Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Mbumbumbu mnashindwa kutegua hii code [emoji28]
Huu ni mpango tu Eng Hersi Said Bado yupo sana Yanga
Wee nae unahaha na wasio husika, pambana na wazee wenu waliofungua Case khaaaah
Poleeeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee ninae mjua mimi ni mzee mpili hao wengine watafutwe tudili nao
20240615_154508.jpg
 
Wee nae unahaha na wasio husika, pambana na wazee wenu waliofungua Case khaaaah
Poleeeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
😅😅😅 Mbumbumbu mshaingia kwenye huu mtego.
Hapo hamna kesi,
Ila Eng Hersi Ana akili sana.
Tukiwapiga 8 tarehe 8 mtakuja kulaumu waamzi tena😅
 
Kuna namna naiona wachezaji hasa wa Simba na hasa wa kigeni kushawishiwa na timu ingine ili waifikirie hiyo timu.
CEO Masingisa was gone
Manara was gone
Chama is gone
Baleke is happy now
Innonga was not happy at the end
Sio maadili ya timu kuwashawishi wachezaji wa timu ingine wakiwa wanaitumikia timu yao
Ubaya Ubwela
Andika Kiswahili, Kingereza hukijuwi, Kingereza chako kinatia kinyaa .
 
Hao wazee, mawakili wao na yeyote aliyehusika kushauri au hata anyeonesha kufurahia uamuzi wa mahakama wakamatwe wapigwe kama ngoma mpaka wakiambiwa waseme ubwabwa wanasema wawa.

Cc
wasiojulikana
Rudisheni timu ya wazee, mmeteka timu, mmebebeba machawa kibao badala ya kuiimba timu mnaimba jina la mfanya biashara
 
Mimi binafsi nilihama Yanga sc mara baada ya kuona timu imeporwa kutoka kwenye mikono ya wazee wetu. Waasisi wa hii timu hawana tena thamani.

Naunga mkono huu uamuzi, Hersi Said na Ghaleeb watupishe hii sio timu ya familia ya kisomali na kiarabu.

Yanga Afrika ni timu ya waafrika.
 
Serikali ishajua kivuli chake ni simba na Yanga, ndo mambo yanayowapumbaza wananchi wake, baada ya Simba kutawala soka miaka minne ikaja zamu ya yanga, kwa mwendo wa eng hersi wanaona kabisa huyu anaweza kutawala soka hata miaka 10, makolo wapate depression waingie mtaani kama gen Z wa kenya, Bora wamtoe makolo wapate hata ahueni kidogo, and the circle goes on
Kalio huwa linakuwasha bila kuitaja Simba
 
Niwe muwazi tu Yanga kuna migogoro mikubwa sana ni vile tu hamuisikii kwenye media. GSM kapora haki zote za wanayanga.

Yaani wazee wa Yanga ni wa kupewa Supu na chapati mbili na buku mbilimbili za nauli ya daladala??

TUNATAKA YANGA YETU
 
KULWA NA DOTO ZA HAPA BONGO MAMBO YAO NI YALE YALE, AKIUMWA HUYU MWINGINE ANAPONA, ITAENDA WEE KIDOGO HUYU ATAANZA KUUMWA NA MWINGINE ATAPONA
kwa style hio mpira utaendelea bongo?🚮
 
View attachment 3044226

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne ( hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.

Source: #MillardAyoUPDATES
PIA SOMA
- Yanga: Mkutano na wanahabari tar 17.07.204

====

Source nyingine:
Wanachama wawili wa Yanga SC JUMA MAGOMA na GEOFREY MWAIPOPO walishinda kesi waliyofungua katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar mwaka jana mwezi Agosti. Kesi yao ilikuwa dhidi ya Baraza la wadhamini la klabu hiyo kuikabidhi klabu kwa mtu wasiyemjua wala asiyekuwa Mwanachama wakati kesi inafunguliwa mwezi Mei mwaka 2022 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa klabu uliomuweka madarakani Rais wa Yanga Eng Hersi Said. Awali walifungua kesi hiyo Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kinyerezi jijini Dar, kabla ya kushauriwa kuihamishia katika Mahakama ya Kisutu.

Walipinga kutumika kwa katiba ya mwaka 2020 ambayo ilitumika kwenye uchaguzi Mkuu uliouweka uongozi uliopo madarakani wakisema katiba hiyo sio halali. Inasemekana RITA waliitwa kutoa ushahidi na wakasema wanaifahamu katiba ya mwaka 2011 ambayo ipo ofisini kwao na hiyo ya mwaka 2020 hawaitambui.

Baada ya kupata hukumu yao mwezi Agosti mwaka 2023 JUMA MAGOMA NA GEOFREY MWAIPOPO wameona hakuna utekelezaji wa hukumu hiyo hata baada ya kuwasilisha kwa wahusika wakaamua kufungua kesi ya kukazia hukumu ambapo itatolewa maamuzi mwezi Agosti tarehe 5 mwaka 2024, ili hukumu hiyo ianze kufanya kazi. Ambapo inategemewa Mkutano Mkuu wa Yanga kuitwa ambao utajumuisha WANACHAMA WOTE HAI sio wawakilishi wa matawi pekee (kama ilivyo sasa) na kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu kwa kufuata katiba ya mwaka 2011.

Kama hili litatokea manake Eng Hersi na timu yake watakuwa wameondoshwa madarakani kwakuwa watakuwa wameingia isivyo halali.
View attachment 3044242
Nifah hukuwahi kuliona hili mamii? Maoni yako yakoje juu ya hii case?
 
Back
Top Bottom