundi)

Ila ukichochea Umma, ambapo ni watu wote..Kunakuwa hakuna Siri Tena

Majaji watalinganisha ..
Issue ya October 29, wakina Katuga wanajaribu kuileta Mahakamani..ila kiufupi haipo.. Majaji hawatoi hukumu kwa kuangalia Tv, au magazeti..
Wanaangalia kilichopo mezani kwao na ushahidi kujitosheleza..

Unakumbuka Mwezi February 2026 Jamuhuri walitaka kuongeza ushahidi Mpya ukakataliwa? Ule ushahidi ulikuwa na mambo ya October 29 (picha na ripoti za uchunguzi)...walitaka kuweka mezani kwa Majaji ili waonyeshe kilichotokea.. ili kuongeza nguvu ya ushahidi wao
Ukisema umma wa Watanzania maana yake hata Rais,Makamu wake,Waziri Mkuu nk walichocheka.
Kwa kweli Lissu ana akili kubwa sana.
Hoja ya pili ni kuweka maneno "...kuzuia uchaguzi..." kwenye mashtaka.
 
Ukisema umma wa Watanzania maana yake hata Rais,Makamu wake,Waziri Mkuu nk walichocheka.
Kwa kweli Lissu ana akili kubwa sana.
Hoja ya pili ni kuweka maneno "...kuzuia uchaguzi..." kwenye mashtaka.
Hii ilitakiwa kuwa kesi ya Uchochezi na sio uhaini
 
Nimefuatilia submission ya Lissu na nimeshangaa ya kwamba ilikuwaje mahakama ikaona Lissu ana kesi ya kujibu. Kosa analoshtakiwa nalo Lissu halipo kisheria hasa kwenye kosa la Uhaini. Jamhuri inamshtaki Lissu kwa kosa la kuchochea umma ili kuitisha serikali. Ila ukienda kwenye Sheria ya kanuni ya Adhabu kifungu/ Sec.39(2)(b) yenyewe inatambua uchochezi kwa mtu binafsi au kikundi cha watu.

Ina maana Jamhuri inadai Lissu alichochea umma wote wa Tanzania ili kuitisha serikali. Sasa swali langu inakuwaje mahakama ikadai Lissu ana kesi ya kujibu kwenye kosa lisilokuwepo Kisheria?. Kwa maana nyingine Lissu hakuchochea mtu au kikundi cha watu kama inavyosema. Jamhuri imemshtaki Lissu kwa kosa lisilokuwepo kwenye Sheria za Jinai za Tanzania.

Hili ni jambo la kutafakari sana kuhusu uhuru wa mahakama zetu Tanzania.
Kangaroo Court
 
Back
Top Bottom