Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Hii ni kesi ya mtego na aibu sio kwa mahakama ni kwa majaji wanaoisikiliza na kuiamua. Hii kesi ikiamuliwa basi itakuwa moja ya kesi za ajabu kuwahi kutokea katika vyumba vya mahakama; na aibu itakuwa kwa wale walioiamua.

Hii kesi inaweza kuleta aibu ya kudumu na ya kihistoria kwa majaji hao watatu. Inaweza kuja kuwa ni kesi "cheshi", kama ile ya "Kipenguria six" iliyowahukumu akina Jomo Kenyatta na wenzie watano kwenda jela maisha, enzi za ukoloni hapo Kenya. 😊

Sema tuu ile kesi, ilikuwa ya kikoloni, lakini ndio ilizua neno maarufu kama "Kangaroo Court", na mpaka sasa inatumika kama rejea kwenye mahakama na shule za sheria sababu iliamuliwa. 😊
unataka wahukumu unavyotaka wewe, tulia hao majaji wanajua wanachofanya mbona mnajiongelesha sana.
 
Katiga ana

Mashahidi kusema sikumbuki,sijui inategemea umewauliza nini na swali lako linalenga kitu gani.
Mahakama ina chaguzi mbili tu kwenye kesi ya uhaini ama mtu anyongwe au aachiwe hakuna adhabu ndogo .Katuga anarejelea kesi ambazo sio za uhaini kui guide mahakama kuwa mahakama inaweza kufanya maamuzi kwa kurejelea hizo kesi kitu ambacho no nonsense
Final submmision ya Likatuga anathibitisha Lisu si mhaini, bali Mungu aliwanyima maono kesi ya kumbambika.

Hata wanaobambikiwa kesi za murder huwa si lengo wanyongwe bali uhangaike na hiyo kesi miaka isiyopunguwa kumi ukiwa jela, sasa siku hizi kuna kesi zimewekewa muda maalum lazima ziishe.

Huu ndio ushetani anaoufanya pia Museven kwa Kiza Besigye.
 
SEHEMU YA 7.

Waheshimiwa Majaji, kiini hiki hakikupingwa wakati wa hoja za awali zilizofanywa mbele ya Mahakama hii.

Ilikuwa ni moja ya undisputed facts kwenye Preliminary Hearing iliyofanyika tarehe 22 September mwaka jana, ukurasa wa 133.

Mshtakiwa alikubali kwamba yeye ni raia wa Tanzania na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa Kifungu cha 198 CPA, Sura ya 20, iliyorekebishwa mwaka 2023, zoezi hili siyo la mapambo.

Jambo lolote ambalo litakuwa undisputed litakuwa limeingia kwenye orodha.

Haya siyo maneno ya Katuga, Waheshimiwa, bali ni Kifungu cha 198(4) kinachosema yale mambo ambayo hayana formal disputes hayana sababu, unless Mahakama ielekeze.

Kwa faida ya Kifungu cha 198, ileweke jukumu la Jamhuri: inatakiwa kuthibitisha kile ambacho kipo katika hati ya mashitaka.

Hoja ambayo imekataliwa kwenye Preliminary Hearing siyo kazi ya Jamhuri kuthibitisha hoja hiyo.

Waheshimiwa Majaji, tuhuma zipo kwenye hati ya mashitaka. Summary of evidence zilizopo katika Preliminary Hearing hazitengenezi tuhuma.

Hata zikiwa zimetengenezwa, ni kumpa Mshtakiwa kuzijibu au kuzikataa.

Kama anakubaliana nazo, linaingia katika Memorandum of Undisputed Facts, Waheshimiwa.

Ni segment ambayo zile summary ambazo ni Memorandum of Agreed Facts.

Summary of evidence haitengenezi tuhuma.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kumaliza hoja ya kwanza, ambayo imethibitika kwa Mshtakiwa kukubali kwake mwenyewe, Mahakama yenu tukufu inabaki na hoja mbili.

Waheshimiwa Majaji, neno Serikali katika Kifungu cha 39(2) limetumika neno Executive.

Hakuna tafsiri mahususi ya neno Executive wala Judiciary.

Tukisema Judiciary, unakuwa umemtishia nani, au Bunge?

The same to Executive, haionyeshi umemtishia nani.

Ukisoma Kifungu cha 39, hakijatumbia Serikali ni nani, ikabaki Serikali ni Serikali.

Ni sawa na hata neno Mahakama, ndiyo halijawa defined.

Waheshimiwa Majaji, ni msimamo wa sheria kwamba inapaswa kutafsiriwa kama ilivyo au kama inavyosema.

Na hii njia ya kutafsiri sheria inaitwa plain meaning.

Kesi ya Nassibu Abubakar Aziega Vs Jamhuri, Criminal Appeal Number 146 ya mwaka 2021, TanzLII July 2024.

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, ikikaa Mbeya.

Mahakama ya Rufaa ilirejea shauri la jinai la Mwesige Godfrey and Another Vs Jamhuri.
 
Hiyo ilikuwa mbinu ya majaji kuendelea kujipatia per diem zao za kutosha.

Kwa siku unakunja per diem ya 300,000 Tzs hata uwe wewe lazima ungesema kuna kesi ya kujibu.

Kufikia leo wamekunja sio chini ya Milioni 150 each.

Lakini kwa information iliyopo pale hakuna kesi ya kujibu maana ushahidi ulikuwa umepwaya vibaya sana hadi aibu kusema there is a case to answer.
Wakati kesi inaanza mliponda hivi hivi mwisho wa siku mwamba akakutwa na kesi ya kujibu ....ukimsoma Katuga kiufipa kweli utasema anapuyanga lakini ukimsoma kisheria anatumia vifungu kumjibu Lisu kuhusu hati ya mashitaka
 
Yaani anaiachia mahakama badala yeye aliyetumwa na CCM kuthibitisha hayo makosa mbele ya mahakama? Ama kweli hawa majaji wa CCM wanabebeshwa mzigo mzito sana!
Unajua mie nachoka kabisa, bafala wao waliofungua case waweke uthibitisho na ushahidi usio na shaka juu ya shauri lao. Eti wanawapa kazi mahakama iangalie makosa hayo km ni kweli ya kihaini au laah?

Huyu Katuga ni mzima kweli kichwani?
 

Attachments

  • Screenshot 2026-09-29 at 12.27.49.png
    Screenshot 2026-09-29 at 12.27.49.png
    1.3 MB · Views: 14
wanataka mahakama imkute na hatia ila adhabu isiwe ya kunyongwa na wamzuie kugombea Uraisi 2030 ndio mpango wao huo, read between the line ndugu yangu... Hio ndio mpango wao kwa sasa, I can clearly see and smell the rat, hii case inaenda all the way to Appeal court.
Nimeona point za Katuga linaelekea huko, Yule Mzee siku zote Yuko mbele ya muda, Ameshamalizana na hili Alisema hatakubali hukumu ya makosa ambayo hajashtakiwa nayo na aliyapinga kwa hoja na Sheria murua.

Pia Alisema hukumu ya uhaini haina kosa Dogo, ni Aidha uachiwe huru au uhukumiwe kunyonywa, nothing between.
 
Nimeona point za Katuga linaelekea huko, Yule Mzee siku zote Yuko mbele ya muda, Ameshamalizana na hili Alisema hatakubali hukumu ya makosa ambayo hajashtakiwa nayo na aliyapinga kwa hoja na Sheria murua.

Pia Alisema hukumu ya uhaini haina kosa Dogo, ni Aisha uachiwe huru au uhukumiwe kunyonywa, nothing between.
Katuga na maCCM wenzake wanajitekenya na kucheka wenyewe
 
Unajua mie nachoka kabisa, bafala wao waliofungua case waweke uthibitisho na ushahidi usio na shaka juu ya shauri lao. Eti wanawapa kazi mahakama iangalie makosa hayo km ni kweli ya kihaini au laah?

Huyu Katuga ni mzima kweli kichwani?
Amechanganyikiwa bula shaka, sio bure!
 
SEHEMU YA 6.

Miller Vs Minister of Pension (1947) Number 2 OER 372 to 373, kesi ambayo imerejewa with approval na kesi ya Sophia Seif Kingazi Vs Jamhuri, Criminal Appeal Number 273 of 2016, ambapo katika ukurasa wa 27 mpaka ukurasa wa 28, ambapo pia siyo kesi hiyo tu ilikuwa quoted.

Kwenye hiyo kesi ya Sophia ime-quote pia kesi ya Chandra Khant Joshubhai Patel Vs Republic of 1998, ambapo wakirejea maneno haya na yake.

Waheshimiwa Majaji, kesi hizi zote tulizo rejea zinaelekeza katika kutafsiri reasonable doubt. Mahakama isiwe strictly kwamba beyond reasonable doubt ilimaanisha beyond...

Mahakama ikijikita huko itakuwa ni tafsiri ya kuwaachia wakosaji dhidi ya jamii.

Sasa Waheshimiwa Majaji, baada ya kuangalia hili jukumu la kuthibitisha beyond reasonable doubt kwa tafsiri ya Mahakama zingine, twende tuangalie ni kitu gani sasa ambacho upande wa Jamhuri ulipaswa kuthibitisha.

Katika kuangalia huku sasa ni kuangalia viini vya kosa kwa hati ya mashitaka iliyo mbele yenu baada ya kuitoa katika Kifungu cha 39.

Kwa ridhaa yenu, tunaiomba Mahakama yenu ijiulize maswali yafuatayo:

1. Kwa mujibu wa mashitaka haya, iangalie kama Mshtakiwa ana utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Tunaiomba Mahakama hii ijiulize kama Mshtakiwa alitengeneza nia kwa ajili ya kuitishia Jamhuri.

3. Tunaomba Mahakama yenu ijiulize kama Mshtakiwa alidhihirisha nia yake ya kuitishia Serikali kwa kutoa na kusambaza maneno.

Haya ndiyo tunaomba Mahakama ijiulize.

Hivyo ndiyo viini vikuu vitatu.

Waheshimiwa Majaji, ukiangalia viini hivi haviendi mbali na viini vikuu katika kesi ya Hatibu Ghandi ambayo nimeshairejea.

Mahakama ya Rufani iliweza kuchambua viini vitatu.

Cha kunote kabisa, kesi hii ilihusisha Kifungu cha 39(2)(a) katika kesi ya Hatibu Ghandi.

Wakati mashitaka yetu yapo 39(2)(d), zote za Kanuni ya Adhabu.

Viini vilikuwa kama washtakiwa wana utii kwa Jamhuri ya Muungano, kama wali-form nia ya uhaini, na kama walidhihirisha nia hiyo by overt act.

Kwa hiyo Waheshimiwa Majaji, ukiangalia viini vilivyo tu, no tofauti na kesi hii.

Wakati wa Hatibu Ghandi, Mahakama ikijadili manifestation by overt act, wakati kesi iliyopo mbele yenu ni manifestation by deed.

Tunaomba Waheshimiwa mjiulize wakati tunaamua.
Deed na over act tulishamalizana nazo kwenye dictionary ya Oxford advanced learners na Black Law dictionary
 
Wakati kesi inaanza mliponda hivi hivi mwisho wa siku mwamba akakutwa na kesi ya kujibu ....ukimsoma Katuga kiufipa kweli utasema anapuyanga lakini ukimsoma kisheria anatumia vifungu kumjibu Lisu kuhusu hati ya mashitaka
Alikutwa na kesi ya kujibu sababu jamhuri ndio iliyoamua. Hakuna wa kuipinga.
 
Jamani sasa mbona hakuna updates? Au CCM wameweka mpira kwapani?

Yaani ukimsikiliza Tundu Lissu akitema nondo halafu ukamsikiliza huyu wakili wa CCM, ndugu Katuga, unaona kabisa ni kama ardhi na mbingu.

Tundu Lissu kamwaga nondo hadi maCCM wanatafutana. Hivi "a group of people" au "any person" ni sawa na public kweli jamani? Hata kama mtu hukuenda shule ndio ukubali kudanganyika kiasi hiki?
Ni aibu kwakweli.
 
Back
Top Bottom