SEHEMU YA 4.
Nassoro Katuga anaendelea:
Hata kwenye Penal Code kuna makosa ya neno “utter”.
Neno “utter” ni kitendo.
Kitendo cha kusudio lake nini?
“Utter” ni verb, haiwezi kusimama peke yake katika tafsiri ya sheria; it’s not a noun.
“By his deed of uttering.”
Kwa hiyo, tafsiri rahisi, kutoa maneno ni kitendo cha kutamka maneno.
Ndiyo maana kuna kosa linalotokana na uttering.
Kwa tafsiri ya sheria, uttering ni kitendo.
Waheshimiwa Majaji, tunalichukua hili kwa kuzingatia kwamba mens rea na actus reus ndiyo chanzo cha kosa.
Kifungu cha 89(1)(a) cha sheria, Kanuni ya Adhabu.
Shitaka limekamilika kwa kuzingatia mens rea na actus reus, kwamba kuna kosa la kutoa maneno.
Yapo makosa mengi ambayo ni ya kutoa maneno, hata vitisho.
Kama maneno ni kitendo, basi jibu ni ndiyo.
Hati ya mashitaka inasema pamoja na kutoa maneno, lakini aliyasambaza.
Waheshimiwa Majaji, kifungu cha 39 kimetumia “publication” kwa sehemu mbili.
Waheshimiwa Majaji, tafsiri ya “publish”, according to Oxford Advanced Learner’s Dictionary, inasema:
“Publish is to make known information to the public.”
Synonym, kwamba taarifa fulani ijulikane kwa umma.
Haya ndiyo maneno labda Mahakama hii Tukufu ingependa kujiuliza yalivyotumika katika hati yetu ya mashitaka.
Waheshimiwa Majaji, kwenye hiyo hiyo hati ya mashitaka Mahakama yenu ingependa kuyaona.
Kwa kifupi, yalilenga kuitishia Serikali, ukiangalia kuna kufunga na kufungua semi yalivyotumika.
Jukumu la kuchambua maneno yapi yalitishia Serikali katika maneno laki moja siyo dhumuni la kifungu cha 5.
Tumechagua maneno machache yanayotishia Serikali kati ya maneno mengi.
Waheshimiwa Majaji, swali la kujiuliza: Haya maneno ni sentensi zilizokamilika kuleta maana?